Category Archives: Shughuli za Kitaifa
RAIS KIKWETE AZINDUA KITUO CHA TAASISI YA KIMATAIFA YA KILIMO CHA KITROPIKI (IITA) DAR ES SALAAM
![]() |
| Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin William Mkapa wakionja mikate iliyotengenezwa kwa unga wa muhogo wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013. |
wakisikiliza maelezo ya kitaalamu juu ya utafiti wa maradhi ya migomba toka kwa Profesa Rony Swennen wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
![]() |
| Wadau wakiwa katika sherehe hizo |
Rais Kikwete awatkaa wanajeshi wanaokwenda DRC,kuilinda heshima ya Tanzania
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wanashuhudia.
PICHA NA IKULU.
RAIS KIKWETE AKIWA ARUSHA KUHANI MISIBA YA WALIOKUFA KATIKA MLIPUKO WA BOMU KANISA LA OLASITI
TAMKO LA RAIS KIKWETE JUU YA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU JIJINI ARUSHA
HOTUBA YA RAIS KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI JIJINI MBEYA
RAIS KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA HOSPITALI YA KAIRUKI, DAR ES SALAAM, LEO
wakiangalia watoto wachanga waliotunzwa katika chumba maalum muda mfupi baada ya kuzaliwa wakati Rais Kikwete alipotembelea sehemu mbalimbali
za hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki akiwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 25 ya kuanzishwa kwake leo Machi 16, 2013.
katika hospitali hiyo miaka 25 iliyopita leo Machi 16, 2013.PICHA NA IKULU.
Rais Kikwete azindua jengo la kitivo cha sayansi chuo kikuu cha kiislamu cha morogoro
![]() |
| Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro Mama Mwantumu Malale akiongea machache na kumkaribisha Rais Kikwete |
HOTUBA YA MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA UFUNGUZI RASMI WA JENGO LA KITIVO CHA SAYANSI KATIKA CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO (MUM),
TAREHE 14 MACHI, 2013, MOROGORO
Mzee Kitwana Suleiman Kondo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF);
Mheshimiwa Joel Bendera, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro;
Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro;
Profesa Hamza Mustafa Njozi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro;
Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na Jumuiya mliohudhuria;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Niruhusuni niungane na wenzangu walionitangulia kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa. Nakushukuru sana Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro na viongozi wenzako kwa kunialika kuja kujumuika nanyi katika siku hii adhimu ya ufunguzi wa jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro. Mmenipa heshima kubwa ya kuwa sehemu ya historia ya Chuo hiki. Kwa kweli, nimefarijika sana kuona Chuo chetu kinazidi kupata mafanikio ya kutia moyo hasa ukizingatia ukweli kwamba kina muda mfupi tu tangu kuanzishwa kwake.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Natoa pongezi nyingi kwako, Makamu Mkuu wa Chuo na wale wote walioshiriki kubuni wazo la kuwa na jengo la Kitivo cha Sayansi na kufanikisha ujenzi wake. Juhudi zao na moyo wao wa kupenda maendeleo ndio umetufanya sisi kujumuika hapa leo kushuhudia mafanikio haya. Hakika ni jambo la kujivunia. Pia, nawapongeza sana Wajenzi na Mhandisi Mshauri kwa kazi nzuri waliyofanya ya ujenzi wa jengo hili. Sote tunaliona jengo lilivyojengwa vizuri na kwa namna yake linapendezesha mandhari ya Chuo.
Kwa namna ya pekee napenda kwa niaba yenu nitoe shukrani zangu za moyoni kwa taasisi ya Al-Barakah kwa kufadhili ujenzi wa jengo hili. Asanteni sana kwa ukarimu wenu na upendo mkubwa mliouonesha kwa nchi yetu na watu wake. Naomba taasisi nyingine na watu binafsi waige mfano huu mzuri wa kusaidia miradi mbalimbali inayonufaisha jamii. Tukumbuke ule msemo wa wahenga kuwa “kutoa ni moyo, usambe si utajiri”.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Mabibi na Mabwana;
Kwa miaka mingi madhehebu ya dini na mashirika ya dini yamekuwa washirika muhimu sana wa Serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Yamekuwa yanajihusisha na kutoa huduma kwa jamii kama vile afya, elimu na nyinginezo. Kwa ajili hiyo watu wengi sana nchini wamenufaika na wanaendelea kunufaika na huduma zinazotolewa na mashirika ya dini.
Kwa miaka mingi mashirika na taasisi za madhehebu ya dini ya Kikristo ndiyo yaliyokuwa yakionekana kutoa huduma hizo. Kwa upande wa Waislamu, ukiacha Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan, mchango umekuwa mdogo sana. Ni jambo la faraja kubwa kuona Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF) ikionyesha njia. Kwa kumiliki na kuendesha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kwa ufanisi, MDF inatoa mchango muhimu katika kuendeleza elimu ya juu na maendeleo nchini. Idadi kubwa ya wanafunzi waliofuzu masomo yao na waliopo katika Chuo hiki tangu kilipoanzishwa mwaka 2005 ni ushahidi tosha wa kazi nzuri inayofanywa na MDF. Hongereni sana. Tunawaombea kwa Mola mpate mafanikio makubwa zaidi miaka ya usoni kwa upande wa elimu na huduma nyingine muhimu.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Katika kipindi cha miaka saba sasa, Serikali yetu imeongeza sana uwekezaji katika upanuzi wa elimu tangu ya awali hadi elimu ya juu. Tumeamua kufanya hivyo kwa sababu vijana wengi waliokuwa wanastahili kupata elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu walikuwa hawapati. Tanzania ni kubwa kuliko Kenya na Uganda kwa eneo na idadi ya watu lakini ndiyo tuliokuwa na idadi ndogo ya wanafunzi kwa ngazi zote hizo. Kwa mfano, mwaka 2005 idadi ya wanafunzi waliokuwa Chuo Kikuu nchini Kenya ilikuwa108,407, Uganda 88,360 na kwa baadhi ya nchi za SADC kama vile Afrika Kusini idadi hiyo ilikuwa 717,973. Wakati wenzetu wakiwa na idadi hiyo, sisi tulikuwa na wanafunzi 40,719 tu katika vyuo vikuu nchini. Hali ilikuwa hivyo pia kwa elimu ya sekondari. Kenya ilikuwa na wanafunzi 925,341, Uganda 619,519 na Afrika Kusini 4,186,882 wakati Tanzania ilikuwa na wanafunzi 524,325 tu waliokuwa katika shule za sekondari.
Tuliona hali hii haikubaliki hivyo tukaamua hatuwezi kuiacha iendelee. Tukaamua kudhibiti. Tukachukua hatua tulizochukua za kupanua elimu katika ngazi zote. Matokeo ya uamuzi huo ni kwamba vijana wanaopata fursa ya kupata elimu katika ngazi zote wamekuwa wengi kuliko wakati mwingine wo wote katika historia ya nchi yetu, tumewafikia na kuwapita majirani zetu. Kazi kubwa tunayoendelea nayo sasa ni kuwekeza katika kuimarisha ubora wa elimu waipatayo vijana wetu kwa kuongeza walimu, vifaa vya kufundishia, vitabu na huduma nyinginezo. Inshallah hata kwa dhamira yetu, hii njema Mola atatuwezesha. Mwanzo mgumu lakini hatma itakuwa nzuri.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Kufuatia juhudi hizo, idadi ya wanafunzi waliopo kwenye vyuo vikuu nchini imeongezeka sana, kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 166,484 mwaka 2012. Kwa upande wa sekondari mwaka 2011 tulikuwa na wanafunzi milioni 1.79 na wenzetu wa Kenya walikuwa na wanafunzi milioni 1.77. Haya ni mafanikio makubwa.
Serikali itaendelea kuwekeza kwenye upanuzi wa fursa za elimu na ubora wake. Hata hivyo ushiriki wa wadau wengine kuunga mkono juhudi za serikali ni jambo muhimu sana. Tumeweka mazingira mazuri kwa wadau hao kufanya hivyo na mafanikio yanaonekana wazi. Kama nilivyokwishasema awali, mashirika ya dini yamekuwa wadau wa kutumainiwa na mchango wao uko wazi. Unajieleza wenyewe. Kwa mfano, katika vyuo vikuu 49 vilivyopo nchini, vinavyomilikiwa na umma ni 14 tu. Vyuo vikuu 24 vinamilikiwa na mashirika ya dini na 11 na sekta binafsi.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa na muhimu unaotolewa na vyuo vikuu vinavyomilikiwa na mashirika ya dini na sekta binafsi. Ninyi mmekuwa washirika wazuri na wa uhakika katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya elimu katika nchi yetu. Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono na kushirikiana nanyi ili kuwawezesha vijana na Watanzania wengi zaidi waweze kupata elimu. Uamuzi wa kufanya utaratibu wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu uhusishe wanafunzi wa vyuo visivyokuwa vya umma ni moja ya mambo mengi muhimu yanayofanywa na Serikali kuthibitisha usemi wangu huo.
Tulipoingia madarakani mwaka 2005 tulifanya mambo mawili muhimu kuhusu mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Kwanza uamuzi kwamba, mikopo itolewe kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma na vile visivyokuwa vya serikali. Kabla ya hapo ilihusu vyuo vya umma pekee. Pili kwamba, kila mwaka tuongeze fedha zinazotengwa kwa ajili ya Mfuko huo ili idadi ya wanafunzi wanaonufaika iongezeke. Tulikuta Mfuko ukiwa na shillingi billioni 56.1 unanufaisha wanafunzi 16,345 mwaka 2005. Tukaongeza kila mwaka na katika mwaka huu wa fedha (2012/13) tumetenga shillingi bilioni 345 zinazowanufaisha wanafunzi 98,772.
Tutaendelea kuongeza fedha katika Mfuko huo ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike na hata ifikie siku moja tuweze kuwakopesha wote bila ya kujali sifa ya uwezo wa wazazi au walezi kulipa ada. Kwa kasi tuliyonayo na kwa jinsi tunavyozidi kufanikiwa katika kukusanya mapato ya serikali, naamini miaka michache ijayo tunaweza kufikia lengo hilo. Nawasihi Bodi ya Mikopo iwekeze katika kuimarisha uwezo wa kuwafuatilia waliokopeshwa kulipa mikopo waliyopewa. Matamanio yangu ni kuwa fedha zilizotolewa zizunguke ili tupunguze kiasi kinachotolewa na bajeti ya serikali kila mwaka.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Mabibi na Mabwana;
Niruhusuni nitumie nafasi hii kukupongeza wewe Mkuu wa Chuo, Makamu Mkuu wa Chuo, Wahadhiri na Jumuiya nzima ya Chuo Kikuu hiki kwa kazi kubwa na nzuri muifanyayo ya kuendeleza na kuboresha Chuo. Tumeshuhudia ujenzi wa jengo nililolifungua leo. Tumeona mafanikio kwa upande wa ongezeko la idadi ya wanafunzi, walimu, wafanyakazi na fani zinazofundishwa katika kipindi hiki kifupi cha uhai wa Chuo hiki.
Nimefurahishwa na kufarijika sana kusikia kuwa ubora wa elimu inayotolewa hapa chuoni ni jambo linalopewa kipaumbele cha kwanza. Jambo hili ni muhimu sana kulisisitiza kwani tunataka wahitimu wa Chuo hiki wafanane na wahitimu wa Chuo chochote kizuri nchini na hata duniani. Ningependa kuona wahitimu wa Chuo hiki wanagombewa katika soko la ajira. Hili ni jambo linalowezekana. Kinachotakiwa ni uamuzi wa Baraza na Seneti kuwa iwe hivyo na kuchukua hatua zipasazo. Sina shaka kuwa mnaweza kufanya hivyo. Hakika mnaweza, na sote kwa umoja wetu tunaweza.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Nimefurahi sana, pia, kusikia kuwa Chuo kinatoa mafunzo ya ualimu. Bila ya shaka mnaelewa kwa nini nafurahi. Tuna uhaba mkubwa wa walimu nchini hivyo Chuo cho chote kinachotoa mafunzo ya ualimu hunifurahisha. Endeleeni kuimarisha mafunzo hayo ili Chuo chenu kitambulike na kukubalika nchini kwa sifa ya kutoa walimu wazuri. Walimu wa kutoka Chuo hiki wawe wale wanaojua vyema masomo wanayofundisha, mahiri kufundisha na waadilifu. Naomba pia mtoe kipaumbele cha juu kwa mafunzo ya ualimu wa masomo ya sayansi na hisabati. Mkifanya hivyo, mtakuwa mnatoa mchango mkubwa katika jitihada za kupunguza uhaba wa walimu wa masomo hayo nchini. Naamini kitendo cha kuzindua Jengo la Kitivo cha Sayansi, kilichofanyika muda mfupi uliopita kinatoa matumaini ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kuchangia katika jitihada za kupunguza pengo la walimu wa sayansi nchini.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Nimewasikia mkieleza kwa ufasaha changamoto kubwa na ndogo ambazo Chuo inakabiliana nazo. Nawapongeza kwa dhati, wewe na viongozi wenzako kwa ubunifu wenu na hatua mnazochukua kuzikabili changamoto hizo. Nawaahidi msaada na ushirikiano wangu na wa serikali kwa yale yaliyoko kwenye uwezo wangu na wa serikali katika kutafuta ufumbuzi kwa changamoto zinazowakabili.
Nawapongeza kwa uamuzi wenu wa kutafuta vyuo vikuu rafiki vilivyoko katika nchi mbalimbali duniani mnavyoweza kushirikiana navyo. Endeleeni kufanya hivyo kwani vyuo vikuu vingi duniani hufanya hivyo. Hamtakuwa wa kwanza na wala hamtakuwa mnafanya jambo la kustaajabisha. Mnaweza, mkipenda, kuwaomba Mabalozi wetu waliopo katika nchi mbalimbali duniani wawasaidie. Ni wajibu wao kufanya hivyo kwani kusaidia kusukuma maendeleo ya hapa nchini kutoka huko waliko ndilo jukumu lao la msingi. Vile vile, nimefurahishwa na mipango yenu ya baadaye ya kuwa na matawi katika mikoa mbalimbali nchini. Hongereni kwa uamuzi wenu wa busara. Lazima Chuo kitanuke kwa maana ya kuwa kikubwa zaidi, makao makuu na kwa kuwa na vyuo vishiriki na shule au vitivo sehemu mbalimbali nchini.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Kazi iliyo mbele yenu ni kubwa, hivyo ni vyema kuweka mikakati mizuri na mipango thabiti ya utekelezaji na ufuatiliaji wa dhamira yenu hiyo njema. Rai yangu kwenu ni kuwaomba muwe wabunifu zaidi hasa katika kutafuta vyanzo vingine vya mapato vitakavyosaidia Chuo kujiendesha bila kutegemea ada peke yake. Chuo kiangalie uwezekano wa kufanya shughuli zitakazowaingizia mapato kama vile kufanya shughuli za kutoa ushauri. Pia muangalie uwezekano wa kuwekeza wenyewe kwenye miradi ya kiuchumi au kwa kushirikiana na wawekezaji katika baadhi ya maeneo.
Kuhusu nafasi mbili za ufadhili nilizopewa na Chuo kikuu cha Tun Abdul Razak cha Malaysia, nitafuatilia kujua kilichoendelea na kinachoendelea. Je, nafasi hizo bado zipo? Zikiwepo, nitawasiliana na wahusika waangalie uwezekano wa kuwapeni. Kama zimeshagawiwa basi tusubiri safari ijayo. Kwa masuala ya ardhi na maombi mengine nimeyasikia, yaleteni tuangalie namna ya kusaidiana.
Ndugu Makamu Mkuu wa Chuo, na
Wafanyakazi wote wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro;
Napenda kuwakumbusha kuwa mnayo dhamana kubwa na wajibu mkubwa na wa kihistoria. Ule ukweli kwamba ni mara ya kwanza kwa Taasisi ya Waislamu wazawa kuwa na Chuo Kikuu inawapeni wajibu maalum wa kuhakikisha Chuo kinafanikiwa. Ni mtihani na changamoto ya aina yake kuthibitisha kuwa Waislamu nao wanaweza kuwa na Chuo kizuri na chenye kutoa elimu ya ubora wa hali ya juu. Kwa sababu hiyo hamna budi kuhakikisha kuwa mna mipango mizuri ya kujenga Chuo cha hadhi na ubora wa hali ya juu. Ihakikishwe kuwa mipango hiyo inatekelezwa kwa ukamilifu.
Aidha jumuiya yote inao wajibu wa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, maarifa na weledi ili dhima hiyo ya Chuo iweze kutimizwa kwa ukamilifu. Timizeni wajibu wenu ipasavyo ili jina la Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro likue haraka. Sifa yake isambae na kuvuma kote nchini. Chuo kifanye vizuri ili wanafunzi waone fahari kuwa wahitimu wa Chuo hiki. Chuo ambacho, wazazi wapende kuleta vijana wao kuja kusoma hapa. Kwa jinsi Mkuu wa Chuo alivyoeleza, mimi nina imani mnaweza, fanyeni kweli.
Ndugu Wanafunzi wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro;
Naomba wote muone fahari ya kuwa wanafunzi katika Chuo cha kihistoria hapa nchini. Nawasihi mjitume kwa kadri ya uwezo na vipaji mlivyopewa na Mwenyezi Mungu mfanikishe kile kilichowaleta. Jifunzeni kwa bidii mfaulu vizuri ili mkihitimu muwe kielelezo kizuri cha mafanikio na ubora wa Chuo Kikuu Cha Waislamu cha Morogoro. Muwe Mabalozi na kioo cha ufanisi wa Chuo hiki. Nawasihi mjiepushe na mambo yatakayowapunguzia muda au kuwaondoa katika shughuli ya msingi iliyowaleta hapa ya kujifunza mpate digrii katika fani mliyochagua mwenyewe kuisomea. Vishawishi ni vingi na wapo watu wengi wanaopanga kuwashawishi mtumie muda wenu adhimu kufanya wanayoyataka wao ambayo mkishiriki huwatoa kwenye malengo na kutekeleza yao. Mambo ya dunia ya nje ya Chuo ni mengi huna budi kutambua lipi ufanye na lipi usifanye na kwa wakati gani!
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu ni mtu mzima, si mtoto. Lazima ujue kuwa unawajibika kwa kila unaloamua na kutenda. Amua kuwajibika vizuri. Fikiri kabla ya kutenda, changanua lipi ni lipi kabla ya kufanya uamuzi wa kile unachotaka kufanya. Wakati wote uongozwe na busara na hekima na siyo jazba na ushabiki wa matakwa ya kundi. Kama ni jema fanya na kama si jema usifanye. Kwanza tambua wewe ni nani na uko hapa kwa ajili gani. Lazima ujue kuwa hatma ya yote uko peke yako. Utafaulu au kufeli wewe. Utapata shahada wewe na si mtu mwingine. Hakuna ubia wa kufaulu au kufeli au kiwango cha kufaulu. It will always remain personal. Katika masomo unanufaika wewe. Shirikiana na wengi lakini usisahau kujali maslahi yako. Maslahi ya wengi yasiyojumuisha yako, yahoji vizuri kabla ya kuamua kushiriki au kufanya. Vinginevyo labda kama umeamua kujitoa muhanga, uwe shujaa. Hata kwa hilo, sijui utakuwa shujaa wa nani.
Mabibi na Mabwana;
Kabla ya kumaliza napenda kutambua na kumshukuru Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa na viongozi wa MDF kwa juhudi zao za pamoja zilizowezesha Chuo hiki kuwepo. Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru wananchi wanaokizunguka Chuo kwa ujirani mwema na wakazi wa Morogoro kwa ujumla kwa kukipokea vizuri na kuishi na wanajumuiya wa Chuo hiki kwa upendo mkubwa. Naomba muendelee na moyo na ushirikiano huo.
Baada ya kusema hayo, nawashukuru sana kwa kunialika. Nawatakia kila la heri na mafanikio tele.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, 28 FEBRUARI, 2013
Utangulizi
Ndugu wananchi;
Namshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kuwasiliana kupitia utaratibu wetu mzuri tuliojiwekea wa kufanya hivyo kila mwisho wa mwezi. Leo nimepanga kuzungumza nanyi mambo matatu; yaani Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Uhusiano wa Waislamu na Wakristo na Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne.
Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano wa
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
Ndugu Wananchi;
Tarehe 8 Februari, 2013 kule Addis Ababa, Ethiopia niliungana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Ban Ki-Moon, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Nkosozana Dlamini Zuma na viongozi wa nchi 12 za Afrika Mashariki, Kati na Kusini kutia saini Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na jirani zake. Pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zilikuwepo nchi za Burundi, Rwanda, Uganda, Sudani Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Angola, Zambia na Tanzania ambazo ni jirani ya Kongo. Nchi za Ethiopia, Msumbiji na Afrika ya Kusini pamoja na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zilitia saini kama wadhamini. Ethiopia kwa nafasi yake ya kuwa Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika na Msumbiji kwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Nchi wanachama wa Mkutano wa Ukanda wa Maziwa Makuu ziliwakilishwa na Uganda ambayo ni Mwenyekiti wake wa sasa. Afrika ya Kusini ilishirikishwa kwa kuwa taifa kubwa na linalotegemewa katika ukanda wetu.
Mpango huu ni jitihada nyingine ya kusaidia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ipate amani ya kudumu. Kama tujuavyo, tangu mwaka 1997 wakati wa vita vilivyosababisha kuondolewa kwa Rais Mobutu Seseseko mpaka sasa nchi hiyo rafiki na jirani haijapata amani na utulivu wa kudumu. Kumekuwepo jitihada na mipango kadhaa ya kuleta amani ambayo hata hivyo baada ya muda fulani machafuko hutokea tena na mipango hiyo kuvurugika. Inakadiriwa kuwa takriban watu milioni 5.4 wamepoteza maisha na watu wengi kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi yao. Pia kumekuwepo na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na mali nyingi kuharibiwa au kuporwa.
Ndugu Wananchi;
Machafuko yaliyoanzishwa na waasi wa Kundi la M23 mapema mwaka wa jana ndiyo sababu ya kuwepo kwa Mpango huu wa sasa tuliotia saini kule Addis Ababa, Ethiopia tarehe 8 Februari, 2013. Katika Mpango huo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na jirani zake, Tanzania ikiwemo, tumekubaliana kutokufanyiana vitendo vinavyohatarisha amani na usalama wa nchi zetu. Tumeazimia tusifanye hivyo ama moja kwa moja kama nchi au kwa kutumia watu wengine. Aidha, tumekubaliana tusiruhusu watu au vikundi vya watu kutumia nchi zetu kuhatarisha usalama wa nchi nyingine. Kimsingi tumekubaliana kuwa majirani wema. Katika Mkataba huo, majukumu ya kila nchi yameainishwa vizuri pamoja na yale ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mashirika ya Kikanda hususan SADC na ICGLR.
Ndugu Wananchi;
Niliamua kukubali kushiriki na kutia saini Mpango ule kwa kutambua ukweli kwamba sisi majirani wa nchi ya Kongo tunao wajibu wa kusaidia kwa kile tunachoweza. Wananchi wa Kongo wameteseka kwa muda mrefu mno hivyo kama Mpango huu utawasaidia kupata amani na usalama hatuna budi kuunga mkono. Ni kwa misingi hiyo hiyo, tulikubali kuchangia kikosi kimoja katika Jeshi la Kimataifa la kulinda amani huko Mashariki ya Kongo kama ilivyoamuliwa na Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu mwezi Julai, 2012. Uamuzi huo umeungwa mkono na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika. Umoja wa Mataifa umeamua Jeshi hilo liwe sehemu ya Jeshi la Umoja wa Mataifa la Kulinda Amani nchini Kongo (MONUSCO) jambo ambalo sote tumeliafiki. Tumepeleka walinzi wa amani Darfur, Sudan na Lebanon, kwa nini tusipeleke Kingo. Miaka ya nyuma tulishapeleka walinzi wa amani Liberia, Siera Leon na Eritrea.
Ni matumaini yetu kuwa Mpango huu mpya utatekelezwa kwa ukamilifu na kuzaa matunda yaliyokusudiwa. Kama nchi jirani, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yenye amani, usalama na utulivu ni jambo lenye maslahi makubwa kwetu. Ina maana ya kutokuwa na wakimbizi kutoka nchi hiyo, uharamia katika Ziwa Tanganyika kutokuwepo na ustawi wa shughuli za kiuchumi na kibiashara kwa upande wetu na wao. Ni chachu muhimu ya maendeleo ya Mikoa ya pembeni mwa Ziwa Tanganyika na Tanzania kwa jumla.
Uhusiano wa Waislamu na Wakristo
Ndugu wananchi;
Jambo la pili ninalopanga kulizungumzia siku ya leo ni uhusiano wa Wakristo na Waislamu hapa nchini. Kwa miezi kadhaa sasa tangu mwaka wa jana kumekuwepo na matukio kadhaa yanayosababisha mifarakano na kupandikiza chuki baina ya waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu. Matukio ya kauli na vitendo vya kudharau dini za wengine, kunajisi vitabu vitakatifu vya dini hizo, kuchoma moto nyumba za ibada na mzozo kuhusu nani achinje. Kumekuwepo na matumizi mabaya ya radio na simu za mkononi na mifumo mingine ya mawasiliano iliyoeneza maneno na ujumbe wa chuki na vitisho kwa waumini na viongozi wa dini zetu hizi kubwa hapa nchini. Kauli na matendo hayo, katika baadhi ya maeneo yamekuwa chanzo cha uhasama na magomvi baina ya waumini na hatimaye kusababisha vifo kama ilivyotokea Buseresere Mkoani Geita na Beit-el-Ras, Zanzibar.
Ndugu zangu;
Watanzania hatujawahi kuwa hivi, kumetokea nini? Miaka yote Watanzania ni watu tunaotambua na kuheshimu tofauti za dini zetu mbalimbali tunazoabudu. Watanzania ni waelewa na kwa ajili hiyo tumekuwa tunavumiliana kwa tofauti zetu na ndiyo maana tumekuwa tunaishi pamoja kidugu, kwa umoja na kushirikiana kwa mambo yote yanayotuhusu maishani isipokuwa wakati kila mmoja anapoingia kwenye nyumba ya ibada kumuomba Mola kwa misingi na taratibu ya dini yake.
Watanzania wa dini zote na makabila tofauti wanaishi nyumba moja, wanasoma pamoja, wanafanya kazi pamoja kwa udugu, upendo, umoja na ushirikiano. Kuna koo na familia zenye watu wa dini tofauti, wengine Waislamu na wengine Wakristo. Wapo Waislamu na Wakristo wameoana, wamezaa na wamejukuu na kila mmoja amebakia kuwa mfuasi wa dini yake. Wapo pia ambao hawakuoa lakini wamezaa watoto na wanashirikiana kulea watoto wao. Hayo ndiyo maisha ya Watanzania na hiyo ndiyo Tanzania yenye amani na utulivu tuliyozaliwa, kukua na kuishi. Nawasihi sana Watanzania wenzangu, tuienzi na kuidumisha tunu hii waliyotujengea mababu zetu.
Ndugu Wananchi;
Kuna wenzetu kwa sababu wanazozijua wao na kwa manufaa wanayoyajua wao wanataka kutuvurugia nchi yetu hii nzuri. Tusiwape nafasi wachochezi hawa kwani hawatutakii mema na wala hawazitakii mema dini zetu na nchi yetu. Sisi katika Serikali hatutasita kuwachukulia hatua wale wote wanaochochea chuki za kidini, wanaodharau vitabu vitakatifu vya dini nyingine na wanaokejeli dini nyingine.
Nimewakumbusha Polisi na mamlaka husika kote nchini wasifanye ajizi kwenye matukio ya namna hiyo. Wawachukulie hatua stahiki wale wote wanaohusika. Nimewataka wazingatie msemo wa Kiswahili usemao “ajizi nyumba ya njaa”. Wachochezi wa mifarakano na chuki za kidini wasipodhibitiwa ipasavyo wataleta maafa kwa Watanzania wasiokuwa na hatia. Nimewakumbusha Wakuu wa Wilaya na Mikoa kama walinzi wa amani wa maeneo yao ya uongozi, watimize ipasavyo wajibu wao. Pia nimewataka Polisi wakamilishe mapema upelelezi wa makosa ya vurugu za kidini na wahusika wafikishwe haraka kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine.
Ndugu Wananchi;
Naendelea kuwasiliana na viongozi wa dini kuzungumza nao juu ya wajibu wao maalum wa kuhakikisha kuwa wafuasi wao hawawi chanzo au sehemu ya tatizo na mifarakano miongoni mwa waumini wa dini mbalimbali nchini. Hali kadhalika naitumia nafasi hiyo kuwakumbusha umuhimu wa kuzungumza na wenzao wa upande mwingine kutatua tofauti au matatizo yanayoathiri uhusiano mwema baina yao.
Ndugu Wananchi;
Kuna msemo maarufu usemao “mjenga nchi ni mwananchi na mbomoa nchi ni mwananchi”. Naomba tuwe wajenga nchi na kamwe tusikubali kuwa wabomoa nchi. Hivi tukiibomoa nchi yetu tutakwenda wapi? Tutaishi wapi? Tusikubali kugeuka wakimbizi ndani ya nchi au nje ya nchi yetu.
Kwa mara nyingine tena, napenda kutumia nafasi hii kuwapa mkono wa pole makanisa, familia, ndugu na jamaa wote wa Mchungaji Kachila na Padri Mushi. Sote tunafahamu machungu waliyonayo kwa kuondokewa na wapendwa wao. Serikali na wapenda amani wote nchini wapo pamoja nanyi katika kipindi hiki kugumu. Vile vile natoa rambirambi zangu nyingi kwa waumini wote wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God na Kanisa Katoliki Tanzania kwa kuondolewa ghafla na viongozi wao. Tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu azipumzishe kwa amani roho za viongozi wetu. Amin.
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2012
Ndugu wananchi;
Tarehe 18 Februari, 2013 Baraza la Mitihani la Taifa lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne ya mwaka 2012. Wanafunzi 397,132 walifanya mtihani huo na kati ya hao, waliofaulu ni 126,851 yaani sawa na asilimia 34.5. Wanafunzi 240,903 ambao ni sawa na asilimia 65.5 hawakufaulu mtihani huo. Kwa ulinganifu, matokeo hayo ni mabaya kuliko matokeo mengine ya mtihani huo ya miaka ya hivi karibuni.
Mwaka 2011, jumla ya wanafunzi 336,782 walifanya mtihani huo na waliofaulu walikuwa asilimia 53.6 na ambao hawakufaulu kabisa walikuwa asilimia 46.4. Mwaka 2010 jumla ya wanafunzi 352,045 walifanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne, asilimia 50.4 ya wanafunzi hao walifaulu na asilimia 49.6 ya wanafunzi hawakufaulu.
Ndugu Wananchi;
Matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012, yameshtua na kufadhaisha watu wengi nchini na kwa sababu stahiki kabisa. Kwanza, kwamba kiwango cha kufaulu kimeporomoka sana, tena ghafla, kutoka asilimia 53.6 mwaka 2011 hadi asilimia 34.5 mwaka 2012. Hili ni anguko la asilimia 19.1 ambalo, kwa kila hali, ni kubwa sana. Pili, kwamba hata shule zinazofahamika kuwa na historia ya kufaulisha vizuri kama vile seminari, shule za watu binafsi, za mashirika ya dini na sekondari kongwe za Serikali ambazo hazina matatizo kama ilivyo kwa zile sekondari za Kata, nazo safari hii hazikupata mafanikio kama ilivyo kawaida yao. Nazo zimejikuta zikiwa na idadi ya vijana waliopata daraja la kwanza, la pili na la tatu ikipungua wakati waliopata daraja la nne na waliofeli wakiongezeka.
Isitoshe na kiwango cha ufaulu wa vijana umepungua pia. Mwaka 2010 wanafunzi 10 bora wote walikuwa wamefaulu daraja la kwanza la alama au pointi 7. Mwaka 2011 katika wanafunzi 10 bora wanane walipata daraja la kwanza kwa alama 7 na wawili alama 8. Mwaka 2012 katika wanafunzi 10 bora, watatu walipata daraja la kwanza kwa alama 9, watatu alama 10 na wawili alama 11.
Ndugu Wananchi;
Haya ndiyo mambo yanayozua maswali kwa watu wengi yanayohitaji kupatiwa majawabu ya uhakika. Kulikoni mwaka 2012? Ndiyo msingi wa uamuzi wa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, kuamua kuunda Tume ya kuliangalia suala zima la mitihani ya mwaka 2012 na matokeo yake. Hali hii haijawahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni. Ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu, hivyo lazima ukweli wake ujulikane kwa uhakika. Hii itawezesha Serikali na wadau wengine kuchukua hatua stahiki kurekebisha mambo mapema iwezekanavyo ili hatimaye mambo yawe mazuri siku za usoni. Tusipofanya hivyo mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi na lawama zinaweza kuwa kubwa zaidi kwa Serikali.
Ndugu Wananchi;
Hivi sasa kunatolewa mawazo lukuki kuhusu sababu za kwa nini matokeo yamekuwa mabaya. Wapo wanaodhani kuwa lipo tatizo katika utungaji wa mitihani, usahihishaji wake au kutoa maksi kwa watahiniwa. Wapo wanaodhani walimu hawawajibiki ipasavyo au baadhi yao kutokumudu masomo wanayofundisha. Wapo wanaofikiria kuwa wanafunzi hawako makini katika kufuatilia masomo na wazazi hawajali kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni. Wapo wanaoinyooshea kidole Serikali kwa sera, mitaala na uwekezaji usiokidhi mahitaji ya maendeleo ya elimu. Wapo wanaofikiria kuwa Serikali kushindwa kuongeza mishahara ya walimu kwa asilimia 100 kama walivyotaka imechangia. Orodha ni ndefu, ali mradi kila mtu ana mawazo yake. Na sisi katika Serikali hatuwezi kuwa tunadhani kwa sababu tunayo dhamana maalum. Lazima tujue ukweli kwa uhakika na ndiyo maana kuna umuhimu wa Tume. Naomba kila mtu mwenye mawazo yake ayafikishe kwenye Tume hiyo hapo itakapoundwa ili tupate jawabu muafaka la tatizo hili.
Ndugu Wananchi;
Napenda kuwahakikishia kuwa sisi katika Serikali tumetoa kipaumbele cha juu sana kwa elimu na kwamba hakuna upungufu wa utashi kwa upande wangu na wenzangu wote Serikalini. Ndiyo maana tumeguswa sana na matokeo haya. Bajeti ya elimu ya shilingi trilioni 3.6 ambayo ni sawa na asilimia 24 ya bajeti yote ya Serikali ndiyo kubwa kuliko zote. Kwa ajili hiyo imetuwezesha kuendelea kukabili mahitaji na changamoto za upanuzi mkubwa wa elimu ya sekondari na elimu ya juu. Bado hatujazimaliza changamoto zote na kwamba bado tuna kazi kubwa mbele yetu, lakini mafanikio yanaendelea kupatikana. Tutaendelea kutoa kipaumbele cha juu kwa elimu mpaka hapo itakapofikia mahali kwamba matatizo makubwa yatakapokuwa yamepungua sana.
Hitimisho
Ndugu Wananchi;
Mungu Ibariki Tanzania!
Mungu Ibariki Afrika!
Nashukuru kwa kunisikiliza!
RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JKT JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Rais Kikwete akagua Ukumbi mpya Wa Mikutano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam
Rais Kikwete afungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi
Rais Kikwete azindua utoaji wa Vitambulisho vya taifa katika viwanja vya Karimjee leo
rasmi mfumo wa usajili na utambuzi wa watu na utoaji wa vitambulisho vya taifa
uliofnyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Watatu kushoto
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi, kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu wa NIDA Bwana Mwaimu na kulia nia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwan Said
Meck Sadik.
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambukisho cha Taifa katika hafla ilkiyofanyika
katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Rais Mama Salma Kikwete kitambulisho chake cha Taifa katika viwanja vya
Karimjee leo huku Rais Kikwete akishuhudia.Kushot o Mkurugenzi Mkuu wa NIDA
Bwana Mwaimu
Mzee Ali Hassan Mwinyi kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee
leo.
Amani Abeid Karume kitambulisho chake cha taifa katika viwanja vya Karimjee
leo.
Benjamin William Mkapa kitambulkisho cha taifa katika viwanja vya Karimjee leo.
Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad kitambilisho cha Taifa katika viwanja vya
Karimjee leo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa mfumo wa usajili na utambuzi wa
watu.
kitambulisho cha taifa.
kitambulisho cha taifa.
Salaam Alhaj Elihad kitambulkisho cha taifa.
Professa Ibrahim Lipumba kitambukisho cha taifa.
Dkt.Ramadhani Dau kitambulisho cha taifa leo katika viwanja vya Karimjee.
Erio kitambulisho cha taifa.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifurahi na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw.William Erio mara baada ya kupokea Kitambulisho cha Taifa
Baadhi ya wageni walioudhuria sherehe za uzinduzi wa Vitambulisho vya Taifa kutoka kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN Bw.Gabriel Nderumaki,Mkurugenzi Mkuu wa NSSF DKt.Ramadhani Dau,Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw.William Erio na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw.Emanuel Humba
Picha na Freddy Maro wa Ikulu
RAIS KIKWETE KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI
![]() |
| Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanasheria leo Februari 6, 2013 katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini |
RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA LEO, PIA AKAGUA UJENZI WA DARAJA LA MALAGARASI
wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013.
MAMA SALMA KIKWETE AWASILI ARUSHA JIONI YA LEO ,TAYARI KWA KUFUNGA MKUTANO WA KIMATAIFA UNAOJADILI AFYA YA MAMA NA MTOTO
Arusha,Magesa Mulongo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)jioni ya leo,kesho atafunga mkutano wa
kimataifa juu afya ya mama katika ukumbi wa mikutano AICC.
wa Arusha,Mama Itanisa mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)jioni ya leo,kesho atafunga mkutano wa
kimataifa juu afya ya mama katika ukumbi wa mikutano AICC.
Arusha,John Mongela mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)jioni ya leo,kesho atafunga mkutano wa
kimataifa juu afya ya mama katika ukumbi wa mikutano AICC.
wa Arusha,Liberatus Sabas mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)jioni ya leo,kesho atafunga
mkutano wa kimataifa juu afya ya mama katika ukumbi wa mikutano AICC.
cha Msanja cha jijini Arusha , mara baada ya kuwasili kwenye uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)jioni ya leo,kesho atafunga
mkutano wa kimataifa juu afya ya mama katika ukumbi wa mikutano
AICC.
.jpg)
SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS JAKAYA KIKWETE
RAIS KIKWETE ATOA MILIONI 30 KWA MRADI WA KULEA NA KUHIFADHI MBWA MWITU KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI MKOANI MARA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametoa shilingi milioni 30 kuchangia mradi endelevu wa kulea na kuhifadhi mbwa mwitu waliokuwa wameanza kutoweka kabisa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.
Mhe. Rais pia amezishukuru na kuzipongeza taasisi za umma na binafsi zinazoshiriki katika kuufanikisha mradi huo unaojulikana kama Vodacom Foundation Serengeti Wild Dogs Conservation Project.
“Juhudi hizi za kurudisha tena makundi ya mbwa mwitu kwenye mbuga hii inayojulikana kimataifa ni ya kupongezwa kwani itahakikisha kwamba wanyama hawa wanaendelea kuwepo Serengeti na pia itaongeza idadi ya vivutio vyetu vya utalii mbugani humu”, alisema Mhe. Rais.
Aliyasema hayo Jumapili Desemba 23, 2012 wakati wa sherehe za kuachiwa huru kundi la pili lenye mbwa mwitu 15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo, lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.
“Nashukuru taasisi zote zinazounga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha kwamba mbwa mwitu wanakuwepo kwa wingi mbugani Serengeti kama ilivyo katika mbuga zingine”, aliongezea Mhe. Rais.
Katika taarifa yake wakati wa sherehe hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Tawiri, Dk. Simon Mduma, alimueleza Rais Kikwete kuwa jumla ya Mbwa mwitu ishirini na sita (26), wamerudishwa mbugani hadi sasa, kufuatia kundi la kwanza la wanyama mwitu hao kumi na moja (11) kuachiwa siku ya Alhamisi Agosti 30, 2012.
Alitanabahisha kwamba mradi huo unaohusisha mbwa mwitu walioondolewa katika msitu wa Samunge wilayani Loliondo ni mojawapo ya juhudi za kurudisha tena makundi ya wanyama hao katika mbuga hiyo maarufu duniani, na kwamba baada ya kuhifadhiwa na hatimaye kuachiwa kwao huku wakiwa wamevishwa collar maalumu zenye redio ili kufuatilia nyendo zao, ni muendelezo wa juhudi za kupata makundi sita yenye mbwa mwitu takriban kumi (10) kila moja, ikiwa ni hatua endelevu ya muda mrefu ya kuhakikisha uwepo wa wanyama hao mbugani humo.
Dkt. Mduma alisema kundi la kwanza la mbwa mwitu hao kumi na moja (11) wote wapo hai na wanaendelea vizuri katika maisha yao mbugani humo, na kwamba pamoja na wanyama hao kutembelea hadi maskani yao ya awali ya Loliondo, malalamiko ya kuwapo kwa uharibifu wa mifugo sehemu hizo kama ilivyokuwa awali hayajaripotiwa hadi sasa.
Mkurugenzi Mkuu huyo wa utafiti wa wanyama pori alieleza kuwa mbwa mwitu wamekuwa wakitoweka kutokana na kuuawa kwa sumu na wananchi baada ya kula mifugo yao, ama kwa kuugua magonjwa mbalimbali kama vile kichaa cha mbwa.
“Hivi sasa kuna makundi 11 yanayofuatiliwa, manane yakiwa Loliondo na matatu katika Hifadhi ya Ngorongoro, yakifanya idadi ya mbwa mwitu kuwa 200″, alisema Dkt Mduma.
Aliongezea kuwa awali, katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti makundi ya mbwa mwitu yalikuwa yakionekana kwa wingi, lakini yamekuwa yakitoweka kwa kasi sana kiasi hata mara ya mwisho ni wanyama mwitu hao wawili tu walioonekana katika mbuga ya Serengeti mnamo mwaka 1998.
Mbwa mwitu ni miongoni mwa wanyamapori ambao wapo hatarini kutoweka duniani. Takwimu zinaonyesha kuwa katika Bara la Afrika kuna mbwa mwitu takriban 8,000 na kwamba Tanzania pekee inakadiriwa kuwa na wanyama hao 3,500 katika mbuga mbalimbali nchini, isipokuwa katika Hifadhi h ya Taifa ya Serengeti ambako walianza kutoweka kabisa kabla ya juhudi hizi za kuwarejesha kuanza.
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imechangia dola za Marekani 450,000 kwa kipindi cha miaka mitatu ili kufanikisha mradi huo, ambao ulizinduliwa rasmi mwezi Julai mwaka 2011.
“Vodacom tunajisikia furaha sana kuwa sehemu ya juhudi za serikali katika kuimarisha sekta ya utalii ambayo kwa sasa mchango wake ni mkubwa sana kwa taifa”, alisema Bw. Salum Mwalimu, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom wakati wa sherehe za kuwarudisha mbugani mbwa mwitu hao 15.
Bw. Mwalimu alisema kampuni yake siku zote inalenga kubadili maisha ya watu na kwamba ni wazi kuimarika kwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti inayochangia kwa kiasi kikubwa sekta ya utalii nchini na ambayo inategemewa kwenye kuongeza pato la Taifa na ustawi wa watu ni jambo muhimu sana.
Taasisi zingine zinazoshiriki katika zoezi hilo ni Idara ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCCA), Frankfurt Zoological Society (FZS) , Grumeti Fund (GF) na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wawakilishi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ambayo imechangia dola za Marekani 450,000 kwa kipindi cha miaka mitatu ili kufanikisha mradi huo, ambao ulizinduliwa rasmi mwezi Julai mwaka 2011. kushoto ni meneja wa mradi huo Bw. Emmanuel Masenga wa Taasisi ya Utafiti wa wanyama pori (TAWIRI).


Mbwa mwitu wakirejea mbugani baada ya kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao 15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo, lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Bw. Joseph Kaboya, mhifadhi wa boma maalumu la mradi huo katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara, kwa kufanikisha zoezi hilo kwa mara ya pili. Kushoto ni meneja wa mradi huo Bw. Emmanuel Masenga wa Taasisi ya Utafiti wa wanyama pori (TAWIRI).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tawiri, Dkt. Simon Mduma (kushoto kwake) na meneja wa mradi huo Bw. Emmanuel Masenga baada ya sherehe hizo eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

RAIS KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUNZI 192 NA KUFUNGUA MAKTABA YA CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHO MONDULI LEO
RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA BOMBA LA GESI ASILIA KUTOKA MTWARA-DAR ES SALAAM
Rais Kikwete akagua miradi 19 katika wiki moja
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
6 Novemba, 2012
RAIS KIKWETE AZINDUA MIRADI YA BARABARA MANYONI-ITIGI-CHAYA na ISSUNA-MANYONI MKOANI SINGIDA LEO
RAIS JAKAYA KIKWETE ZIARANI JIJINI ARUSHA
Rais Kikwete azindua mradi wa kuboresha na kuendeleza miji ya Tanzania jijini Arusha
Mradi wa TSCP unalenga kuboresha huduma za msingi katika miji saba na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) kwa kujenga upya, kukarabati na kupanua miundombinu pamoja na kuijengea uwezo wa kukusanya na kusimamia mapato ya miji husika.
Aidha, chini ya TSCP, miji hiyo itajengewa miundombinu ya barabara zenye jumla ya kilomita 141.2, ujenzi wa madampo matano, ununuzi wa vifaa vya kusimamia taka ngumu, vituo vya mabasi sita, vituo viwili vya kuegesha malori na kilomita 15.9 za mitaro ya maji ya mvua.
Katika mji wa Arusha, kiasi cha barabara za lami zenye urefu wa kilomita 7.23 zitajengwa, mtaro mkubwa wa maji ya mvua wa mita 800 utajengwa, zitafungwa taa za kuongoza magari kwenye makutano ya barabara tatu ambazo ni Sokoine na Viwandani, Sokoine na Esso na Kanali Middleton na Makongoro. Katika awamu ya pili, kiasi cha barabara zenye urefu wa kilomita 7.8 zitajengwa katika Jiji la Arusha.
DMDP kwa ajili ya Jiji la Dar Es Salaam, itahusika wilaya zote tatu za Kinondoni, Ilala na Temeke na utagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 75.
Rais Kikwete amezindua miradi hiyo ikiwa ni shughuli zake katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku mbili kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Arusha. Rais amewasili Arusha mchana wa leo kutoka Dodoma.
RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA BARABARA YA KWA SADALA-MASAMA, WILAYANI HAI,LEO
RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI BARABARA YA MKUU ROMBO-TARAKEA
RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAZI KWA MAWAZIRI NA MAAFISA WAANDAMIZI WA SERIKALI
Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa
St Gaspar mjini Dodoma.
wanaokutana kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Pamoja naye meza kuu ni
Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali (kulia) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika
ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.
Rais Kikwete amteua Meja Jenerali Samuel Albert Ndomba kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Jenerali Raphael Mugoya Muhuga kuwa mkuu wa JKT
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete amemteua Meja Jenerali Samuel Albert Ndomba (pichani kushoto) kuwa Mnadhimu Mkuu
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Rais Kikwete amempandisha cheo Meja Jenerali Ndomba kuwa Luteni Jenerali. Taarifa
iliyotolewa leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012, mjini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais –
Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo unaanza leo.
hiyo ya Balozi Sefue imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Meja Jenerali Ndomba
alikuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahman A. Shimbo ambaye amestaafu Jeshi kwa mujibu
wa sheria baada ya kufikisha umri wa miaka 60.
kuwa Rais Kikwete amemteua Brigedia Jenerali Raphael Mugoya Muhuga (pichani kulia) kuwa Mkuu wa
Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012.
Rais Kikwete amempandisha cheo Brigedia Jenerali Muhuga kuwa Meja Jenerali. Kabla
ya uteuzi wake, Brigedia Jenerali Muhuga alikuwa Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
na:
Rais Kikwete azindua ujenzi wa Daraja la Kigamboni
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Daraja la Kigamboni katika hafla iliyofanyika huko Kurasini jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli na wapili kulia ni mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau.NSSF itatoa asilimia 60 za ujenzi wa daraja hilo na serikali itatoa asilimia 40
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akiongea na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni uliofanyika huko Kurasini jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck
Sadik
hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Daraja hilo ulofanyika Kurasini jijini Dar ea Salaam.
Rais Kikwete aweka jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Msata
Ndoto ya miaka mingi ya kujengwa kwa barabara ya Msata-Bagamoyo kwa kiwango cha lami imetimia leo, Jumanne, Septemba 18, 2012, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipoweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara hiyo katika sherehe kubwa iliyofanyika eneo la Kiwangwa.
Rais Kikwete aishukuru Vodacom kwa kuchangia katika mradi wa kuhifadhi mbwa mwitu Hifadhi ya Taifa ya wanyama ya Serengeti
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kuchangia katika mradi wa kuhifadhi mbwa mwitu katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mradi unaojulikana kama Vodacom Foundation Serengeti Wild Dogs Conservation Project, kwa dola za Marekani 450,000 kwa kipindi cha miaka mitatu.
Rais ametoa shukrani hizo Kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom hapa nchini Bw. Rene Meza, Ikulu Dar-Es-Salaam, walipokutana jana jioni, Ijumaa Agosti 31,2012
”Napenda kutoa shukrani zangu kwa Vodacom kwa msaada huu mkubwa, tunashukuru kwa jitihada zenu kubwa katika hili” Rais amesema.
Naye Mtendaji Mkuu wa Vodacom amemhakikishia Rais kuwa kampuni yake itaendelea kushirikiana na serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo, elimu na Afya.
“Tunajisikia faraja sana kuwa miongoni mwa washirika wa mradi huu. Ni heshima kwetu na tuko makini nao, tunataka kuendelea na mradi huu” Bw, Rene Meza amemhakikishia Rais.
Tayari mbwa mwitu kumi na Moja, wamerudishwa mbugani siku ya Alhamisi Agosti 30, 2012 baada ya kuhifadhiwa kwenye boma maalumu la mradi huo, katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.
Wadau wengine walioshiriki na kufanikisha zoezi hilo ni pamoja na Idara ya Wanyamapori, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCCA), Frankfurt Zoological Society , Grumeti Fund na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Kuachiwa kwa Mbwa Mwitu hao 11 walioondolewa katika msitu wa Samunge wilayani Loliondo ni mojawapo ya juhudi za kurudisha tena makundi ya wanyama hao katika mbuga hiyo maarufu duniani. Hivi sasa kuna makundi 11 yanayofuatiliwa, manane yakiwa Loliondo na matatu katika Hifadhi ya Ngorongoro, yakifanya jumla ya Mbwa Mwitu 200.
Mtafiti wa Magonjwa ya Wanyama kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyama (TAWIRI) Dkt. Ernest Mjingo, alimwambia Rais Kikwete kwamba katika Hifadhi ya Serengeti makundi ya Mbwa Mwitu yalikuwa yakionekana kwa wingi, lakini sasa yametoweka na mara ya mwisho Mbwa Mwitu wawili walionekana mwaka 1998.
Mtafiti huyo alisema Mbwa Mwitu wamekuwa wakitoweka kutokana na kuuawa kwa sumu na wananchi baada ya kula mifugo yao na kuugua magonjwa mbalimbali kama kichaa cha mbwa.
Dkt. Mjingo alisema baada ya kuachiwa Mbwa Mwitu hao, waliovishwa collar maalumu zenye redio, juhudi zitaendelea ili kupata makundi sita yenye Mbwa Mwitu takriban kumi kila moja, ikiwa ni hatua endelevu ya muda mrefu ya kuhakikisha uwepo wa wanyama hao mbugani humo.
Mbwa Mwitu ni miongoni mwa wanyamapori ambao wapo hatarini kutoweka duniani. Takwimu zinaonyesha kuwa katika Bara la Afrika kuna Mbwa Mwitu wanaofikia 8,000 na Tanzania pekee inakadiriwa kuwa wanyama hao 3,500 katika mbuga mbalimbali nchini. Katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti walitoweka kabisa kabla ya juhudi hizi za kuwarejesha kuanza.
HOTUBA YA MHESHIMIWA DK JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI KUHAMASISHA SENSA YA WATU NA MAKAZI, TAREHE 25 AGOSTI, 2012
RAIS KIKWETE AZINDUA AWAMU YA TATU YA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF III) KATIKA UWANJA WA JAMHURI,MJINI DODOMA LEO
RAIS KIKWETE AWAAPISHA WATENDAJI WAKUU WA MAHAKAMA LEO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wapya wa Mahakama ya Tanzania, mara baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Ombeni Sefue, Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Mhe. Ignas Paul Kitusi, Msajili Mkuu wa Mahakama na Mhe. Panterine Kente, Msajili wa Makahama ya Rufani.
KEYNOTE ADDRESS BY HIS EXCELLENCY JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, AT THE OFFICIAL OPENING OF A SPECIAL CABINET RETREAT ON TRANSFORMATION OF GOVERNMENT DELIVERY SYSTEMS, 4-5 AUGUST, 2012, DODOMA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua warsha kuhusu mfumo wa kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa mawaziri, makatibu wakuu na wakuu wa taasisi za serikali leo Agosti 4, 2012 katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua warsha kuhusu mfumo wa kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa mawaziri, makatibu wakuu na wakuu wa taasisi za serikali leo Agosti 4, 2012 katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.
Waziri katika ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia Mhe Idris Jala akitoa mada ya utangulizi katika warsha kuhusu mfumo wa kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa mawaziri, makatibu wakuu na wakuu wa taasisi za serikali leo Agosti 4, 2012 katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.
Washiriki wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua warsha kuhusu mfumo wa kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa mawaziri, makatibu wakuu na wakuu wa taasisi za serikali leo Agosti 4, 2012 katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma
Washiriki wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua warsha kuhusu mfumo wa kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa mawaziri, makatibu wakuu na wakuu wa taasisi za serikali leo Agosti 4, 2012 katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wakuu wa serikali pamoja na wawezeshaji kutoka Malaysia baada ya kufungua warsha kuhusu mfumo wa kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa mawaziri, makatibu wakuu na wakuu wa taasisi za serikali leo Agosti 4, 2012 katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.
Your Excellency Dr. Mohammed Gharib Bilal, Vice President of the United Republic of Tanzania;
Your Excellency Dr. Ali Mohammed Shein, President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council;
Honourable Mizengo Kayanza Peter Pinda, Prime Minister of the United Republic of Tanzania;
Honourable Anne Makinda, Speaker of the Parliament of the United Republic of Tanzania;
Honourable Dato’ Sri Idris Jala, Minister and Chief Executive Officer of the Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU), Prime Minister’s Office, Government of Malaysia;
Honourable Ministers;
Ambassador Ombeni Sefue, Chief Secretary and Head of Public Service;
Dr. Abdulhamid Yahya Mzee, Chief Secretary, Zanzibar;
Permanent Secretaries;
Distinguished facilitators from PEMANDU;
Ladies and Gentlemen;
I am pleased to welcome you all to this unique seminar on Transformation of Government Delivery Systems. To you Dato’ Idris Jala and the entire team from Malaysia and the United States, I say welcome to Tanzania and welcome to Dodoma. In a very special way let me sincerely thank the government of Malaysia for allowing you and your colleagues to come and share with us the experience of Malaysia. I also commend Dr. Philip Mpango, the Executive Secretary of the Planning Commission and his staff for organizing this important Seminar so well. To all my fellow participants may you realize that this is a rare opportunity for us so we must utilize well.
Ladies and Gentlemen;
The idea of holding this Seminar was conceived in May 2011 during my participation at the Langkawi International Dialogue that took place in Kuala Lumpur, Malaysia. It was during that meeting the Malaysian government shared with Heads of State and Government attending the meeting, two of their development models. These were the Government Transformation Programme (GTP) and the Economic Transformation Programme (ETP). All of us were fascinated by these models and wanted to learn more about Malaysia’s experience, particularly its delivery systems. The idea hidden behind the minds of all of us was the wish to learn more about these models and see how to emulate their good examples.
The government of Malaysia accepted our request and organized a special seminar in November 2011 on the Big Fast Results (BFR) approach. They invited senior officials from different countries of the Smart Partnership Movement to participate. We sent a delegation led by Dr. Phillip Mpango, the Executive Secretary of the Planning Commission, to attend the Seminar. Indeed, the delegation came back home excited and eager to see our government use the BFR methodology to help us perform better in the discharge of our responsible.
It is worth mentioning that the Prime Minister of Malaysia did a special favour to me when he agreed to allow Dato’ Idris Jala to give Tanzania extra tuition after the general briefing to all Heads of State and Government. It was during this private session that I requested Dato’ Idris Jala to come to Tanzania and conduct this seminar to my Cabinet and other senior government officials. It is heartwarming, indeed, that we have him and his powerful team with us this morning.
On return from the November, 2011 seminar, Dr. Mpango and his team began preparations for this seminar. They worked tirelessly with PEMANDU and Mckinsey to develop ideas and concretise the preparations of holding this seminar. This event today, therefore, is the outcome of the tremendous efforts of the Planning Commission of Tanzania and PEMANDU of Malaysia. Personally, I have been anxious to see this seminar is held because I thought what I learnt in Malaysia was worth sharing with the top echelons of my government. I believe learning the ABCs of Big Fast Results approach will interest all of us gathered here and inspire us to do better.
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
Many of you here may know that at our independence in 1961, the per capita income of Mainland Tanzania was about the same level as that of India and Pakistan. More interesting, our economic structure was generally similar to that of India, Pakistan and to some extent that of Malaysia. The economies of all the four countries were characterized by heavy dependency on agriculture. For example, in Tanzania the contribution of agriculture to GDP was 59 percent, Pakistan 45 percent, India 42 percent, and Malaysia 36 percent. The share of manufacturing sector in each of those four countries was less that 15 percent of GDP.
After 50 years, one can no longer compare Tanzania with those other three countries. They have just moved too many steps up the ladder of socio-economic transformation and development. While Tanzania remains undeveloped, heavily depending on agriculture with a low per capita income of US dollar 550, India, Pakistan and Malaysia have transformed their economies to remarkable levels. They have become highly industrialized and the share of agriculture has diminished significantly although it remains highly productive. These countries are big exporter of food and manufactured goods.
With regard to Malaysia, her story is even more fascinating. The country has been transformed incredibly from a commodity-based economy focusing on rubber and tin at independence in 1957 to one of the world’s largest producers of electronics and electrical products. They make cars and military hardware including sub-marines. Malaysia is now a high middle income, export-oriented economy with per capita income close to US dollar 10,000. Their target now is to become a developed country by 2020. Coming from such humble beginnings to what it is today gives us inspiration that we too can make it. That is why I felt learning their examples particularly about how they made it relevant to our country.
Ladies and Gentlemen;
Since 1961 Tanzania’s political leadership both on the mainland and Zanzibar have demonstrated strong political will to see their country develop fast. They identified poverty, disease and ignorance as the most critical challenges to the country’s development. Indeed, deliberate and focused efforts have been made in order to overcome these challenges. Immediately after the independence the government launched the first development plan for 1961-1964 and later made a longer development plan of 15 years (1964-1980), divided into three equal implementation periods of five years.
Some of you will recall that the implementation of the first two phases were encouraging, but the third phase between 1975-1980 was heavily disrupted by various challenges of the time including drought, fuel crisis and disintegration of the East Africa Community. On top of that, the government was also forced to divert the resources from the development activities to protect the country’s territorial integrity during the Idd Amin invasion in 1978. Later in the mid 1980’s and early 1990’s, in response to the deteriorating economic situation, a major economic shift was made by introducing a market-oriented economy.
Ladies and Gentlemen;
Despite the many challenge encountered in our past planning initiatives, in 1994 the government started the preparations of another long term national development vision whose objective was to help lift millions of Tanzanians out of poverty. Subsequently it meant making the country graduate into middle –income country by 2025.The work of preparing the new national development framework was completed in 1999 and the new blue print document that builds on the National Strategy for Growth and Poverty Reduction as well as sector specific programmes was launched.
As you will recall, in 2008 I established the Planning Commission. Among the major tasks I directed it to do was to undertake a comprehensive review of the Vision 2025 and develop structured systems of guiding its implementation. The Commission dutifully obliged. They came up with both a Reviewed Vision 2025 and proposal for a long Terms Development Plan divided into three phases of five years each. In June, 2011 we launched the first of the three Five Years Development Plan covering the period 2011/12 – 2015/16. The main objective of this plan is to remove obstacles to growth and unleash Tanzania’s latent growth potentials.
Ladies and Gentlemen;
Our persistent efforts and commitment have enabled us to post modest progress, especially at the macro-economic level: macro-economic stability has been preserved; expenditure on social services has increased; exports and foreign currency reserves have increased; FDI flow has increased; inflation has been kept in check despite current challenges. We have enjoyed relatively high economic growth rates over the past decade and a half. We have registered a modest increase of per capita income. However despite the encouraging progress we still have long ground to cover as poverty remained a major challenge. Many people still live below the poverty line.
In my view strengthening government delivery systems d improving the performance of the private sector and the individual farmer and worker is the answer. We would be able to adequately translate our wishes inscribed on the many papers and documents into concrete results that would change lives of our people and our nation. Learning from examples of friends who not long ago were at our level could be useful. That is why we have invited our Malaysian friends to come and tell us their story of success and learn from their good examples.
Excellencies;
Ladies and Gentlemen;
This Seminar is intended to do that. I would like it to be a turning point towards a journey where plans are effectively implemented. Where performance will be measured against clear and concrete deliverables. Let it be a journey of hope that will ensure the first five year development plan and indeed the long-term dream of Vision 2025 is realized in a timely manner. It is a journey of entrenching accountability that will see us move beyond planning and focus more on implementing what we have agreed to do in order to realize socio-economic transformation and development of our country. A journey that we must all embark today and lead Tanzanians and their great country to momentous victory in the fight against underdevelopment, hunger, poverty and deprivation.
Distinguished Participants;
This requires of us all to read all our major national development frameworks including the first five year development plan of 2011/ 12 – 2015/16 and the Vision 2025. We should fully understand the thrust and priorities contained in those frameworks. We must align policies and our sectoral budgets to the objectives of the major national development frameworks. There should be unity of purpose, because all of us are working towards a common goal. But all these efforts would be meaningless if our follow up mechanisms and delivery systems remain weak.
A strong delivery system is a key element to sustainable improvement and development. A weak delivery system breeds a poor service delivery to the public and makes it difficult to break the poverty cycle. In this regard, the time has come for Tanzania to formulate sound delivery frameworks and hold political leaders and top executives responsible for their failures. Perhaps this Seminar is a good starting point that will enable us to develop a forceful follow up mechanism. I therefore implore all of you here to be attentive throughout the Seminar and learn the new tested approaches of delivering high quality services to citizens and develop a nation from poor to developed. Engage facilitators, seek clarification and also share your own experience and frustrations. There is a lot to learn and improve upon.
Excellencies;
Distinguished Guests;
Ladies and Gentlemen;
In conclusion, I want to thank once again the government of Malaysia for accepting our invitation and agreeing to send Honourable Jala and his team. I also thank the Planning Commission for excellent arrangements of the Seminar. We are now ready to listen, learn and be converted. I look forward to a successful Seminar.
Thank you for your kind attention.
=============================
WELCOMING REMARKS BY AMBASSADOR OMBENI SEFUE, CHIEF SECRETARY OF THE GOVERNMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DURING THE WORKSHOP ON TRANSFORMATIONAL LEADERSHIP FOR EFFECTIVE AND EFFICIENT GOVERNMENT DELIVERY ON THE TANZANIA DEVELOPMENT VISION 2025
ST.GASPAR’S CONFERECE CENTRE, DODOMA
4-5 AUGUST, 2012
RAIS KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO LA TATU LA JUKWAA LA UHUSIANO WA CHINA NA AFRICA KATIKA KUPUNGUZA UMASKINI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika lenye lengo la kuondoa umaskini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam July 28, 2012.Wa tatu toka kushoto ni Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian, wa pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya rais Mhe Steven Wassira, wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Maendeleo ya Uchumi wa Sierra Leone Mhe Momodu Kargbo, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Mipango Dkt Philip Mpango na kulia kabisa ni Balozi wa China hapa nchini Mhe L.V. Youqing.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ufunguzi wa Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam July 28, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian baada ya ufunguzi wa Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika lenye lengo la kuondoa umaskini,ufunguzi huo ulifanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam July 28, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian(kuhsoto) na Balozi wa China hapa nchini Mhe L.V. Youqing. baada ya kufungua Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe toka china unaohudhulia Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini,lililofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam July 28, 2012.PICHA NA IKULU.
RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA KARAKANA (HANGA) YA NDEGE ZA SHIRIKA LA NDEGE LA PRECISION AIR
| Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Precision Air Bw Michael Shirima wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere tayari kwa uziduzi wa Karakana wa ndege za kampuni hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw Alfonce Kioko, katikati ni Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik |
![]() |
| Mkurugenzi wa Hoteli ya Kibo Palace ya Arusha Bw Vicent Laswai naye amehudhuria katika uzinduzi huo kama mdau wa Utalii.Picha zaidi Bofya Hapa. |
MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM
Rais Kikwete azindua mradi wa maji jijini Mbeya
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Kamishna wa Maendeleo katika Jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs(wapili kushoto), balozi wa jumuiya ya ulaya nchini Cerian Philberto Sebregondi(kushoto),Balozi wa Ujerumani nchini Klaus Peter Brandes na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakikata utepe kuzindua rasmi mradi wa maji safi na mazingira Mjini Mbeya leo mchana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Kamishna wa Maendeleo katika jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs wafunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa MRADI WA MAJI SAFI na usafi wa mazingira katika eneo la Swaya mjni Mbeya leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Kamishna wa Maendeleo Jumuiya ya Ulaya Andris Piebalgs(Watau kushoto) na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakikagua chanzo cha maji eneo la Swaya mjini Mbeya wakati wa uzinduzi wa mradi maji safi na mazingira mjni humo leo mchana.Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.
RAIS KIKWETE AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE NA ULINZI NA USALAMA, ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA SMART PARTNERSHIP
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na wajumbe wa Kamati Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyomtembelea jijini London, Uingereza, Julai 12, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,Mhe. Edward Lowassa muda mfupi baada ya kukutana nao jijini London,Uingereza, Julai 12, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyomtembelea jijini London, Uingereza, Julai 12, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika kikao maalumu cha maandalizi ya mkutano wa Commonwealth Partnership for Technology Management (CPTM) kwenye makao makuu ya CPTM inayojiandaa kwa mkutano wake mkuu wa Global 2012 International Smart Partneship Dialogue unaotarajiwa kufanyika mwezi Mei Mwakani jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU
wananchi wafurahia kuonana na Rais Jakaya Kikwete viwanja vya sabasaba
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi katika viunga vya uwanja wa maonesho vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Wananchi walijipanga njiani na kusalimiana naye wakati yeye na Mama Salma Kikwete walipokuwa wakitembelea banda moja hadi lingine.
Unamuona…yuleeeee anapita!
Na mimi badooo jamani….
Sisi tunatoka Marekani… tunafurahi kusabahiana nawe
Wow! The man himself…awesome…
Hamjambo,,,?
Mambo,,,,!
Tumefurahi…
RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI TOKA RWANDA NA BURUNDI
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana jioni wakitokea Burundi na Rwanda walikohuidhuria sherehe za miaka 50 wa uhuru wa nchi hizo. Anayeongozana nao ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Mecky Sadik.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Afande Saidi Mwema na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana jioni wakitokea Burundi na Rwanda walikohuidhuria sherehe za miaka 50 wa uhuru wa nchi hizo.PICHA NA IKULU.
HOTUBA YA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 30 JUNI, 2012
Ndugu Wananchi,
Asanteni kwa Kunisikiliza.
Rais Kikwete aongoza kikao cha baraza la Mawaziri mjini Dodoma
Rais Kikwete aongoza watanzania sherehe za Muungano jijini Dar es Salaam leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wananchi wakati alipokuwa akiingia katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kuongoza maadhimisho ya mika 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo asubuhi.
Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya miaka 48 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba wakati alipowasili katika uwanja wa Uhuru kuongoza sherehe za Muungano zilizofanyika leo jijini Dar es salaam.picha na Freddy Maro.
RAIS KIKWETE KUZINDUA RASMI TUME YA KATIBA APRILI 13, 2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atazindua rasmi Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Mabadiliko ya Katiba na kuapisha wajumbe wa Tume hiyo Ijumaa ijayo, Aprili 13, mwaka huu, 2012.
Tume hiyo itazinduliwa na wajumbe wake kuapishwa kulingana na matakwa ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 iliyounda Tume hiyo. Aidha, Tume hiyo itazinduliwa rasmi wiki moja baada ya kuwa imetangazwa rasmi. Rais Kikwete alitangaza Tume hiyo jana, Ijumaa, Aprili 6, 2012, kwenye mkutano wa wahariri uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Tume hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti Jaji Joseph Sinde Warioba akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Augustino Ramadhan ina wajumbe 30, ikiwa ni wajumbe 15 kutoka kila moja ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wajumbe wa Tume hiyo kutoka Tanzania Bara ni Profesa Mwesiga L Baregu, Ndugu Riziki Shahari Mngwali, Dkt. Edmund Adrian Sengodo Mvungi, Ndugu Richard Shadrack Lyimo, Ndugu John J Nkolo, Alhaji Saidi El Maamry na Ndugu Jesca Sydney Mkuchu.
Wajumbe wengine wa Tume hiyo kutoka Bara ni Profesa Palamagamba Kabudi, Ndugu Humphrey Polepole, Ndugu Yahya Msulwa, Ndugu Esther Mkwizu, Ndugu Maria Malingumu Kashonda, Mheshimiwa Al-Shaymaa J Kwegyir, Ndugu Mwantumu Jasmine Malale na Ndugu Joseph Butiku.
Wajumbe wa Tume hiyo kutoka Tanzania Visiwani ni Dkt. Salim Ahmed Salim, Ndugu Fatma Saidi Ali, Ndugu Omar Sheha Mussa, Ndugu Raya Suleiman Hamad, Ndugu Awadh Ali Saidi, Ndugu Ussi Khamis Haji na Ndugu Salma Maoulidi.
Wengine kutoka Visiwani ni Ndugu Nassor Khamis Mohammed, Ndugu Simai Mohammed Said, Ndugu Muhammed Yussuf Mshamba, Ndugu Kibibi Mwinyi Hassan, Ndugu Suleiman Omar Ali, Ndugu Salama Kombo Ahmed, Ndugu Abubakar Mohammed Ali na Ndugu Ally Abdullah Ally Saleh.
Shughuli za Tume hiyo zitaratibiwa na Sekretarieti ambayo Katibu wake atakuwa Ndugu Assaa Ahmad Rashid na Naibu Katibu atakuwa Ndugu Casmir Sumba Kyuki.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
07 Aprili, 2012
President Kikwete opens Anti Corruption meeting in Arusha today
RAIS KIKWETE AFUNGAU MKUTANO MKUU WA MWAKA WA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI LEO MJINI MOSHI
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili Chuo cha Polisi mjini Moshi leo tayari kwa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh. Shamsi Vuai Nahodha na kushoto kwake ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Saidi Mwema.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akizindua mojawapo ya vitabu vya muongozo wa Jeshi la Polisi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Chuo cha Polisi mjini Moshi leo.Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh. Shamsi Vuai Nahodha wa kulia kwa Rais ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Saidi Mwema akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh. Leonidas Gama.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Chuo cha Polisi mjini Moshi leo.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Chuo cha Polisi uliofunguliwa na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Moshi leo.PICHA NA IKULU
HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI,
CHUO CHA POLISI MOSHI, TAREHE 06 MACHI 2012
Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;
Inspekta Generali wa Polisi, Said Ally Mwema;
Mheshimiwa Leonidas Gama, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro;
Makamishna na Manaibu Makamishna wa Jeshi la Polisi;
Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Nakushukuru sana wewe Mheshimiwa Waziri pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kwa kunialika kuja kufungua Mkutano wenu. Nakupongeza kwa dhati Mkuu wa Jeshi la Polisi na viongozi wenzako kwa kuwa na utaratibu wa kukutana kila mwaka kufanya tathmini ya shughuli zenu. Huu ni utaratibu mzuri kwa vile kila Kamanda kwa ngazi yake anatoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa sera, mikakati na mipango mbalimbali ihusuyo usalama wa raia na mali zao katika eneo lake la uongozi.
Nathubutu kusema kuwa msingeweza kuwa na utaratibu mwingine mzuri kushinda huu. Matumaini yangu ni kuwa taarifa hizo zinafanya uchambuzi wa kina wa mafanikio yaliyopatikana, kasoro zilizojitokeza na changamoto mlizokabiliana nazo na mnazoendelea kukabiliana nazo. Aidha, ni matumaini yangu kuwa mjadala unakuwa wa uwazi na ukweli na kwamba hamtaoneana muhali kuambiana ukweli kuhusu kasoro za mwenzenu pale inapostahili. Ni jambo jema na la kijasiri kujiwekea utaratibu wa kujipima wenyewe.
Mheshimiwa Waziri,
Ndugu Mkuu wa Jeshi la Polisi;
Nimefurahishwa sana na Kauli Mbiu ya mkutano wenu “Usingoje, tumia rasilimali ulizonazo kuongeza ufanisi”. Ni Kauli Mbiu muafaka inayohimiza uwajibikaji na ufanisi wa kazi kwa kuzingatia rasilimali zilizopo. Inatambua hali halisi kwamba utegemee ulichonacho kutimiza majukumu yako. Usisubiri usichokuwa nacho. Usisubiri ulichoomba au ulichoahidiwa kupata. Nawaomba mkitoka hapa mwende kwenye vituo vyenu vya kazi mkiwa mmebeba ujumbe huu mzito wa Kauli Mbiu. Mwende mkatekeleze maudhui yake kwa vitendo, kwa kushirikiana na maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali. Mkifanya hivi, bila shaka mtaweza kukidhi matarajio ya wananchi na hivyo kulinda heshima ya Jeshi letu la Polisi.
Ni ukweli ulio wazi kuwa sote tungetamani muwe na zana na vitendea kazi vilivyo bora, vingi vya kutosheleza mahitaji yetu. Lakini uwezo wa kifedha uliopo ni mdogo, vitu hivyo unavyovitaka hutavipata vyote kwa wakati mmoj. Hivyo basi hamna budi kuwa na subira, kupanga vipaumbele vyenu vizuri na hasa kuwa wabunifu ili kwa kutumia vifaa vilivyopo vizuri muweze kutekeleza majukumu yenu kwa kiwango cha kuridhisha.
Mheshimiwa Waziri;
Ndugu IGP,
Maafisa na Askari,
Nataka kuwahakikishia kuwa mimi na viongozi wenzangu Serikalini tunatambua umuhimu wa kuendelea kuliongezea Jeshi la Polisi uwezo wa kibajeti ili liweze kutimiza kwa ufanisi zaidi majukumu yake. IGP ni shahidi kwa kiasi gani tumeendelea kuongeza bajeti ya Jeshi la Polisi mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, mwaka 2005 Bajeti ilikuwa Shilingi 69 bilioni na mwaka huu wa fedha zimetengwa Shilingi 134 bilioni. Nawaahidi kuwa tutaendelea kuongeza fedha kila mwaka katika miaka ijayo. Pia tumetumia uhusiano wetu na nchi rafiki kuomba misaada inayoendelea kuimarisha Jeshi letu kwa zana, mafunzo na weledi.
Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza Maofisa, Wakaguzi na askari wote kwa kazi kubwa na nzuri muifanyayo katika kulinda maisha na mali za raia. Nawapongeza kwa uchapakazi wenu na moyo wenu wa kujitolea na kujituma. Hakika maudhui ya Kauli Mbiu yenu ya mwaka huu mmekuwa mnayatekeleza kwa vitendo. Matokeo ya jitihada zenu yanaonekana. Mafanikio ya kutia moyo yanazidi kupatikana na sote tunayashuhudia. Mwenye macho haambiwi tazama. Uhalifu (hususan wa kutumia nguvu) unaendelea kupungua nchini kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma. Kulingana na takwimu za mwaka wa jana makosa makubwa ya jinai yalipungua kutoka 94,390 mwaka 2010 hadi 76,052 mwaka 2011.
Haya ni mafanikio ya kutia moyo, lakini hamna budi mtambue kuwa bado idadi ya makosa 76,052 ni kubwa mno. Hivyo bado mnayo na tunayo kazi kubwa ya kufanya mbele yenu na yetu. Inatupasa tuongeze juhudi maradufu au hata zaidi ili tupunguze kabisa uhalifu nchini.
Ndugu Makamanda,
Maofisa Waandamizi wa Polisi;
Mheshimiwa Waziri na Inspekta Generali wamezieleza vizuri changamoto zinazolikabili Jeshi la Polisi na mimi sina haja ya kuzirudia. Napenda kutumia nafasi hii kurudia kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kusaidiana nanyi kwa kuwawezesha ili muweze kuzikabili changamoto hizo kwa mafanikio. Tumefanya hivyo miaka iliyopita, tunafanya hivyo hivi sasa na tutafanya hivyo miaka ijayo.
Tutaendelea kuliwezesha Jeshi la Polisi kifedha ili muweze kutekeleza ipasavyo majukumu yenu. Tutaendelea kuwawezesha muongeze idadi ya askari. Tutawawezesha mpate vyombo vya usafiri, zana na vitendea kazi vya kisasa vya kufanyia kazi za kukabiliana na uhalifu. Kazi ya kulipatia Jeshi la Polisi zana na vifaa vipya vya kazi inaendelea ikiwa ni sehemu ya Programu ya Maboresho ya Jeshi la Polisi. Nawahakikishia kuwa tutaendelea kutoa fedha za kutekeleza Programu hiyo na shughuli nyingine za Jeshi la Polisi.
Tutaendelea kuwawezesha katika kuboresha mafunzo ya askari na maafisa wa Jeshi la Polisi. Natambua mahitaji ya kuviboresha vyuo vilivyopo sasa. Panapohitaji kukarabati pakarabatiwe na panapotakiwa ujenzi wa majengo mapya yajengwe. Na panapotakiwa kuanzishwa chuo kipya kianzishwe. Hatuna budi kuwekeza katika mafunzo kwani mafunzo ni msingi mzuri wa weledi na kuwa na askari wenye tabia na mwenendo mwema. Kupata zana za kisasa za upelelezi na kudhibiti uhalifu pekee hazitoshi kama zitakuwa mikononi mwa askari asiyejua kitu, asiyekuwa na nidhamu na utiifu. Kufanya hivyo kunalihakikishia Jeshi uwezo wa kutimiza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na kuleta sifa kwa Jeshi la Polisi Tanzania.
Dunia imebadilika, Tanzania imebadilika na mbinu za uhalifu na aina za uhalifu yamebadilika. Pia, mbinu, mikakati na maarifa ya kukabiliana na uhalifu, nayo yamebadilika duniani. Lazima tusisitize mafunzo, kwani ndiyo msingi wa weledi na ufanisi. Mafunzo ndiyo njia ya kuwawezesha askari na maofisa wa Jeshi la Polisi kupata elimu na maarifa mapya kuhusu uhalifu na namna ya kukabiliana nao. Mafunzo ndiyo yatakayowezesha kuelewa zana na vifaa vipya vya kupambana na uhalifu na kujua namna ya kuvitumia. Hakuna badala ya mafunzo.
Mheshimiwa Waziri,
Ndugu Inspekta Jenerali,
Maofisa,
Wakaguzi na Askari;
Mimi na wenzangu katika Serikali tunatambua umuhimu wa kuboresha maslahi ya maofisa na askari wa Jeshi la Polisi pamoja na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kuishi. Mara baada ya kuchaguliwa mwaka 2005, nilipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na baadhi ya kambi nilijifunza mengi kuhusu hali ya maslahi na mazingira ya kazi na malazi ya wanajeshi wetu. Baada ya hapo tulianza kuyachukulia hatua mambo hayo na tumekuwa tunaendelea kufanya hivyo hadi sasa. Tumeboresha maslahi kwa kiasi chake na bado tunaendelea. Tumeanza ujenzi wa nyumba bora za kuishi na bado tunaendelea na mpango huo.
Napenda kurudia kuwahakikishia kuwa kwangu na wenzangu Serikalini, hakuna upungufu wa dhamira ya kuboresha na kuimarisha Jeshi la Polisi nchini kwa maana ya idadi, mafunzo, vitendea kazi, maslahi na mazingira ya kuishi. Kinachotutatiza ni uwezo wa kifedha wa Serikali ambao si mkubwa sana kuweza kumudu sawia mahitaji yote ya kugharamia shughuli zote za Serikali na Taifa. Pamoja na changamoto hizo, bado tumeendela kuthubutu kuchukua hatua na kwa haya tuliyoweza kufanya kwa upande wa Jeshi la Polisi si haba. Tunaendelea.
Mheshimiwa Waziri,
Ndugu IGP;
Sina budi kuelezea furaha yangu na pongezi za dhati kwako IGP, Makamishna walioko Makao Makuu ya Polisi pamoja na Makamanda wa ngazi mbalimbali kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na rasilimali iliyopo. Huu ni uthibitisho wa uongozi wako makini ukishirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Jeshi letu. Hakika Kauli Mbiu ya mwaka huu kwenu si jambo geni hivyo tunategemea kuona mafanikio makubwa zaidi miaka ijayo. Aidha, mnanipa moyo kuwa hapo rasilimali zitakapoongezeka Jeshi la Polisi litastawi sana.
Usalama Barabarani
Mheshimiwa Waziri,
Inspekta Generali wa Polisi,
Ndugu Makamanda;
Napenda kutumia nafasi hii kurudia maombi yangu kwenu kuimarisha usimamizi wa usalama barabarani. Ajali za barabarani zimezidi mno, hatuna budi kuzizuia zisizidi kuongezeka. Tufanye kila tuwezalo zipungue. Nawaomba mtumie fursa ya mkutano wenu huu kujadili tatizo hili kwa marefu na mapana yake na mkubaliane juu ya nini cha kufanya. Naamini mtaweza.
Nawaomba jambo hili mlipe uzito unaostahili kabla halijageuka kuwa janga la kitaifa. Ukweli kwamba katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka juzi (2010) jumla ya watu 3,687 walipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani. Mwaka na jana (2011) katika kipindi hicho hicho idadi hiyo iliongezeka na kufikia watu 4,013. Hili si ongezeko dogo inatulazimu kushtuka na kuchukua hatua. Nafahamu dhana ya kuwianisha kuongezeka kwa ajali na kuongezeka kwa pikipiki na magari na hali ya barabara zetu. Hata hivyo hivi visiwe visingizio vya kuona kuongezeka kwa ajali za barabarani ni jambo la kawaida. Tuseme ukweli kuwa ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wa madereva kutokuheshimu Sheria ya Usalama Barabarani na ubovu wa vyombo vya usafiri. Kwa sababu zote hizi mbili Jeshi la Polisi lina wajibu maalum kukabiliana nazo. Tafadhali timizeni ipasavyo wajibu wenu. Mkajipange vizuri, kwa kushirikiana na Idara nyingine husika za Serikali, ili ajali na vifo viweze kupungua.
Madereva wazembe, walevi na wasiotaka kufuata Sheria na Kanuni za usalama barabarani wachukuliwe hatua kali. Wakati umefika madereva wakaidi wanyang’anywe leseni zao ili wasihatarishe tena maisha ya Watanzania. Najua haiwezekani kukomesha kabisa ajali za barabarani, lakini naamini kuzipunguza inawezekana. Endapo kuna msaada mnahitaji au jambo mnataka kutoka kwetu, tuambieni. Kama mnadhani Sheria ya Usalama Barabarani na Kanuni zake zinahitaji marekebisho, tuleteeni mapendekezo yenu tuyafanyie kazi. Au kama mnaona kuna mapungufu katika mfumo wa kitaasisi uliopo, msisite kutushauri na sisi tutaangalia namna ya kurekebisha.
Mheshimiwa Waziri,
Ndugu IGP,
Makamanda, Maafisa na Askari,
Jambo lingine ninalopenda mlizungumze kwa kina na mkubaliane katika Jeshi letu ni juu ya hatua za kuchukua dhidi ya tuhuma za kuenea kwa vitendo vya rushwa katika Jeshi la Polisi. Najua mnajitahidi lakini bado ni hisia ya muda mrefu ya wananchi na haionekani kubadilika. Utafiti unaofanywa na taasisi zinazojihusisha na masuala ya utawala bora kuhusu rushwa bado zinalinyooshea kidole chombo chetu hiki muhimu sana cha dola. Natamani sana hisia na taarifa hizo ingekuwa hazina chembe ya ukweli lakini, bahati mbaya huo ndio mtazamo wa jamii na inaelezea wakati mwingine kwa nini baadhi ya wananchi huchukua sheria mikononi mwao.
Pamoja na kuwepo kwa hisia hizo mimi naamini wapo Polisi wengi wazuri na kwamba hali haijafikia kusema imeshindikana kupambana na kukomesha vitendo vya rushwa katika Jeshi la Polisi. Penye nia pana njia. Tafadhali sana tieni nia ya dhati kupambana na tatizo hili na kushinda. Watambueni wale wenzenu miongoni mwenu wenye tabia ya kuomba kitu kidogo muwawajibishe ipasavyo kwa adhabu zinazostahili. Hawa ni watu wanaosaidia wahalifu wasibanwe na mkono wa sheria hivyo ni kikwazo kwa Jeshi la Polisi kutimiza ipasavyo wajibu wake wa msingi wa kupambana na uhalifu. Waondoeni katika Jeshi kwani wanaharibu sifa yenu nzuri na kudhoofisha Chombo chetu.
Mheshimiwa Waziri,
Ndugu IGP,
Ndugu Makamishna,
Maofisa Waandamizi wa Polisi;
Mabibi na Mabwana;
Yamekuwapo malalamiko mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayoelekezwa kwa Jeshi letu la Polisi katika utendaji kazi. Taarifa za kila mwaka zinazotolewa na Tume ya Haki za Binadamu na taasisi nyingine mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa zimekuwa zikionesha hivyo. Yapo pia madai ya watu kunyanyaswa na Polisi kwa kukamatwa bila makosa, kubambikiwa makosa, kuteswa wakiwa mahabusu na hata kuuliwa. Kuna madai ya Polisi kutumia nguvu kupita kiasi na hata kusababisha vifo ya raia.
Nawaomba mtumie fursa ya mkutano huu myazungumze madai hayo na kuamua hatua zipasazo za kuchukua. Natambua kuwa katika Programu ya Maboresho ya Jeshi kuwaelimisha wanajeshi wetu kuhusu masuala ya haki za binadamu ni moja ya mambo yaliyopewa kipaumbele. Nawaomba mtekeleze dhamira yenu hii njema kwa kasi zaidi ili katika kipindi kifupi muwafikie Polisi wetu wote. Aidha, mafunzo kuhusu haki za binadamu yawemo katika mitaala ya vyuo vyetu hapa CCP, Police College – Kurasini na Chuo cha Maafisa Wakuu Kidatu.
Aidha, Jeshi liweke utaratibu mzuri na unaoeleweka wa kupokea na kufanyia kazi malalamiko au maoni yanayopelekwa kwao na wananchi.
Ni muhimu kwa Jeshi la Polisi kusisitiza na kusimamia kwa dhati nidhamu ya maofisa na askari wake. Nidhamu ni sifa ya msingi ya askari. Askari asiye na nidhamu amepoteza sifa ya kuendelea kuwa mwanajeshi. Ni hatari sana kwa usalama wa raia na anaharibu sifa ya Jeshi. Vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyofanywa na baadhi ya maofisa na askari kamwe visivumiliwe. Hivi majuzi nimesikia kuwa hapa Moshi askari ametoroka lindo na kwenda disco, tena akiwa na silaha! Vitendo vya namna hii vinaleta fedheha kwa Jeshi la Polisi na kuwaacha watu wakishangaa na kuwa na maswali mengi juu ya Jeshi lao. Inawezekanaje ifikie hapo kwa askari aliyefunzwa vizuri.
Nawaomba mzingatie upya taratibu zenu za ajira. Wakati umefika wa kuwepo na utaratibu mzuri wa upekuzi wa vijana kabla ya kuteuliwa kusomea kazi ya Polisi. Pawepo na utaratibu thabiti na kufuatilia mienendo ya askari wakati wote wa utumishi wao. Majeshi mengine yanafanya hivyo. Kufanya hivyo kutasaidia kupata vijana walio safi kwa tabia na mwenendo kuajiriwa na kuendelea na utumishi katika Jeshi la Polisi. Kwa ajili hiyo tutakuwa na askari walio watiifu, waaminifu, wachapa kazi hodari na kuliletea sifa Jeshi letu.
Mwisho
Mheshimiwa Waziri,
Inspekta Generali,
Makamanda wa Polisi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu napenda kurudia kutoa pongezi za dhati kwa kazi kubwa na nzuri muifanyayo pamoja na changamoto mbalimbali mnazokabiliana nazo. Nawapongeza sana kwa kubuni utaratibu wa Polisi Jamii ambao ni mfano mzuri wa ubunifu wa kutumia rasilimali zilizopo. Tafadhali uimarisheni na kuuboresha utaratibu huu mzuri. Sisi katika Serikali tutafanya kila linalowezekana kuongeza rasilimali kwa Jeshi la Polisi ili kuliwezesha kukabiliana na uhalifu nchini. Nawaomba mkumbuke na kuzingatia ukweli kwamba katika kila hatua mnayopiga, sisi Serikalini na taifa zima kwa ujumla tutakuwa pamoja nanyi kuwapa moyo na kuwaunga mkono kwa rasilimali muhimu.
Ndugu Inspekta Jenerali,
Makamanda wa Mikoa na Vikosi,
Mabibi na Mabwana,
Baada ya kusema hayo, ninayo furaha sasa kutamka kwamba, Mkutano Mkuu wa Mwaka 2012 wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi umefunguliwa rasmi. Nawatakia mkutano mwema, mazungumzo yenye ufanisi na matokeo mazuri.
“Ahsanteni kwa kunisikiliza”

















































.bmp)









































.jpg)
.jpg)



















.jpg)



.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)











































































































































































































