Author Archives: admin
Rais Kikwete akutana na Mwenyekiti wa Direct AID Charity Organisation ya Kuwait
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu jijini Dar es Salaam Dkt.Abdul RahmanAl Muhailan ambaye ni mwenyekiti wa asasi ya Direct AID Charity Organisation leo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Dkt.Abdul RahmanAl Muhailan ambaye ni mwenyekiti wa asasi ya Direct AID Charity Organisation leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Dkt.Abdul RahmanAl Muhailan ambaye ni mwenyekiti wa asasi ya Direct AID Charity Organisation mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam leo.picha na Freddy Maro,Ikulu.
Rais Kikwete afungua mkutano wa Maendeleo ya Kilimo Barani Afrika
RAIS KIKWETE AZINDUA KITUO CHA TAASISI YA KIMATAIFA YA KILIMO CHA KITROPIKI (IITA) DAR ES SALAAM
![]() |
| Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin William Mkapa wakionja mikate iliyotengenezwa kwa unga wa muhogo wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013. |
wakisikiliza maelezo ya kitaalamu juu ya utafiti wa maradhi ya migomba toka kwa Profesa Rony Swennen wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
![]() |
| Wadau wakiwa katika sherehe hizo |
RAIS KIKWETE AREJEA TOKA AFRIKA KUSINI LEO
Rais Kikwete ahudhuria kikao cha SADC jijini CAPE TOWN
Rais Kikwete awasili nchini Afrika Kusini kuhudhilia kikao cha viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
Rais Kikwete awatkaa wanajeshi wanaokwenda DRC,kuilinda heshima ya Tanzania
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wanashuhudia.
PICHA NA IKULU.
RAIS KIKWETE AKIWA ARUSHA KUHANI MISIBA YA WALIOKUFA KATIKA MLIPUKO WA BOMU KANISA LA OLASITI
Mama Kikwete akiomba kituo cha watoto wenye utindio wa ubongo kushirikiana na Tanzania kutoa mafunzo kwa watoto hao
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekiomba kituo cha watoto wenye mtindio wa Ubongo kilichopo nchini Kuwait kushirikina na Tanzania ili waweze kufanya kazi kwa pamoja ya kuwasaidia na kutoa mafunzo kwa watoto wenye matatizo kama hayo waliopo nchini.
RAIS KIKWETE AKATIZA ZIARA YA NCHINI KUWAIT
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la kigaidi la mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60 wamejeruhiwa.
Rais Kikwete aliyekuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, kukatiza ziara hiyo na anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.
Miongoni mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika eneo la Ahmadi mjini Kuwait. Aidha, Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni ambacho alikuwa anaandaliwa na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.
Rais Kikwete jana alitoa taarifa rasmi ya kulaani kitendo hicho cha kigaidi. Taarifa kamili ni kama ifuatayo:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha. Tukio hilo la kigaidi limesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa. Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu wake.
Rais Kikwete ameagiza vyombo vya usalama nchini kumsaka mtu au watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali na vyombo vyake inaendelea kufuatilia tukio hili. Tutawasaka popote walipo na kupambana nao bila huruma. Aidha, tutakabiliana na aina yoyote ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au aina yoyote ya uhalifu wa namna hiyo au wa namna nyingine, uwe na chimbuko lake ndani ya nchi ama nje ya nchi yetu. Kamwe hatutakubali kuwaacha wavuruge amani na usalama wa Tanzania na watu wake. Rais anaamini kuwa Serikali, kwa msaada na ushirikiano wa wananchi, watu hao watapatikana na kuadabishwa ipasavyo.
Aidha, Rais Kikwete anatoa rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wafiwa na wale wote ambao wamejeruhiwa katika tukio hilo. Anaungana nao katika machungu na msiba. Rais pia anawaombea wote walioumia katika tukio hili wapate nafuu ya haraka na waendelee na shughuli zao za ujenzi wa taifa.
Rais Kikwete vilevile anatoa pole nyingi kwa viongozi na waumini wa Kanisa Katoliki kwa tukio hili la kusikitisha na kuvurugika kwa ibada na shughuli yao muhimu ya uzinduzi wa Kanisa lao.
TAMKO LA RAIS KIKWETE JUU YA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU JIJINI ARUSHA
RAIS KIKWETE AANZA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI NCHINI KUWAIT LEO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah wakipokea mashada ya mauwa alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah wakiingia sehemu ya mapokezi na kukagua gwaride rasmi mara tu alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah katika mazungumzo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.PICHA NA IKULU
Rais Kikwete aongoza mazishi ya Marehemu Balozi Alfred Tandau

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Waziri wa Zamani wa Kazi ,Marehemu Balozi Alfred Tandau wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Marehemu Alfred Tandau ambaye alishika nyadhifa mbalimbali serikalini alifariki tarehe 30 Mwezi Aprili wiki iliyopita.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la Mau katika kaburi la Marehemu Balozi Afred Tandau wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo jioni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa(picha na Ikulu)
RAIS KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS RAJOELINA WA MADAGASCAR
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mhe Andry Rajoelina wakati wa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam Mei 3, 2013.

Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mheshimiwa Andry Rajoelina amewasili mjini Dar Es Salaam jioni ya leo , Ijumaa Mei 3, 2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Amepokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar Es Salaam na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi hao wanatarajiwa kufanya mazungumzo baadaye leo Ikulu, Dar Es salaam.
Rais Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi yaa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Anakutana na Rais Rajoelina kwa mara ya tatu sasa, mara ya kwanza ikiwa ni mwezi Desemba mwaka jana, na baadaye mwezi Januari mwaka huu.
Rais Kikwete alipokutana mara ya mwisho na Rais huyo wa serikali ya mpito ya Madagascar alifanikiwa kumshawishi akubaliane na mapendekezo ya nchi za SADC kuwa asigombee kwenye uchaguzi mkuu utaofanyika mwaka huu kama njia ya kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.
Rais Kikwete awali ya hapo aliweza pia kumshawishi Rais wa zamani wa Madagascar Mhe Marc Ravalomanana asigombee katika uchaguzi mkuu huo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
03 Mei, 2013
RAIS KIKWETE AKUTANA NA WASHIKADAU WA SMART PARTNESHIP IKULU JIJINI DAR
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwenye hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mkutano wa Smart Partnership Mei 3, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washikadau toka katika mashirika binafsi na ya umma walioalikwa katika hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mkutano wa Smart Partnership Mei 3, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU.
RAIS KIKWETE AMPOKEA RAIS WA SERIKALI YA MPITO YA MADAGASCAR ALIETUA DAR JIONI HII
Rais Kikwete apongeza wanabahari kwa kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari Duniani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewapongeza wanahabari ,wadau wa habari na Tasnia nzima ya habari nchini kwa kuadhimisha Miaka 20 ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani (World Press Freedom Day) leo, Ijumaa, Mei 3, akiwahakikishia kuwa Serikali yake itaendelea kukuza, kulea, kulinda na kutetea Uhuru wa Habari ulioshamiri kwa kiwango cha juu kabisa nchini kwa sasa.
Aidha, Rais Kikwete amesisitiza kuwa Serikali yake na yeye binafsi, kama mdau wa habari, wataendeleza kuelekeza nguvu kubwa katika kupanua Uhuru wa Habari kwa sababu uhuru huo ni kigezo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Tanzania na katika kujenga na kupanua demokrasia nchini.
Katika salamu zake kwa wanahabari, wadau wa habari na Tasnia nzima ya habari nchini ambayo inasherehekea Miaka 20 ya Siku ya Uhuru wa Habari Dunia kitaifa mjini Arusha leo katika shughuli zilizoandaliwa na Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika (MISA), Tawi la Tanzania, Rais Kikwete amesema:
“Kama muumini na mdau wa Uhuru wa Habari ambao ni sehemu ya Uhuru Mpana Zaidi wa Kutoa Maoni (Freedom of Expression), napenda kuwapongezeni wanahabari wote nchini na wadau wenzenu duniani katika kusherehekea siku hii ya kuadhimisha Miaka 20 ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani ambayo kitaifa hapa kwetu inaadhimishwa na shughuli zilizoandaliwa na MISA-Tan mjini Arusha.”
Ameongeza Mheshimiwa Rais: “Sisi katika Tanzania tunayo kila sababu ya kusheherekea Siku hii ya leo ya Uhuru wa Habari nchini kwa sababu sote ni wadau wa habari ni mashahidi wa mafanikio makubwa na mengi katika nyanja ya habari katika miaka 20 iliyopita katika nchi yetu. Kwa sababu hiyo, naungana nanyi katika kusheherekea na kuadhimisha mafanikio haya makubwa.”
Siku ya Uhuru wa Habari Duniani ambayo chimbuko lake ni Mkutano wa Waandishi wa Habari wa Afrika waliokutana na kutoa Tamko la Windhoek (Namibia) – the Windhoek Declaration on Promoting an Independent and Pluralistic African Press pamoja na kuanzisha Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika – Media institute of Southern Africa (MISA), Mei 3, mwaka 1991, ilichaguliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa Siku ya Uhuru Duniani mwaka 1993.
Amesisitiza Rais Kikwete: “Napenda kutumia Siku hii ya leo kuwapongezeni tena kwa kazi yenu nzuri ambayo imeendelea kuchangia maendeleo ya nchi yetu kupitia njia ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha wananchi. Vile vile, napenda kutumia nafasi ya Siku ya leo kuwaelezeeni utayari wa Serikali yetu kuendelea kuithamini kazi hii nzuri. Ni matumaini yangu kuwa mtaendelea kuifanya kazi yenu kwa kuongozwa na misingi mikuu ya weledi wa taaluma ya uandishi wa habari.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Aidha, kama ambavyo tumekuwa tukifanya, napenda kuwahakikishieni kuwa mimi binafsi na Serikali ninayoingoza nitaendelea kushirikiana nanyi katika kupanua, kulea, kulinda na kutetea Uhuru wa Habari nchini ikiwa ni haki ya waandishi kufanya kazi yao kwa mazingira mwafaka ya kisiasa, kiuchumi, kisheria na kijamii. Vile vile, napenda kuwahakikisheni tutaendelea kushirikiana nanyi katika kulinda uhuru wa wapata habari nchini ambao ni muhimu kama ulivyo uhuru wa vyombo vya habari.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
03 Mei, 2013
RAIS KIKWETE AMTEUA PROF. PETER MSOLLA KUWA MSHAURI MKUU WA MAKAMU WA RAIS
KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE AKUTANA NA BALOZI WA CANADA NCHINI MHE ALEXANDRE LEVEQUE LEO
jijini Dar es salaam leo asubuhi. Balozi Leveque aliongozana na Mkurugenzi Mwandamizi na Mkuu wa Ushirikiano wa Canadian International Development Agency (CIDA), Bi Patricia McCullagh. Wa pili kushoto ni
Balozi Dorah Msechu, Mkurugenzi katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa anayeshughulikia kurugenzi ya Nchi za Ulaya na Amerika, akifuatiwa na
ofisa dawati Bi Upendo Mwasha.Picha na Ikulu
HOTUBA YA RAIS KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI JIJINI MBEYA
RAIS KIKWETE AFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU MZEE ALFRED TANDAU JIJINI DAR ES SALAAM LEO
NEW PRESIDENT OF CHINA XI JINPING RECEIVES ROUSING WELCOME IN DAR ES SALAAM
China’s new President Xi Jinping arrived in Tanzania today ahead of a three-nation Africa tour also taking in South Africa and the Republic of the Congo.
President Xi flew into Dar es Salaam with his wife from Moscow. After holding official talks scores of ministers and CEO of Chinese companies signed a totalo of 16 accords before the new President of China gave a keynote speech on relations with Africa during a state banquet later on.
He is scheduled to head to Durban, South Africa, tomorrow for a summit of leaders of the world’s major emerging economies, known as the BRICS, on Tuesday and Wednesday, and could endorse plans to create a joint foreign exchange reserves pool and an infrastructure.
RAIS KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA HOSPITALI YA KAIRUKI, DAR ES SALAAM, LEO
wakiangalia watoto wachanga waliotunzwa katika chumba maalum muda mfupi baada ya kuzaliwa wakati Rais Kikwete alipotembelea sehemu mbalimbali
za hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki akiwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 25 ya kuanzishwa kwake leo Machi 16, 2013.
katika hospitali hiyo miaka 25 iliyopita leo Machi 16, 2013.PICHA NA IKULU.
RAIS KIKWETE ASHIRIKI HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA KIGURUNYEMBE, MOROGORO

Rais Kikwete azindua jengo la kitivo cha sayansi chuo kikuu cha kiislamu cha morogoro
![]() |
| Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro Mama Mwantumu Malale akiongea machache na kumkaribisha Rais Kikwete |
HOTUBA YA MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA UFUNGUZI RASMI WA JENGO LA KITIVO CHA SAYANSI KATIKA CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO (MUM),
TAREHE 14 MACHI, 2013, MOROGORO
Mzee Kitwana Suleiman Kondo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF);
Mheshimiwa Joel Bendera, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro;
Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro;
Profesa Hamza Mustafa Njozi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro;
Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na Jumuiya mliohudhuria;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Niruhusuni niungane na wenzangu walionitangulia kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa. Nakushukuru sana Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro na viongozi wenzako kwa kunialika kuja kujumuika nanyi katika siku hii adhimu ya ufunguzi wa jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro. Mmenipa heshima kubwa ya kuwa sehemu ya historia ya Chuo hiki. Kwa kweli, nimefarijika sana kuona Chuo chetu kinazidi kupata mafanikio ya kutia moyo hasa ukizingatia ukweli kwamba kina muda mfupi tu tangu kuanzishwa kwake.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Natoa pongezi nyingi kwako, Makamu Mkuu wa Chuo na wale wote walioshiriki kubuni wazo la kuwa na jengo la Kitivo cha Sayansi na kufanikisha ujenzi wake. Juhudi zao na moyo wao wa kupenda maendeleo ndio umetufanya sisi kujumuika hapa leo kushuhudia mafanikio haya. Hakika ni jambo la kujivunia. Pia, nawapongeza sana Wajenzi na Mhandisi Mshauri kwa kazi nzuri waliyofanya ya ujenzi wa jengo hili. Sote tunaliona jengo lilivyojengwa vizuri na kwa namna yake linapendezesha mandhari ya Chuo.
Kwa namna ya pekee napenda kwa niaba yenu nitoe shukrani zangu za moyoni kwa taasisi ya Al-Barakah kwa kufadhili ujenzi wa jengo hili. Asanteni sana kwa ukarimu wenu na upendo mkubwa mliouonesha kwa nchi yetu na watu wake. Naomba taasisi nyingine na watu binafsi waige mfano huu mzuri wa kusaidia miradi mbalimbali inayonufaisha jamii. Tukumbuke ule msemo wa wahenga kuwa “kutoa ni moyo, usambe si utajiri”.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Mabibi na Mabwana;
Kwa miaka mingi madhehebu ya dini na mashirika ya dini yamekuwa washirika muhimu sana wa Serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Yamekuwa yanajihusisha na kutoa huduma kwa jamii kama vile afya, elimu na nyinginezo. Kwa ajili hiyo watu wengi sana nchini wamenufaika na wanaendelea kunufaika na huduma zinazotolewa na mashirika ya dini.
Kwa miaka mingi mashirika na taasisi za madhehebu ya dini ya Kikristo ndiyo yaliyokuwa yakionekana kutoa huduma hizo. Kwa upande wa Waislamu, ukiacha Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan, mchango umekuwa mdogo sana. Ni jambo la faraja kubwa kuona Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF) ikionyesha njia. Kwa kumiliki na kuendesha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kwa ufanisi, MDF inatoa mchango muhimu katika kuendeleza elimu ya juu na maendeleo nchini. Idadi kubwa ya wanafunzi waliofuzu masomo yao na waliopo katika Chuo hiki tangu kilipoanzishwa mwaka 2005 ni ushahidi tosha wa kazi nzuri inayofanywa na MDF. Hongereni sana. Tunawaombea kwa Mola mpate mafanikio makubwa zaidi miaka ya usoni kwa upande wa elimu na huduma nyingine muhimu.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Katika kipindi cha miaka saba sasa, Serikali yetu imeongeza sana uwekezaji katika upanuzi wa elimu tangu ya awali hadi elimu ya juu. Tumeamua kufanya hivyo kwa sababu vijana wengi waliokuwa wanastahili kupata elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu walikuwa hawapati. Tanzania ni kubwa kuliko Kenya na Uganda kwa eneo na idadi ya watu lakini ndiyo tuliokuwa na idadi ndogo ya wanafunzi kwa ngazi zote hizo. Kwa mfano, mwaka 2005 idadi ya wanafunzi waliokuwa Chuo Kikuu nchini Kenya ilikuwa108,407, Uganda 88,360 na kwa baadhi ya nchi za SADC kama vile Afrika Kusini idadi hiyo ilikuwa 717,973. Wakati wenzetu wakiwa na idadi hiyo, sisi tulikuwa na wanafunzi 40,719 tu katika vyuo vikuu nchini. Hali ilikuwa hivyo pia kwa elimu ya sekondari. Kenya ilikuwa na wanafunzi 925,341, Uganda 619,519 na Afrika Kusini 4,186,882 wakati Tanzania ilikuwa na wanafunzi 524,325 tu waliokuwa katika shule za sekondari.
Tuliona hali hii haikubaliki hivyo tukaamua hatuwezi kuiacha iendelee. Tukaamua kudhibiti. Tukachukua hatua tulizochukua za kupanua elimu katika ngazi zote. Matokeo ya uamuzi huo ni kwamba vijana wanaopata fursa ya kupata elimu katika ngazi zote wamekuwa wengi kuliko wakati mwingine wo wote katika historia ya nchi yetu, tumewafikia na kuwapita majirani zetu. Kazi kubwa tunayoendelea nayo sasa ni kuwekeza katika kuimarisha ubora wa elimu waipatayo vijana wetu kwa kuongeza walimu, vifaa vya kufundishia, vitabu na huduma nyinginezo. Inshallah hata kwa dhamira yetu, hii njema Mola atatuwezesha. Mwanzo mgumu lakini hatma itakuwa nzuri.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Kufuatia juhudi hizo, idadi ya wanafunzi waliopo kwenye vyuo vikuu nchini imeongezeka sana, kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 166,484 mwaka 2012. Kwa upande wa sekondari mwaka 2011 tulikuwa na wanafunzi milioni 1.79 na wenzetu wa Kenya walikuwa na wanafunzi milioni 1.77. Haya ni mafanikio makubwa.
Serikali itaendelea kuwekeza kwenye upanuzi wa fursa za elimu na ubora wake. Hata hivyo ushiriki wa wadau wengine kuunga mkono juhudi za serikali ni jambo muhimu sana. Tumeweka mazingira mazuri kwa wadau hao kufanya hivyo na mafanikio yanaonekana wazi. Kama nilivyokwishasema awali, mashirika ya dini yamekuwa wadau wa kutumainiwa na mchango wao uko wazi. Unajieleza wenyewe. Kwa mfano, katika vyuo vikuu 49 vilivyopo nchini, vinavyomilikiwa na umma ni 14 tu. Vyuo vikuu 24 vinamilikiwa na mashirika ya dini na 11 na sekta binafsi.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa na muhimu unaotolewa na vyuo vikuu vinavyomilikiwa na mashirika ya dini na sekta binafsi. Ninyi mmekuwa washirika wazuri na wa uhakika katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya elimu katika nchi yetu. Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono na kushirikiana nanyi ili kuwawezesha vijana na Watanzania wengi zaidi waweze kupata elimu. Uamuzi wa kufanya utaratibu wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu uhusishe wanafunzi wa vyuo visivyokuwa vya umma ni moja ya mambo mengi muhimu yanayofanywa na Serikali kuthibitisha usemi wangu huo.
Tulipoingia madarakani mwaka 2005 tulifanya mambo mawili muhimu kuhusu mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Kwanza uamuzi kwamba, mikopo itolewe kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma na vile visivyokuwa vya serikali. Kabla ya hapo ilihusu vyuo vya umma pekee. Pili kwamba, kila mwaka tuongeze fedha zinazotengwa kwa ajili ya Mfuko huo ili idadi ya wanafunzi wanaonufaika iongezeke. Tulikuta Mfuko ukiwa na shillingi billioni 56.1 unanufaisha wanafunzi 16,345 mwaka 2005. Tukaongeza kila mwaka na katika mwaka huu wa fedha (2012/13) tumetenga shillingi bilioni 345 zinazowanufaisha wanafunzi 98,772.
Tutaendelea kuongeza fedha katika Mfuko huo ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike na hata ifikie siku moja tuweze kuwakopesha wote bila ya kujali sifa ya uwezo wa wazazi au walezi kulipa ada. Kwa kasi tuliyonayo na kwa jinsi tunavyozidi kufanikiwa katika kukusanya mapato ya serikali, naamini miaka michache ijayo tunaweza kufikia lengo hilo. Nawasihi Bodi ya Mikopo iwekeze katika kuimarisha uwezo wa kuwafuatilia waliokopeshwa kulipa mikopo waliyopewa. Matamanio yangu ni kuwa fedha zilizotolewa zizunguke ili tupunguze kiasi kinachotolewa na bajeti ya serikali kila mwaka.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Mabibi na Mabwana;
Niruhusuni nitumie nafasi hii kukupongeza wewe Mkuu wa Chuo, Makamu Mkuu wa Chuo, Wahadhiri na Jumuiya nzima ya Chuo Kikuu hiki kwa kazi kubwa na nzuri muifanyayo ya kuendeleza na kuboresha Chuo. Tumeshuhudia ujenzi wa jengo nililolifungua leo. Tumeona mafanikio kwa upande wa ongezeko la idadi ya wanafunzi, walimu, wafanyakazi na fani zinazofundishwa katika kipindi hiki kifupi cha uhai wa Chuo hiki.
Nimefurahishwa na kufarijika sana kusikia kuwa ubora wa elimu inayotolewa hapa chuoni ni jambo linalopewa kipaumbele cha kwanza. Jambo hili ni muhimu sana kulisisitiza kwani tunataka wahitimu wa Chuo hiki wafanane na wahitimu wa Chuo chochote kizuri nchini na hata duniani. Ningependa kuona wahitimu wa Chuo hiki wanagombewa katika soko la ajira. Hili ni jambo linalowezekana. Kinachotakiwa ni uamuzi wa Baraza na Seneti kuwa iwe hivyo na kuchukua hatua zipasazo. Sina shaka kuwa mnaweza kufanya hivyo. Hakika mnaweza, na sote kwa umoja wetu tunaweza.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Nimefurahi sana, pia, kusikia kuwa Chuo kinatoa mafunzo ya ualimu. Bila ya shaka mnaelewa kwa nini nafurahi. Tuna uhaba mkubwa wa walimu nchini hivyo Chuo cho chote kinachotoa mafunzo ya ualimu hunifurahisha. Endeleeni kuimarisha mafunzo hayo ili Chuo chenu kitambulike na kukubalika nchini kwa sifa ya kutoa walimu wazuri. Walimu wa kutoka Chuo hiki wawe wale wanaojua vyema masomo wanayofundisha, mahiri kufundisha na waadilifu. Naomba pia mtoe kipaumbele cha juu kwa mafunzo ya ualimu wa masomo ya sayansi na hisabati. Mkifanya hivyo, mtakuwa mnatoa mchango mkubwa katika jitihada za kupunguza uhaba wa walimu wa masomo hayo nchini. Naamini kitendo cha kuzindua Jengo la Kitivo cha Sayansi, kilichofanyika muda mfupi uliopita kinatoa matumaini ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kuchangia katika jitihada za kupunguza pengo la walimu wa sayansi nchini.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Nimewasikia mkieleza kwa ufasaha changamoto kubwa na ndogo ambazo Chuo inakabiliana nazo. Nawapongeza kwa dhati, wewe na viongozi wenzako kwa ubunifu wenu na hatua mnazochukua kuzikabili changamoto hizo. Nawaahidi msaada na ushirikiano wangu na wa serikali kwa yale yaliyoko kwenye uwezo wangu na wa serikali katika kutafuta ufumbuzi kwa changamoto zinazowakabili.
Nawapongeza kwa uamuzi wenu wa kutafuta vyuo vikuu rafiki vilivyoko katika nchi mbalimbali duniani mnavyoweza kushirikiana navyo. Endeleeni kufanya hivyo kwani vyuo vikuu vingi duniani hufanya hivyo. Hamtakuwa wa kwanza na wala hamtakuwa mnafanya jambo la kustaajabisha. Mnaweza, mkipenda, kuwaomba Mabalozi wetu waliopo katika nchi mbalimbali duniani wawasaidie. Ni wajibu wao kufanya hivyo kwani kusaidia kusukuma maendeleo ya hapa nchini kutoka huko waliko ndilo jukumu lao la msingi. Vile vile, nimefurahishwa na mipango yenu ya baadaye ya kuwa na matawi katika mikoa mbalimbali nchini. Hongereni kwa uamuzi wenu wa busara. Lazima Chuo kitanuke kwa maana ya kuwa kikubwa zaidi, makao makuu na kwa kuwa na vyuo vishiriki na shule au vitivo sehemu mbalimbali nchini.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Kazi iliyo mbele yenu ni kubwa, hivyo ni vyema kuweka mikakati mizuri na mipango thabiti ya utekelezaji na ufuatiliaji wa dhamira yenu hiyo njema. Rai yangu kwenu ni kuwaomba muwe wabunifu zaidi hasa katika kutafuta vyanzo vingine vya mapato vitakavyosaidia Chuo kujiendesha bila kutegemea ada peke yake. Chuo kiangalie uwezekano wa kufanya shughuli zitakazowaingizia mapato kama vile kufanya shughuli za kutoa ushauri. Pia muangalie uwezekano wa kuwekeza wenyewe kwenye miradi ya kiuchumi au kwa kushirikiana na wawekezaji katika baadhi ya maeneo.
Kuhusu nafasi mbili za ufadhili nilizopewa na Chuo kikuu cha Tun Abdul Razak cha Malaysia, nitafuatilia kujua kilichoendelea na kinachoendelea. Je, nafasi hizo bado zipo? Zikiwepo, nitawasiliana na wahusika waangalie uwezekano wa kuwapeni. Kama zimeshagawiwa basi tusubiri safari ijayo. Kwa masuala ya ardhi na maombi mengine nimeyasikia, yaleteni tuangalie namna ya kusaidiana.
Ndugu Makamu Mkuu wa Chuo, na
Wafanyakazi wote wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro;
Napenda kuwakumbusha kuwa mnayo dhamana kubwa na wajibu mkubwa na wa kihistoria. Ule ukweli kwamba ni mara ya kwanza kwa Taasisi ya Waislamu wazawa kuwa na Chuo Kikuu inawapeni wajibu maalum wa kuhakikisha Chuo kinafanikiwa. Ni mtihani na changamoto ya aina yake kuthibitisha kuwa Waislamu nao wanaweza kuwa na Chuo kizuri na chenye kutoa elimu ya ubora wa hali ya juu. Kwa sababu hiyo hamna budi kuhakikisha kuwa mna mipango mizuri ya kujenga Chuo cha hadhi na ubora wa hali ya juu. Ihakikishwe kuwa mipango hiyo inatekelezwa kwa ukamilifu.
Aidha jumuiya yote inao wajibu wa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, maarifa na weledi ili dhima hiyo ya Chuo iweze kutimizwa kwa ukamilifu. Timizeni wajibu wenu ipasavyo ili jina la Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro likue haraka. Sifa yake isambae na kuvuma kote nchini. Chuo kifanye vizuri ili wanafunzi waone fahari kuwa wahitimu wa Chuo hiki. Chuo ambacho, wazazi wapende kuleta vijana wao kuja kusoma hapa. Kwa jinsi Mkuu wa Chuo alivyoeleza, mimi nina imani mnaweza, fanyeni kweli.
Ndugu Wanafunzi wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro;
Naomba wote muone fahari ya kuwa wanafunzi katika Chuo cha kihistoria hapa nchini. Nawasihi mjitume kwa kadri ya uwezo na vipaji mlivyopewa na Mwenyezi Mungu mfanikishe kile kilichowaleta. Jifunzeni kwa bidii mfaulu vizuri ili mkihitimu muwe kielelezo kizuri cha mafanikio na ubora wa Chuo Kikuu Cha Waislamu cha Morogoro. Muwe Mabalozi na kioo cha ufanisi wa Chuo hiki. Nawasihi mjiepushe na mambo yatakayowapunguzia muda au kuwaondoa katika shughuli ya msingi iliyowaleta hapa ya kujifunza mpate digrii katika fani mliyochagua mwenyewe kuisomea. Vishawishi ni vingi na wapo watu wengi wanaopanga kuwashawishi mtumie muda wenu adhimu kufanya wanayoyataka wao ambayo mkishiriki huwatoa kwenye malengo na kutekeleza yao. Mambo ya dunia ya nje ya Chuo ni mengi huna budi kutambua lipi ufanye na lipi usifanye na kwa wakati gani!
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu ni mtu mzima, si mtoto. Lazima ujue kuwa unawajibika kwa kila unaloamua na kutenda. Amua kuwajibika vizuri. Fikiri kabla ya kutenda, changanua lipi ni lipi kabla ya kufanya uamuzi wa kile unachotaka kufanya. Wakati wote uongozwe na busara na hekima na siyo jazba na ushabiki wa matakwa ya kundi. Kama ni jema fanya na kama si jema usifanye. Kwanza tambua wewe ni nani na uko hapa kwa ajili gani. Lazima ujue kuwa hatma ya yote uko peke yako. Utafaulu au kufeli wewe. Utapata shahada wewe na si mtu mwingine. Hakuna ubia wa kufaulu au kufeli au kiwango cha kufaulu. It will always remain personal. Katika masomo unanufaika wewe. Shirikiana na wengi lakini usisahau kujali maslahi yako. Maslahi ya wengi yasiyojumuisha yako, yahoji vizuri kabla ya kuamua kushiriki au kufanya. Vinginevyo labda kama umeamua kujitoa muhanga, uwe shujaa. Hata kwa hilo, sijui utakuwa shujaa wa nani.
Mabibi na Mabwana;
Kabla ya kumaliza napenda kutambua na kumshukuru Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa na viongozi wa MDF kwa juhudi zao za pamoja zilizowezesha Chuo hiki kuwepo. Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru wananchi wanaokizunguka Chuo kwa ujirani mwema na wakazi wa Morogoro kwa ujumla kwa kukipokea vizuri na kuishi na wanajumuiya wa Chuo hiki kwa upendo mkubwa. Naomba muendelee na moyo na ushirikiano huo.
Baada ya kusema hayo, nawashukuru sana kwa kunialika. Nawatakia kila la heri na mafanikio tele.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
RAIS KIKWETE AMTEMBELEA MZEE YUSUF MZIMBA ALIYELAZWA MUHIMBILI KWA KUGONGWA NA BODABODA

Mzee Mzimba amevunjika mguu wa kushoto na kupata majeraha ya usoni na mikononi. Hadi jana hali yake ilikuwa inaendelea vyema na Rais Kikwete amempa pole nyingi kwa maumivu aliyoyapata na kumtakia
apate nafuu ya haraka.PICHA NA IKULU
RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWENYEKITI WA BHARTI AIRTEL YA INDIA BW SUNIL MITTAL IKULU, DAR ES SALAAM
WAZIRI MKUU WA DENMARK APOKEWA KWA SHANGWE IKULU, DAR ES SALAAM
RAIS KIKWETE AMKARIBISHA WAZIRI MKUU WA DENMARK IKULU JIJINI DAR LEO
Mhe Helle Thorning-Shmidt wakiingia Ikulu huku wakishangiliwa.
Thorning-Shmidt katika viunga vya Ikulu kabla ya mgeni huyo kupanda mti
wa kumbukumbu.
waandamizi wa Ikulu katika viunga vya Ikulu kabla ya mgeni huyo kupanda
mti wa kumbukumbu.
Thorning-Shmidt katika viunga vya Ikulu kabla ya mgeni huyo kupanda mti
wa kumbukumbu.
RAIS KIKWETE AMLAKI WAZIRI MKUU WA DENMARK ANAYETEMBELEA TANZANIA LEO
RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI LEO,PIA AAGANA NA BALOZI WA UAE
wa kufanya kazi nchini Mhe. Mallalla Mubarak Al Ameir alipoagana naye Ikulu, Dar es salaam, leo Machi 1. 2013.
wa kufanya kazi nchini Mhe. Mallalla Mubarak Al Ameir alipoagana naye Ikulu, Dar es salaam, leo Machi 1. 2013
wa kufanya kazi nchini Mhe. Mallalla Mubarak Al Ameir alipoagana naye Ikulu, Dar es salaam, leo Machi 1. 2013.PICHA NA IKULU.
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, 28 FEBRUARI, 2013
Utangulizi
Ndugu wananchi;
Namshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kuwasiliana kupitia utaratibu wetu mzuri tuliojiwekea wa kufanya hivyo kila mwisho wa mwezi. Leo nimepanga kuzungumza nanyi mambo matatu; yaani Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Uhusiano wa Waislamu na Wakristo na Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne.
Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano wa
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
Ndugu Wananchi;
Tarehe 8 Februari, 2013 kule Addis Ababa, Ethiopia niliungana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Ban Ki-Moon, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Nkosozana Dlamini Zuma na viongozi wa nchi 12 za Afrika Mashariki, Kati na Kusini kutia saini Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na jirani zake. Pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zilikuwepo nchi za Burundi, Rwanda, Uganda, Sudani Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Angola, Zambia na Tanzania ambazo ni jirani ya Kongo. Nchi za Ethiopia, Msumbiji na Afrika ya Kusini pamoja na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zilitia saini kama wadhamini. Ethiopia kwa nafasi yake ya kuwa Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika na Msumbiji kwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Nchi wanachama wa Mkutano wa Ukanda wa Maziwa Makuu ziliwakilishwa na Uganda ambayo ni Mwenyekiti wake wa sasa. Afrika ya Kusini ilishirikishwa kwa kuwa taifa kubwa na linalotegemewa katika ukanda wetu.
Mpango huu ni jitihada nyingine ya kusaidia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ipate amani ya kudumu. Kama tujuavyo, tangu mwaka 1997 wakati wa vita vilivyosababisha kuondolewa kwa Rais Mobutu Seseseko mpaka sasa nchi hiyo rafiki na jirani haijapata amani na utulivu wa kudumu. Kumekuwepo jitihada na mipango kadhaa ya kuleta amani ambayo hata hivyo baada ya muda fulani machafuko hutokea tena na mipango hiyo kuvurugika. Inakadiriwa kuwa takriban watu milioni 5.4 wamepoteza maisha na watu wengi kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi yao. Pia kumekuwepo na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na mali nyingi kuharibiwa au kuporwa.
Ndugu Wananchi;
Machafuko yaliyoanzishwa na waasi wa Kundi la M23 mapema mwaka wa jana ndiyo sababu ya kuwepo kwa Mpango huu wa sasa tuliotia saini kule Addis Ababa, Ethiopia tarehe 8 Februari, 2013. Katika Mpango huo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na jirani zake, Tanzania ikiwemo, tumekubaliana kutokufanyiana vitendo vinavyohatarisha amani na usalama wa nchi zetu. Tumeazimia tusifanye hivyo ama moja kwa moja kama nchi au kwa kutumia watu wengine. Aidha, tumekubaliana tusiruhusu watu au vikundi vya watu kutumia nchi zetu kuhatarisha usalama wa nchi nyingine. Kimsingi tumekubaliana kuwa majirani wema. Katika Mkataba huo, majukumu ya kila nchi yameainishwa vizuri pamoja na yale ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mashirika ya Kikanda hususan SADC na ICGLR.
Ndugu Wananchi;
Niliamua kukubali kushiriki na kutia saini Mpango ule kwa kutambua ukweli kwamba sisi majirani wa nchi ya Kongo tunao wajibu wa kusaidia kwa kile tunachoweza. Wananchi wa Kongo wameteseka kwa muda mrefu mno hivyo kama Mpango huu utawasaidia kupata amani na usalama hatuna budi kuunga mkono. Ni kwa misingi hiyo hiyo, tulikubali kuchangia kikosi kimoja katika Jeshi la Kimataifa la kulinda amani huko Mashariki ya Kongo kama ilivyoamuliwa na Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu mwezi Julai, 2012. Uamuzi huo umeungwa mkono na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika. Umoja wa Mataifa umeamua Jeshi hilo liwe sehemu ya Jeshi la Umoja wa Mataifa la Kulinda Amani nchini Kongo (MONUSCO) jambo ambalo sote tumeliafiki. Tumepeleka walinzi wa amani Darfur, Sudan na Lebanon, kwa nini tusipeleke Kingo. Miaka ya nyuma tulishapeleka walinzi wa amani Liberia, Siera Leon na Eritrea.
Ni matumaini yetu kuwa Mpango huu mpya utatekelezwa kwa ukamilifu na kuzaa matunda yaliyokusudiwa. Kama nchi jirani, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yenye amani, usalama na utulivu ni jambo lenye maslahi makubwa kwetu. Ina maana ya kutokuwa na wakimbizi kutoka nchi hiyo, uharamia katika Ziwa Tanganyika kutokuwepo na ustawi wa shughuli za kiuchumi na kibiashara kwa upande wetu na wao. Ni chachu muhimu ya maendeleo ya Mikoa ya pembeni mwa Ziwa Tanganyika na Tanzania kwa jumla.
Uhusiano wa Waislamu na Wakristo
Ndugu wananchi;
Jambo la pili ninalopanga kulizungumzia siku ya leo ni uhusiano wa Wakristo na Waislamu hapa nchini. Kwa miezi kadhaa sasa tangu mwaka wa jana kumekuwepo na matukio kadhaa yanayosababisha mifarakano na kupandikiza chuki baina ya waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu. Matukio ya kauli na vitendo vya kudharau dini za wengine, kunajisi vitabu vitakatifu vya dini hizo, kuchoma moto nyumba za ibada na mzozo kuhusu nani achinje. Kumekuwepo na matumizi mabaya ya radio na simu za mkononi na mifumo mingine ya mawasiliano iliyoeneza maneno na ujumbe wa chuki na vitisho kwa waumini na viongozi wa dini zetu hizi kubwa hapa nchini. Kauli na matendo hayo, katika baadhi ya maeneo yamekuwa chanzo cha uhasama na magomvi baina ya waumini na hatimaye kusababisha vifo kama ilivyotokea Buseresere Mkoani Geita na Beit-el-Ras, Zanzibar.
Ndugu zangu;
Watanzania hatujawahi kuwa hivi, kumetokea nini? Miaka yote Watanzania ni watu tunaotambua na kuheshimu tofauti za dini zetu mbalimbali tunazoabudu. Watanzania ni waelewa na kwa ajili hiyo tumekuwa tunavumiliana kwa tofauti zetu na ndiyo maana tumekuwa tunaishi pamoja kidugu, kwa umoja na kushirikiana kwa mambo yote yanayotuhusu maishani isipokuwa wakati kila mmoja anapoingia kwenye nyumba ya ibada kumuomba Mola kwa misingi na taratibu ya dini yake.
Watanzania wa dini zote na makabila tofauti wanaishi nyumba moja, wanasoma pamoja, wanafanya kazi pamoja kwa udugu, upendo, umoja na ushirikiano. Kuna koo na familia zenye watu wa dini tofauti, wengine Waislamu na wengine Wakristo. Wapo Waislamu na Wakristo wameoana, wamezaa na wamejukuu na kila mmoja amebakia kuwa mfuasi wa dini yake. Wapo pia ambao hawakuoa lakini wamezaa watoto na wanashirikiana kulea watoto wao. Hayo ndiyo maisha ya Watanzania na hiyo ndiyo Tanzania yenye amani na utulivu tuliyozaliwa, kukua na kuishi. Nawasihi sana Watanzania wenzangu, tuienzi na kuidumisha tunu hii waliyotujengea mababu zetu.
Ndugu Wananchi;
Kuna wenzetu kwa sababu wanazozijua wao na kwa manufaa wanayoyajua wao wanataka kutuvurugia nchi yetu hii nzuri. Tusiwape nafasi wachochezi hawa kwani hawatutakii mema na wala hawazitakii mema dini zetu na nchi yetu. Sisi katika Serikali hatutasita kuwachukulia hatua wale wote wanaochochea chuki za kidini, wanaodharau vitabu vitakatifu vya dini nyingine na wanaokejeli dini nyingine.
Nimewakumbusha Polisi na mamlaka husika kote nchini wasifanye ajizi kwenye matukio ya namna hiyo. Wawachukulie hatua stahiki wale wote wanaohusika. Nimewataka wazingatie msemo wa Kiswahili usemao “ajizi nyumba ya njaa”. Wachochezi wa mifarakano na chuki za kidini wasipodhibitiwa ipasavyo wataleta maafa kwa Watanzania wasiokuwa na hatia. Nimewakumbusha Wakuu wa Wilaya na Mikoa kama walinzi wa amani wa maeneo yao ya uongozi, watimize ipasavyo wajibu wao. Pia nimewataka Polisi wakamilishe mapema upelelezi wa makosa ya vurugu za kidini na wahusika wafikishwe haraka kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine.
Ndugu Wananchi;
Naendelea kuwasiliana na viongozi wa dini kuzungumza nao juu ya wajibu wao maalum wa kuhakikisha kuwa wafuasi wao hawawi chanzo au sehemu ya tatizo na mifarakano miongoni mwa waumini wa dini mbalimbali nchini. Hali kadhalika naitumia nafasi hiyo kuwakumbusha umuhimu wa kuzungumza na wenzao wa upande mwingine kutatua tofauti au matatizo yanayoathiri uhusiano mwema baina yao.
Ndugu Wananchi;
Kuna msemo maarufu usemao “mjenga nchi ni mwananchi na mbomoa nchi ni mwananchi”. Naomba tuwe wajenga nchi na kamwe tusikubali kuwa wabomoa nchi. Hivi tukiibomoa nchi yetu tutakwenda wapi? Tutaishi wapi? Tusikubali kugeuka wakimbizi ndani ya nchi au nje ya nchi yetu.
Kwa mara nyingine tena, napenda kutumia nafasi hii kuwapa mkono wa pole makanisa, familia, ndugu na jamaa wote wa Mchungaji Kachila na Padri Mushi. Sote tunafahamu machungu waliyonayo kwa kuondokewa na wapendwa wao. Serikali na wapenda amani wote nchini wapo pamoja nanyi katika kipindi hiki kugumu. Vile vile natoa rambirambi zangu nyingi kwa waumini wote wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God na Kanisa Katoliki Tanzania kwa kuondolewa ghafla na viongozi wao. Tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu azipumzishe kwa amani roho za viongozi wetu. Amin.
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2012
Ndugu wananchi;
Tarehe 18 Februari, 2013 Baraza la Mitihani la Taifa lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne ya mwaka 2012. Wanafunzi 397,132 walifanya mtihani huo na kati ya hao, waliofaulu ni 126,851 yaani sawa na asilimia 34.5. Wanafunzi 240,903 ambao ni sawa na asilimia 65.5 hawakufaulu mtihani huo. Kwa ulinganifu, matokeo hayo ni mabaya kuliko matokeo mengine ya mtihani huo ya miaka ya hivi karibuni.
Mwaka 2011, jumla ya wanafunzi 336,782 walifanya mtihani huo na waliofaulu walikuwa asilimia 53.6 na ambao hawakufaulu kabisa walikuwa asilimia 46.4. Mwaka 2010 jumla ya wanafunzi 352,045 walifanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne, asilimia 50.4 ya wanafunzi hao walifaulu na asilimia 49.6 ya wanafunzi hawakufaulu.
Ndugu Wananchi;
Matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012, yameshtua na kufadhaisha watu wengi nchini na kwa sababu stahiki kabisa. Kwanza, kwamba kiwango cha kufaulu kimeporomoka sana, tena ghafla, kutoka asilimia 53.6 mwaka 2011 hadi asilimia 34.5 mwaka 2012. Hili ni anguko la asilimia 19.1 ambalo, kwa kila hali, ni kubwa sana. Pili, kwamba hata shule zinazofahamika kuwa na historia ya kufaulisha vizuri kama vile seminari, shule za watu binafsi, za mashirika ya dini na sekondari kongwe za Serikali ambazo hazina matatizo kama ilivyo kwa zile sekondari za Kata, nazo safari hii hazikupata mafanikio kama ilivyo kawaida yao. Nazo zimejikuta zikiwa na idadi ya vijana waliopata daraja la kwanza, la pili na la tatu ikipungua wakati waliopata daraja la nne na waliofeli wakiongezeka.
Isitoshe na kiwango cha ufaulu wa vijana umepungua pia. Mwaka 2010 wanafunzi 10 bora wote walikuwa wamefaulu daraja la kwanza la alama au pointi 7. Mwaka 2011 katika wanafunzi 10 bora wanane walipata daraja la kwanza kwa alama 7 na wawili alama 8. Mwaka 2012 katika wanafunzi 10 bora, watatu walipata daraja la kwanza kwa alama 9, watatu alama 10 na wawili alama 11.
Ndugu Wananchi;
Haya ndiyo mambo yanayozua maswali kwa watu wengi yanayohitaji kupatiwa majawabu ya uhakika. Kulikoni mwaka 2012? Ndiyo msingi wa uamuzi wa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, kuamua kuunda Tume ya kuliangalia suala zima la mitihani ya mwaka 2012 na matokeo yake. Hali hii haijawahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni. Ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu, hivyo lazima ukweli wake ujulikane kwa uhakika. Hii itawezesha Serikali na wadau wengine kuchukua hatua stahiki kurekebisha mambo mapema iwezekanavyo ili hatimaye mambo yawe mazuri siku za usoni. Tusipofanya hivyo mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi na lawama zinaweza kuwa kubwa zaidi kwa Serikali.
Ndugu Wananchi;
Hivi sasa kunatolewa mawazo lukuki kuhusu sababu za kwa nini matokeo yamekuwa mabaya. Wapo wanaodhani kuwa lipo tatizo katika utungaji wa mitihani, usahihishaji wake au kutoa maksi kwa watahiniwa. Wapo wanaodhani walimu hawawajibiki ipasavyo au baadhi yao kutokumudu masomo wanayofundisha. Wapo wanaofikiria kuwa wanafunzi hawako makini katika kufuatilia masomo na wazazi hawajali kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni. Wapo wanaoinyooshea kidole Serikali kwa sera, mitaala na uwekezaji usiokidhi mahitaji ya maendeleo ya elimu. Wapo wanaofikiria kuwa Serikali kushindwa kuongeza mishahara ya walimu kwa asilimia 100 kama walivyotaka imechangia. Orodha ni ndefu, ali mradi kila mtu ana mawazo yake. Na sisi katika Serikali hatuwezi kuwa tunadhani kwa sababu tunayo dhamana maalum. Lazima tujue ukweli kwa uhakika na ndiyo maana kuna umuhimu wa Tume. Naomba kila mtu mwenye mawazo yake ayafikishe kwenye Tume hiyo hapo itakapoundwa ili tupate jawabu muafaka la tatizo hili.
Ndugu Wananchi;
Napenda kuwahakikishia kuwa sisi katika Serikali tumetoa kipaumbele cha juu sana kwa elimu na kwamba hakuna upungufu wa utashi kwa upande wangu na wenzangu wote Serikalini. Ndiyo maana tumeguswa sana na matokeo haya. Bajeti ya elimu ya shilingi trilioni 3.6 ambayo ni sawa na asilimia 24 ya bajeti yote ya Serikali ndiyo kubwa kuliko zote. Kwa ajili hiyo imetuwezesha kuendelea kukabili mahitaji na changamoto za upanuzi mkubwa wa elimu ya sekondari na elimu ya juu. Bado hatujazimaliza changamoto zote na kwamba bado tuna kazi kubwa mbele yetu, lakini mafanikio yanaendelea kupatikana. Tutaendelea kutoa kipaumbele cha juu kwa elimu mpaka hapo itakapofikia mahali kwamba matatizo makubwa yatakapokuwa yamepungua sana.
Hitimisho
Ndugu Wananchi;
Mungu Ibariki Tanzania!
Mungu Ibariki Afrika!
Nashukuru kwa kunisikiliza!
Rais Kikwete apokea ujumbe Maalum Kutoka Kwa Rais Omar El Bashir wa Sudan
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe maalumu
kutoka kwa Rais Omar El Bashir wa Sudan ulioletwa na Mhe.Dkt.Nafie Ali Nafie
ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JKT JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Rais Kikwete akagua Ukumbi mpya Wa Mikutano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam
Rais Kikwete akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Mhe.Yousuf bin Alawi bin Abdulah ikulu jijini Dar es Salaam
Rais Kikwete Katika mazishi ya baba yake rais musveni wa uganda
Rais Kikwete na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh.Shamsi Vuai Nahodha waliondoka kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo.
yake yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura. Kulia ni Mama Janet Museveni
RAIS KIKWETE ASHIRIKI UTIAJI SAINI MPANGO WA UMOJA WA MATAIFA WA AMANI, USALAMA NA USHIRIKIANO KATIKA DRC
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013.

Rais Kikwete awasili Jijini Addis Ababa leo
RAIS KIKWETE AKIFUNGUA WARSHA MAALUMU KATIKA HOTEL YA WHITE SANDS
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua warsha maalumu itakayojadili mikakati ya kutekeleza ili kufikia Dira ya Maendeleo Tanzania 2025 katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo inaongozwa na Waziri Idris Jala Kutoka Malaysia aliyebobea katika masuala ya Uchumi na Maendeleo.
Baadhi ya Washiriki wanaohudhuria Warsha Maalum itakayojadili mikakati ya kutekeleza ili kufikia Dira ya Maendeleo Tanzania 2025 katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo inaongozwa na Waziri Idris Jala Kutoka Malaysia aliyebobea katika masuala ya Uchumi na Maendeleo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal(Watatu Kushoto),Waziri Mkuu Mizengo Pinda(wane kushoto) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Wapili kulia) na,Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu.Wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya ufunguzi wa Warsha Maalumu itakayojadili mikakati ya kutekeleza ili kufanikiwa kufikia Dire ya Maendeleo Tanzania 2025 inayofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.Warsha hiyo inaongozwa na Waziri Idris Jala Kutoka Malaysia(wapili kushoto)(picha na Freddy Maro)
BALOZI SEFUE AKUTANA NA MKUU WA PEMANDU TOKA MALAYSIA DKT IDRIS JALA
RAIS KIBAKI AHITIMISHA ZIARA YAKE YA KISERIKALI YA SIKU MBILI NCHINI
UZINDUZI RASMI WA BARABARA YA MWAI KIBAKI LEO
![]() |
| Vifijo na nderemo baada ya uzinduzi huo. |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya muda mfupi kabla ya kufanya mazungumzo rasmi(official talks)Ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwatambulisha kwa rais Mwai Kibaki baadhi ya Mawaziri waliohudhuria dhifa ya kitaifa ikulu jinni Dar es Salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonga glasi na mgeni wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa Ikulu kwa heshima ya Rais Kibaki aliyeko nchini kwa ziara yaka ya mwisho ya kiserikali.
Rais Kibaki awasili kwa Ziara ya Kiserikali ya siku Mbili
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Mwai Kibaki wa Kenya muda mfupi
baaada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa
ziara ya kiserikali (State Visit) ya siku mbili.
Mwai kibaki wa Kenya akikaribishwa kwa maua na Mwanafunzi Tazmina Rasul(6) muda mfupi baada ya
kuwasili nchini kwa ziara ya kiserikali (State Visit) ya siku mbili huku
mwenyeji wake Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiangalia. (Picha na Freddy Maro).
President Kikwete meets USAID administrator Dr. Rajiv Shah at Dar es Salaam State House
RAIS KIKWETE AKUTANA NA WANACHAMA WA SIMIYU COMMUNITY BANK LEO IKULU
leo Februari 19, 2013 kumwelezea mipango ya kufungua benki hiyo itayoshirikisha jamii katika mkoa huo mpya na ya jirani katika azma ya kumkomboa mjasiriamali na mkulima
mdogo.
leo Februari 19, 2013
leo Februari 19, 2013.PICHA NA IKULU






























.bmp)























.bmp)






.jpg)






















































.jpg)



.jpg)
.jpg)

















































.jpg)




















