Rais Kikwete amuapisha Mkuu Mpya wa JKT Meja Jenerali Samwel Ndomba ikulu Jijini Dar es Salaam

Amiri Jeshi mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange(kushoto) na Mkuu mpya wa JKT Meja Jenerali Samwel Ndomba muda mfupi baada ya hafla ya kumuapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,(kushoto)Waziri Mkuu Mizengo Pinda(kulia) na Mkuu mpya wa JKT Meja Jenerali Samwel Ndomba wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya hafla ya kumuapisha mkuu huyo mpya wa JKT ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mzee Albert Ndomba(85),baba mzazi wa Mkuu Mpya wa JKT, Meja Jenerali Samwel Ndomba(wapili kushoto) baada ya halfa ya kumuapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni mke wa Meja Jenerali Ndomba na waliosimama nyuma ni wanafamilia.
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miongozo ya kazi mkuu mpya wa JKT meja Jenerali Samwel Ndomba wakati wa hafla ya kumuapisha iliyofanyika leo asubuhi ikulu jijini Dar es Salaam.

Mkuu Mpya wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Samwel Ndomba akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi ya Meja Jenerali Samwel Kitundu aliyestaafu hivi karibuni kwa mujibu wa sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*

HTML tags are not allowed.