Rais Kikwete ahudhuria mazishi ya shemeji yake mjini Lindi leo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amehudhuria mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani Kinyozi (45), aliyefariki Jumamosi iliyopita jijini Dar es salaam, na kuzikwa katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi.Pichani ni Rais Kikwete akishiriki katika swala ya kumuombea marehemu mjini Lindi leo.

Rais Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya shemeji yake, Marehemu Amani Kinyozi, katika makaburi ya Mitandi mjini Lindi leo Julai 30, 2012.PICHA NA IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, amewasili mjini Lindi leo, Jumatatu, Julai 30, 2012 kwa ziara ya siku mbili ambako miongoni mwa mambo mengine atafuturisha wananchi na viongozi wa mkoa wa Lindi.

Aidha, rais Kikwete amehudhuria mazishi ya shemeji yake , Marehemu Amani Kinyozi, aliyefariki siku ya Jumamosi jijini Dar es salaam.

Rais Kikwete, ambaye ameongozana na mke wake Mama Salma Kikwete, alijumuika na mamia ya wakazi wa mji wa Lindi kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Mitandi, mjini humo.

Marehemu Amani Kinyozi, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 45, ameacha mke na watoto wawili.

Enzi za uhai wake marehemu alikuwa mtaalamu wa kutengeneza mifuko ya karatasi, na pia alikuwa akifundisha kinamama wajasiriamali ufundi huo katika juhudi za kuepukana na matumizi ya mifuko ya plastiki, maarufu kama mifuko ya rambo ya kufungia bidhaa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
30 Julai, 2012

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*

HTML tags are not allowed.