MAJINA YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA

UTANGULIZI

1.              Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.

 

2.           Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-

(i)               Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;

(ii)            Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na

(iii)         Wajumbe 201 kwa mujibu wa  Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.

 

3.           Makundi hayo ni  kama ifuatavyo:-

 

(i)                  Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)

(ii)               Taasisi za Kidini (20)

(iii)            Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);

(iv)             Taasisi za Elimu (20);

(v)                Watu wenye Ulemavu (20);

(vi)             Vyama vya Wafanyakazi (19);

(vii)          Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);

(viii)       Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);

(ix)             Vyama vya Wakulima (20); na

(x)                Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).

 

4.           Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.

5.           Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

 

6.           Kufuatia mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao. Mapendekezo hayo yalijumuisha majina 2,762 kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu 874. Hivyo basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria, watu 118 walijipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.

 

7.           Mchanganuo wa idadi ya watu walipendekezwa katika makundi mbalimbali ni kama ifuatavyo:

 

 

Na.

Kundi/Taasisi

Taasisi zilizoleta mapendekezo

Idadi ya Watu Waliopendekezwa

Idadi ya Wajumbe Wanaotakiwa

Idadi ya Walioteuliwa

Tanzania Bara

Zanzibar

Tanzania Bara

Zanzibar

Tanzania Bara

Zanzibar

1.     

Taasisi zisizokuwa za Kiserikali

246

98

1,203

444

20

13

7

2.     

Taasisi za Kidini

55

17

344

85

20

13

7

3.     

Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu

21

14

129

69

42

28

14

4.     

Taasisi za Elimu

9

9

84

46

20

13

7

5.     

Makundi ya Walemavu

24

6

97

43

20

13

7

6.     

Vyama vya Wafanyakazi

20

1

89

13

19

13

6

7.     

Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji

8

1

43

4

10

7

3

8.     

Vyama vinavyowakilisha Wavuvi

7

3

45

12

10

7

3

9.     

Vyama vya Wakulima

22

8

115

44

20

13

7

10.            

Makundi yenye Malengo Yanayofanana

142

21

613

114

20

14

6

 

Mapendekezo Binafsi

-

-

118

-

 

 

 

 

Jumla

672

178

2,880

874

201

134

67

 

Jumla Kuu

850

3,754

 

 

 

 

 

8.           Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba. Masharti hayo ni pamoja na wajumbe wasiopungua theluthi moja wanatakiwa kutoka Zanzibar na theluthi mbili kutoka Tanzania Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe 201, wajumbe 67 watatoka Zanzibar na wajumbe 134 watatoka Tanzania Bara. Aidha, mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na hayo, wajumbe hao wawakilishe sura ya wananchi wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama vya siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka. Katika mazingira haya, zoezi la kupata wajumbe 201 halikuwa rahisi hata kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.

9.           Kama nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa Zanzibar, majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua taasisi zisizo za kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara walipendekezwa watu 1,203, wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni 13 tu. Kwa upande Zanzibar, taasisi zisizokuwa za kiserikali zilikuwa zimependekeza majina 444 ikilinganishwa na nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.

 

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA

10.      Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:

(a)             Uteuzi umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijanawatu wazima na wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati miaka 22-35, ni wajumbe 35. Wajumbe wenye umri wa kati, yaani miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.

(b)             Sheria inataka kuwepo na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.

(c)              Uwakilishi wa vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe wawili umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa kutoka katika kila chama.

Baada ya maelezo hayo ya utangulizi, ifuatayo ndiyo orodha ya wajumbe 201 wa Bunge Maalum la Katiba waliobahatika kuteuliwa:

 

 

TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI- (WAJUMBE 20)

TANZANIA BARA (13)

1.     Magdalena Rwebangira

2.        Kingunge Ngombale Mwiru

3.     Asha D. Mtwangi

4.        Maria Sarungi Tsehai

5.     Paul Kimiti

6.        Valerie N. Msoka

7.     Fortunate Moses Kabeja

8.        Sixtus Raphael Mapunda

9.     Elizabeth Maro Minde

10.   Happiness Samson Sengi

11. Evod Herman Mmanda

12.   Godfrey Simbeye

13. Mary Paul Daffa

 

TANZANIA ZANZIBAR (7)

1.     Idrissa Kitwana Mustafa

2.          Siti Abbas Ali

3.     Abdalla Abass Omar

4.          Salama Aboud Talib

5.     Juma Bakari Alawi

6.          Salma Hamoud Said

7.     Adila Hilali Vuai

 

 

 

TAASISI ZA KIDINI- (WAJUMBE 20)

TANZANIA BARA (13)

1.   Tamrina Manzi

2.        Olive Damian Luwena

3.   Shamim Khan

4.        Mchg. Ernest Kadiva

5.   Sheikh Hamid Masoud Jongo

6.        Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela

7.   Magdalena Songora

8.        Hamisi Ally Togwa

9.   Askofu Amos J. Muhagachi

10.   Easter Msambazi

11.                                                           Mussa Yusuf Kundecha

12.   Respa Adam Miguma

13.                                                           Prof. Costa Ricky Mahalu

 

TANZANIA ZANZIBAR (7)

1.     Sheikh Thabit Nouman Jongo

2.     Suzana Peter Kunambi

3.     Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu

4.     Fatma Mohammed Hassan

5.     Louis Majaliwa

6.     Yasmin Yusufali E. H alloo

7.     Thuwein Issa Thuwein

 

 

 

 

 

VYAMA VYOTE VYA SIASA

VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE 42)

TANZANIA BARA (28)

1.        Hashim Rungwe Spunda

2.           Thomas Magnus Mgoli

3.        Rashid Hashim Mtuta

4.           Shamsa Mwangunga

5.        Yusuf  S. Manyanga

6.           Christopher Mtikila

7.        Bertha Ng’angompata

8.           Suzan Marwa

9.        Dominick Abraham Lyamchai

10.      Mbwana Salum Kibanda

11.   Peter Kuga Mziray

12.      Isaac Manjoba Cheyo

13.   Dr. Emmanuel John Makaidi

14.      Prof. Ibrahim Haruna Lipumba

15.   Modesta Kizito Ponera

16.      Prof. Abdallah Safari

17.   Salumu Seleman Ally

18.      James Kabalo Mapalala

19.   Mary Oswald Mpangala

20.      Mwaka Lameck Mgimwa

21.   Nancy  S. Mrikaria

22.      Nakazael Lukio Tenga

23.   Fahmi Nasoro Dovutwa

24.      Costantine  Benjamini Akitanda

25.   Mary Moses Daudi

26.      Magdalena Likwina

27.   John Dustan Lifa Chipaka

28.      Rashid Mohamed Ligania Rai

TANZANIA ZANZIBAR (14)

1.     Ally Omar Juma

2.     Vuai Ali Vuai

3.     Mwanaidi Othman Twahir

4.     Jamila Abeid Saleh

5.     Mwanamrisho Juma Ahmed

6.     Juma Hamis Faki

7.     Tatu Mabrouk Haji

8.     Fat –Hiya Zahran Salum

9.     Hussein Juma

10.     Zeudi Mvano Abdullahi

11.     Juma Ally Khatibu

12.     Haji Ambar Khamis

13.     Khadija Abdallah Ahmed

14.     Rashid Yussuf Mchenga

 

 

 

TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20)

TANZANIA BARA

1.     Dr. Suzan Kolimba

2.     Prof. Esther Daniel Mwaikambo

3.     Dr. Natujwa Mvungi

4.     Prof. Romuald Haule

5.     Dr. Domitila A.R. Bashemera

6.     Dr. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa

7.     Prof. Bernadeta Kilian

8.     Teddy Ladislaus Patrick

9.     Dr. Francis Michael

10.    Prof. Remmy J. Assey

11.               Dr. Tulia Ackson

12.               Dr. Ave Maria Emilius Semakafu

13.               Hamza Mustafa Njozi

 

TANZANIA ZANZIBAR (7)

1.     Makame Omar Makame

2.     Fatma Hamid Saleh

3.     Dr. Aley Soud Nassor

4.     Layla Ali Salum

5.     Dkt. Mwinyi Talib Haji

6.     Zeyana Mohamed Haji

7.     Ali Ahmed Uki

 

 

 

WATU WENYE ULEMAVU-(WAJUMBE 20)

TANZANIA BARA (13)

1.        Zuhura Musa Lusonge

2.     Frederick Msigala

3.        Amon Anastaz Mpanju

4.     Bure Zahran

5.        Edith Aron Dosha

6.     Vincent Venance Mzena

7.        Shida Salum Mohamed

8.     Dr. Henry Mwizengwa Nyamubi.

9.        Elias Msiba Masamaki

10.                   Faustina Jonathan Urassa

11.   Doroth Stephano Malelela

12.                   John Josephat Ndumbaro

13.   Ernest Njama Kimaya

 

TANZANIA ZANZIBAR (7)

1.     Haidar Hashim Madeweyya

2.     Alli Omar Makame

3.     Adil Mohammed Ali

4.     Mwandawa Khamis Mohammed

5.     Salim Abdalla Salim

6.     Salma Haji Saadat

7.     Mwantatu Mbarak Khamis

 

 

 

VYAMA VYA WAFANYAKAZI-(WAJUMBE 19)

TANZANIA BARA (13)

1.     Honorata Chitanda

2.     Dr. Angelika Semike

3.     Ezekiah Tom Oluoch

4.     Adelgunda Michael Mgaya

5.     Dotto M. Biteko

6.     Mary Gaspar Makondo

7.     Halfani Shabani Muhogo

8.     Yusufu Omari Singo

9.     Joyce Mwasha

10.                   Amina Mweta

11.                   Mbaraka Hussein Igangula

12.                   Aina Shadrack Massawe

13.                   Lucas Charles Malunde

 

TANZANIA ZANZIBAR (6)

1.   Khamis Mwinyi Mohamed

2. Jina Hassan Silima

3.   Makame Launi Makame

4. Asmahany Juma Ali

5.   Mwatoum Khamis Othman

6. Rihi Haji Ali

 

 

VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAFUGAJI-(WAJUMBE 10)

TANZANIA BARA (7)

1.     William Tate Olenasha

2.     Makeresia Pawa

3.     Mabagda Gesura Mwataghu

4.     Doreen Maro

5.     Magret Nyaga

6.     Hamis Mnondwa

7.     Ester Milimba Juma

 

TANZANIA ZANZIBAR (3)

1.     Said Abdalla Bakari

2.     Mashavu Yahya

3.     Zubeir Sufiani Mkanga

 

 

 

VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAVUVI –(WAJUMBE 10)

TANZANIA BARA (7)

1.     Hawa A. Mchafu

2.     Rebecca Masato

3.     Thomas Juma Minyaro

4.     Timtoza Bagambise

5.     Tedy Malulu

6.     Rebecca Bugingo

7.     Omary S. Husseni

 

TANZANIA ZANZIBAR (3)

1.     Waziri Rajab

2.     Issa Ameir Suleiman

3.     Mohamed Abdallah Ahmed

 

 

 

VYAMA VYAWAKULIMA-(WAJUMBE 20)

TANZANIA BARA (13)

1.     Agatha  Harun Senyagwa

2.     Veronica Sophu

3.     Shaban Suleman Muyombo

4.     Catherine Gabriel Sisuti

5.     Hamisi Hassani Dambaya

6.     Suzy Samson Laizer

7.     Dr. Maselle Zingura Maziku

8.     Abdallah Mashausi

9.     Hadijah Milawo Kondo

10.                                                   Rehema Madusa

11.                  Reuben R. Matango

12.                                                   Happy Suma

13.                  Zainab Bakari Dihenga

 

TANZANIA ZANZIBAR (7)

1.     Saleh Moh’d Saleh

2.     Biubwa Yahya Othman

3.     Khamis Mohammed Salum

4.     Khadija Nassor Abdi

5.     Fatma Haji Khamis

6.     Asha Makungu Othman

7.     Asya Filfil Thani

 

 

 

WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20)

TANZANIA BARA (14)

1.        Dr. Christina Mnzava

2.     Paulo Christian Makonda

3.        Jesca Msambatavangu

4.     Julius Mtatiro

5.        Katherin Saruni

6.     Abdallah Majura Bulembo

7.        Hemedi Abdallah Panzi

8.     Dr. Zainab Amir Gama

9.        Hassan Mohamed Wakasuvi

10.               Paulynus Raymond Mtendah

11.   Almasi Athuman Maige

12.               Pamela Simon Massay

13.   Kajubi Diocres Mukajangwa

14.               Kadari Singo

TANZANIA ZANZIBAR (6)

1.     Yussuf Omar Chunda

2.     Fatma Mussa Juma

3.     Prof. Abdul Sheriff

4.     Amina Abdulkadir Ali

5.     Shaka Hamdu Shaka

6.     Rehema Said Shamte

 

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

 

7 Februari, 2014

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA NCHINI LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo wakati akitoa hotuba yake kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigawa rasimu ya katiba kwa viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa vyama vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad katika picha ya pamoja na wenyeviti wa vyama vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa vyama vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maali Seif Shariff Hamad   wakiongozana na Sehemu ya viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa,wakitoka katika mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.Picha na Issa Michuzi.
 Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akisoma dua kabla ya kikao hicho cha Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili kuanza katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaa
 Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa wakiomba dua katika kikao hicho cha Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili kabla ya kuanza katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
  Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa katika kikao hicho cha Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili  katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
   Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa katika kikao hicho cha Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili kuanza katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
   Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa katika kikao hicho cha Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
   Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya siasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha APPT-Maendeleo, Mhe Peter Mziray akisoma hotuba yake katika  kikao hicho cha Baraza la Vyama Vya Siasa vyenye usajili  katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala toka kwa Mwenyekiti wa Barza la Vyama vya Siasa Mhe. Peter Mziray
 Viongozin wakisikiliza hotuba kwa makini
 Viongozi wa vyama vya siasa wakiwa kikaoni hapo
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akiwa na Kamishna Isaya Mungulu Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai DCI wakiwa wageni waalikwa kikaoni hapo
 Rais Kikwete akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho
 Rais Kikwete akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho
 Rais Kikwete akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho
 Viongozi wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete
 Rais Kikwete akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa kikao hicho
 Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
 Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
 Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
 Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
 Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
 Wajumbe wakifiuatilia hotuba ya Rais Kikwete
 Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
 Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
 Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
 Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe na Katibu wake Mhe Wilbroad Slaa wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete kwa makini
 Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe akifuatilia hotuba hiyo
 Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
 Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
 Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake
 Viongozi wakimpigia makofi Rais Kikwete
 Viongozi wakiangua kicheko 
 Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akitoa neno la shukurani
 Rais Kikwete, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariffa Hamad, Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi na viongozi wa vyama na maafisa wa serikali wakitelemka ngazini baada ya kupata chakula cha mcha pamoja
 Rais Kikwete na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariffa Hamad wakiongea
 Sehemu ya wajumbe wa kikao
 Wajumbe wa kikao
 Wajumbe kikaoni
 Wajumbe kikaoni
 Rais Kikwete akiendelea na hotuba
 Wajumbe wakisikiliza kwa makini
 Rais Kikwete akimalizia hotuba yake
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Pokea rasimu ya katiba mheshimiwa…
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akikabidhi kwa viongozi wa vyama vya siasa nakala za rasimu ya katiba mpya
 Rais Kikwete akisalimiana na Mhe Tundu Lissu baada ya kufungua kikao
 Rais Kikwete, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika picha ya kumbukumbu na wenyeviti wa vyama vya siasa baada ya ufunguzi wa kikao hicho
 Rais Jakaya Kikwete akipongezwa na Mhe Freeman Mbowe kwa hotuba nzuri
 Picha ya pamoja na viongozi wa vyama vya siasa
 Picha ya pamoja na makatibu wakuu wa vyama vya siasa
 Picha ya pamoja na wajumbe wa kikao
 Picha ya pamoja na viongozi wa dini na wa vyama vya siasa pamoja na wageni waalikwa
 Rais Kikwete akiongea na Mhe James Mapalala
 Rais Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila
 Mhe William Lukuvi akisalimiana na Mhe Wilbroad Slaa
 Rais Kikwete, Maalim Seif Shariff Hamad, Jaji Francis Mutungi Mhe Peter Mziray na Mhe Freeman Mbowe wakitoka nje ya ukumbi
 Rais Kikwete akiongea na viongozi baada ya kufungua kikao hicho
Rais Kikwete akiagana na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya siasa Mhe Peter Mziray na viongozi wengine.

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAJENGO YA BUNGE MJINI DODOMA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi inayokarabati na kufanyia marekebisho ukumbi wa bunge mjini Dodoma tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi huu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali za majengo ya Bunge jijini Dodoma alikotembea kukagua inayokarabati na kufanyiwa marekebisho tayari tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi huu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua sehemu ya kukalia katika Ukumbi wa Bunge  mjini Dodoma alikotembea kukagua maendeleo ya ukarabati na kufanyiwa marekebisho tayari kwa kupokea wajumbe wa Bunge la katiba baadaye mwezi huu.PICHA NA IKULU

RAIS JAKAYA KIKWETE AGUSWA NA UTENDAJI KAZI WA KINANA, ATAKA AWE MFANO WA KUIGWA

 Rais Kikwete akihutubia maelfu ya watu waliofika kwenye sherehe hizo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete leo amevunja ukimya na kuzungumzia suala la mawaziri waliotuhumiwa na wananchi kuwa mizigo wakati wa ziara za Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadhi ya wajumbe wa sekretarieti katika mikoa kadhaa nchini mwishoni mwa mwaka jana.
“Najua wapo baadhi ya watanzania, walitaka Mawaziri waliotajwa kuwa ni mizigo wafukuzwe kazi, na kwa vile halikufanyika basi suala hilo limegeuzwa kuwa la malumbano,  ni vyema ieleweke kuwa kuitwa kwa Mawaziri hao na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakuna maana ya kuishia kufukuzwa”, alisema, Kikwete leo akihutubia maelfu ya watu katika sherehe za kilele cha miaka 37 ya CCM, kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. 
Alisema Mawaziri hao waliitwa kwa sababu ya kuwepo matatizo yaliyoonekana yanatakiwa yapatiwe ufumbuzi, matatizo hayo yamezungumzwa na maelekezo kutolewa kuhusu nini cha kufanya.
“Kamati Kuu ya CCM imetimiza wajibu wake uliobaki ni wa serikali.Kamati Kuu itaendelea kufuatilia na kama hakuna maendeleo ndipo inapoweza kuamua kuomba mamlaka ya uteuzi ichukue hatua zipasazo dhidi ya mhusika.Huko hatujafika” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alimpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisema, ziara ambazo amekuwa akifanya ni mfano unaopaswa kuigwa na viongozi wengine hasa wa CCM kwa sababu ndio hasa unaotakiwa.
Alisema ziara za Kinana zinakijenga Chama na kutoa taswira nzuri ya CCM katika jamii kwani zinahuisha uhai wa CCM kwa kuwa Katibu Mkuu huyo katika ziara hizo huenda hadi kwa wanachama waliopo ngazi za chini.
“Katibu Mkuu Kinana amekuwa anafanya mambo ambayo baadhi ya watu wanadhani kuwa ni mageni, lakini katika kufanya hayo amekuwa pia akionyesha umahiri na ujasiri mkubwa kwa kwenda  maeneo ambayo ni magumu kufikika” alisema Rais Kikwete na kuongeza;
“Katika ziara hizo  wakati mwingine amekuwa anatumia njia za usafiri zinazoogopesha, amewahi kutumia meli  ya MV Songea kutoka mkoani Ruvuma hadi Mbeya, amepanda milima na mabonde kwa magari katika maeneo ambayo ni hatari, lakini lengo likiwa ni kuhakikisha anawafikia wanachama wa ngazi za chini kabisa”.
Rais Kikwete alisema mambo mengine yalivyomvutia katika ziara za Kinana, ni hatua ya Katibu mkuu huyo kwenda kukaa na  kula na wananchi katika ngazi za chini na kisha kufanya nao kazi za maendeleo  na zaidi kutoa fursa kwa wananchi kueleza matatizo na manung’uniko yanayowasibu.
Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa alisema Katibu mkuu wa Chama amekuwa anashiriki katika kutafuta majawabu na matatizo anayoambiwa hali ambayo imesaidia sana kumaliza baadhi ya matatizo kulekule mikoani.
“Pale ambapo pamekuwa panahitaji hatua zaidi za serikali hakusita kutoa taarifa kwa Waziri Mkuu, vile vile amekuwa anatoa taarifa ya ziara zake kwenye Kamati Kuu ya CCM” alisema Rais Kikwete.

RAIS KIKWETE AONGOZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA KUZALIWA CCM MKOANI MBEYA LEO

Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia Wananchi na Wanachama wakereketwa wa chama hicho,mapema leo jioni kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea kilele cha miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio hilo.
 Sehemu ya Umati wa Watu waliofika kwenye shamrashamra hizo leo.
Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika jembe na nyundo,ikiwa ni alama ya Mkulima na Mfanyakazi mara baada ya kuwasili jioni ya leo kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio hilo. 
Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,mara baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama cha CCM jioni ya leo. 
Katibu wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.
Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete  akimkabidhi zawadi ya gitaa Msanii maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awil,anaeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi.Zakia Meghji. 
 Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakifuatilia yanayojiri hivi sasa ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine,mkoani Mbeya juu ya kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
Mmoja wasanii Mwimbaji na Mwigizaji wa filamu,ajulikanae kwa jina la kisani kama Dokii akiimba mbele ya umati mkubwa wa wananchi na wanachama wa CCM waliofika kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama cha CCM,ndani ya uwanja wa Kumbukumbu ya  Sokoine,mkoani Mbeya
Kikundi cha TOT Plus kiongozwa na gwiji wa mipasho hapa nchini,Khadija Kopa wakiimba jukwaani.
JB akizungumza machace kwa niaba ya wenzake mara baada ya kutamka kuwa wamejiunga na chama cha CCM.
Wasanii hao wa Filamu wakifurahia jambo jukwaani.
Nape na wanachama wengine wakiserebuka kwa raha zao.
 
Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa chama hicho,Ndugu Kinana akiwapungia wananchi na wanachama wa CCM,waliofika kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya.
 Nape Nnauye akiwa amembeba mtoto ambaye alionesha umahiri wake mkubwa wa kucheza ngoma ya kiasili.
 Vijana wenye umri wa miaka 37 wakirusha njiwa angani kuashiria amani,utulivu na mshikamano wetu tulionayo.
 Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye sherehe hizo jioni ya leo. 
 Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akipiga gitaa kabla ya kumzawadia msanii wa muziki maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awilo.
Vijana wa Halaiki.

RAIS KIKWETE AONGOZA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO YA MIAKA 37 YA CCM JIJINI MBEYA,KUHUTUBIA TAIFA MCHANA WA LEO

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete  akiwapungia mkono
baadhi ya Wananchi (hawapo pichani),walioshirikia matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya mapema leo asubuhi,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kushoto kati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji wakishiriki matembezii hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa jijini humo.Rais Kikwete ambaye ndiye mgeni rasmi wa sherehe hizo atahutubia leo  mchana kwenye maadhimisho ya sherehe hizo zitakazofanyika katika uwanja wa Sokoine mkoani humo.
Rais Kikwete akiongoza  matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto akiwa sambamba na baadhi ya watoto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kushoto kati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji wakishiriki matembezii hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa jijini humo. 
 Baadhi ya vijana wakereketwa na chama cha CCM wakiwa na mabango yao. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete (pilia kulia) akiwa tayari kuongoza wanachana na Wananchi (hawapo pichani) kushiriki matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya
Soweto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya mapema leo asubuhi,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM,Bwa.Phillip Mangula,wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji pamoja na Waziri Ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum,Prof Mark Mwandosya wakiwa tayai kuyaanza matembezi hayo.
 Rais Kikwete akizungumza na baadhi ya watoto waliokuwa miongoni mwa watoto waliojitokeza kushiriki  matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto mapema leo asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
 Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakishiriki kuchukua matukio yaliyokuwa yakijiri kwenye matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto mapema leo asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele
cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete akipokelewa na viongozi wa chama hicho ngazi za juu,pichani akisalimiana na  Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana na anaeshuhudia pichani kati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM,Mh.Phillip Mangula,tayari kwa kuongoza matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
 Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto mapema leo asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akifurahi jambo na Waziri Ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum,Prof Mark Mwandosya 
 Ndugu Kinana akizunguza jambo na Mwigulu Nchemba kabla ya kuanza matembezi ya mshikamano. 
  Msafara wa Rais ukiwasili sehemu ya kuanza matembezi ya mshikamano. 

 Mambo ya matembezi ya mshikamani yakiwa yameiva

 Rais Kikwete pia aliungana na Watoto katika matembezi hayo. 

 Mwenyekiti wa CCM,Rais Kikwete akiwasili kwenye bustani za uwanja wa Sokoine kufikia kilele cha matembezi ya mshikamano

 Sehemu ya Wananchi na wakereketwa wanachama mbalimbali wa wa CC Mwakiwa wamekusanyika kwa pamoja tayari kumsikiliza Rais Kikwete mara baada ya kumaliza matembezi hayo yalifanikiwa kwa kiasi kikubwa.
 Baada ya kumaliza matembezi ya mshikamano viongozi wa juu wa CCM,wakisiliza utaratibu wa kuadhimisha sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
 
Rais Kikwete akizungumza machache mara baada ya kumaliza matembezi ya mshikamano,Rais Kikwete atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo zitakazoanza mapema leo mchana ndani ya uwanja wa Sokoine,jijin Mbeya.

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU JIJINI DAR LEO

Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Ummy Mwalimu, kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha George Boniface Tuguluvala Simbachawene, kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Kaika Saning’o Telele, kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakia katika picha ya pamoja na Waziri na Manaibu Waziri walioapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wapya na wa zamani wa Ofisi yake, baada ya kuapishwa wapya katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kutoka (kulia) ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Muhangwa Kitwanga, ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu na aliyekuwa Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Terezya Huvisa, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR.

Finland’s Prime Minister Jyrki Katainen arrives in Dar es salaam for three-day state visit

The car carrying Finland’s Prime Minister Jyrki Katainen arrives at the East Gate of the State House in Dar es salaam this morning for his official reception, ahead of his three-day visit of Tanzania.
 
The purpose of their visit is to strengthen bilateral relations and trade and development links, as well as promoting export and internationalisation opportunities for Finnish companies in Ethiopia and Tanzania. In Tanzania,The ministers will also conduct negotiations on bilateral development cooperation. The trip to Tanzania will include a short visit to Zanzibar.
 
During this Team Finland trip for the promotion of exports and internationalization, the Prime Minister and the Minister for International Development will be accompanied by a business delegation, assembled by Finpro, with representatives from 27 Finnish companies. The companies involved operate internationally in the fields of energy, infrastructure construction, logistics, the information society, extractive industry, education, health, and agriculture and forestry.
 

  Finland’s Prime Minister Jyrki Katainen stands at attention for the national anthems with his host President Jakaya Kikwete
 Gun-salute for  Finland’s Prime Minister Jyrki Katainen
  A member of  TPDF Brass band play as Finland’s Prime Minister Jyrki Katainen arrives at the State House
 Finland’s Prime Minister Jyrki Katainen receives red carpet reception 

PRESIDENT KIKWETE OPENS THE AGRIBUSINESS CONGRESS EAST AFRICA IN DAR ES SALAAM

 

 President Jakaya Mrisho Kikwete arrives at the Serena Inn in Dar es salaam to officially open the Agribusiness Congress East Africa , 28 JANUARY, 2014

 

 Warm welcome from the Serena staff
 Heading for the function hall
 Introductory speech
 Part of the participants
  Eng. Christopher Chiza, (MP), Minister of
Agriculture, Food Security and Cooperatives, invites the President
 A cross section of participants following up the proceedings
 Click…
 President Kikwete delivers his keynote speech
 Participants listen attentively
 It’s a full house
 I thank the organisers for choosing Tanzania to
play host to this important meeting: the Agribusiness Congress East Africa. I
also commend them for organising the Congress so well and for choosing the
theme “
Driving Innovation for
Agricultural Development in East Africa”.
 

 


 ”Three key things need to be done by nations.  First, is to develop visions, plans and
programmes to anchor innovation in agriculture.

Secondly, is to provide adequate financial, human and technological
resources needed to implement the plans and programmes.
  And, last but not least empower farmers to
participate effectively in the implementation of the plans and programmes of
innovation in agriculture…”
 
 RSA Seed and Grain pavillion
 Pesticide sprayers
 SEEDCO pavillion
 Silo specialists
 At the Afrivet pavillion
 At the AECF pavillion
 At TECHNOSERVE pavillion
 at ETG
The President with  Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT) officers
 Special handshake for Mr. Geoffrey Kirenga, CEO of the Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT)
 Manam sower
 More pamphlets
 Mahindra tractor
 Mahindra staff
With a  giant John Deere tractor
 Tractors
 More exhibits
 A souvenir photo with the organisers
 Group photo with the exhibitors
 President Kikwete greets Professor Msolwa
 Special photo op
Welcome again, sir…
 The President leaves the venue a happy man
Thank you Your Excellency for sparing your time for us

The day WAMA Nakayama girl’s Secondary school in Rufiji went digital with Opportunity tablets…

 Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts from Omaha, Nebraska, in the US signs the visitor’s book upon arrival at the WAMA Nakayama Girl’s Secondary School at Nyamisati village in Rufiji District, Coast Region, January 27, 2014 as hostess Tanzania First Lady and school founder Salma Kikwete with the school’s Chairman of Board of Directors Dr Ramadhani Dau look on prior to the launch of the a programme that aims at providing Tanzania secondary
school students with tablets pre-loaded with educational materials.
 Wanawake na Maendeleo (WAMA) Chairperson Tanzania First Lady Salma Kikwete welcomes Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts  on prior to the launch of the a programme that aims at providing Tanzania secondary school students with tablets pre-loaded with educational materials.
 Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts from Omaha, Nebraska, in the US presents a Chicago Cubs jersey to his hostess Tanzania First Lady and school Salma Kikwete 
  Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts from Omaha, Nebraska, in the US heads for the hall of  the WAMA Nakayama Girl’s Secondary School at Nyamisati village in Rufiji District, Coast Region January 27, 2014 with hostess Tanzania First Lady and school founder Salma Kikwete and  the school’s Chairman of Board of Directors Dr Ramadhani Dau and headmistress
 Standing ovation as the VIP’s enter the hall
  Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts from Omaha, Nebraska, in the US stand at attention   as the National Anthem and school song raise the curtains upon arrival at the WAMA Nakayama Girl’s Secondary School at Nyamisati village in Rufiji District, Coast Region January 27, 2014 with  hostess Tanzania First Lady and school founder Salma Kikwete, Minister for Education and Vocational Education Dr Shukuru Kawambwa (right) with the school’s Chairman of Board of Directors Dr Ramadhani Dau (left)
 WAMA Nakayama students sing the National Anthem
 Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts from Omaha, Nebraska, in the US stand at attention   as the National Anthem and school song raise the curtains upon arrival at the WAMA Nakayama Girl’s Secondary School at Nyamisati village in Rufiji District, Coast Region January 27, 2014 with  hostess Tanzania First Lady and school founder Salma Kikwete, Minister for Education and Vocational Education Dr Shukuru Kawambwa (right) with the school’s Chairman of Board of Directors Dr Ramadhani Dau (left)
  WAMA Nakayama school’s Chairman of Board of Directors Dr Ramadhani Dau makes his welcome note
 WAMA Nakayama ..school Headmistress Ms Tuma Mensa delivers her speech
 One of WAMA beneficiaries gives his testimony 
 Representative of the Opportunity Education Foundation in Tanzania Mbakileki Mutahaba speaks out about the Opportunity Tablet programme
 Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts from Omaha, Nebraska, in the US makes a brief speech
 Traditional entertainment by WAMA Nakayama students
 Friends of WAMA Nakayama
 PPF Director General Mr William Erio (left) whose instution is one of the major donors was also in attendance
 A short play the students
 Minister for Education and Vocational Education Dr Shukuru Kawambwa gives his statement
 Coast Regional Commissioner Hon. Hajat Mwantumu Mahiza speaks
 Chairman of the Opportunity Education Foundation Joe Ricketts gets ready to hand over the tablets with  a word or two to Tablet
Manager from the foundation’s office in Tanzania, Ms Sandra Tetty.
 
 Tablet
Manager from the foundation’s office in Tanzania, Ms Sandra Tetty hand over one of the tablets to 
First Lady and school founder Salma Kikwete, Minister for Education and Vocational Education Dr Shukuru Kawambwa (right) with the school’s Chairman of Board of Directors Dr Ramadhani Dau and school’s headmistress Ms Tuma Mensa
 
 irst Lady and school founder Salma Kikwete in return hands over the tablets to students
 A visibly excited student holds shows off her tablet to the rolling cameras
 Mr Joe Ricketts joins in to bask in the warmth of the historical moment
 First Lady and school founder Salma Kikwete gives her statement of gratitude
 Some of the WAMA Nakayama students
 Tablet tutor sits with the students
 Another standing ovasion for First Lady as she and her guests leave the hall
 A group photo with members of the Opportunity Education Foundation team
 With WAMA Nakayama teachers and administrators
 With student representatives
 With Nyamisati Village leaders
 With WAMA Nyamisati friends
 Form two students with the tablets
 Now, this is awesome….
 PPF Director General Mr William Erio offers some tips on how to operate the Kindle-like Opportunity tablets
 Now, where is the log in icon?
 Hey, you have to log in first…
 Open sesame!
 Simply can’t believe this is happening to us…
 Okay, show us how its done…
 Girls, I have decided to offer a tablet to each students of the entire school…
 Sir, thank you…
 Okay, Sir, I start by logging in my personal details…Easy like ABC
 Well, Sir, it took me just under ten minutes to grasp how to use this. We are very, very thankful for your generosity, Sir. We really are….
 Minister for Education and Vocational Education Dr Shukuru Kawambwa is happy and thankful for this pilot programme
 Multi-tablet charging decks. One full charge lasts for over eight hours.
 And this is our humble library…
 At the computer lab
Hey, i told you no Facebook, Instagram of Whatsapp in here…. Just lessons and important references like wikipoedia and encyclopedia etc. Good for us, ain’t it?
 
A NEW era dawned in Tanzania’s digital education landscape today when a programme that
aims at providing secondary school students with tablets pre-loaded with educational materials was launched.
The programme’s ultimate goal is to provide each secondary school student in the country with a tablet to enable them access educational materials electronically.
It will be implemented by the government and an American NGO — Opportunity Education Foundation (OEF).
Implementation will begin with a pilot phase in 10 secondary schools on Tanzania Mainland and Zanzibar, which will involve provision of about 1,100 tablets pre-loaded with Science, Mathematics, Geography and History materials for Form Two students. 
Each Form Two student in those schools will get one tablet, according to Tablet Manager from the foundation’s office in Tanzania, Ms Sandra Tetty.
The donation makes Tanzania the first country in the world to receive the tablets
under the OEF educational support programme, which earmarks 34 countries around the globe.
Launching of the programme involved handing over of 61 tablets to WAMA Nakayama Girls Secondary School at Nyamisati in Rufiji District by OEF Founder, Mr Joe Ricketts.
They were received by the Minister for Education and Vocational Training, Dr Shukuru Kawambwa and WAMA Chairperson, Mama Salma Kikwete. Mr Ricketts pledged a further donation of tablets for the entire school.
Dr Kawambwa hailed the donation, saying it was a valuable support to the government in its effort to improve the quality of education in the country through technology.
He noted that when rolled out throughout the country, the programme would go a long way toward addressing the shortage of teachers and text books in secondary schools.
The minister said his ministry had prepared science and mathematics content for secondary schools, which would be loaded into the tablets ready to be used by the students, while efforts to digitalise materials for other subjects go on.
This would entail replacement of the content in the donated tablets, which according to Ms Tetty, is about 60 per cent relevant to the country’s O level and A level syllabuses.
“We are committed in this. We have started and there will be no going back,” said the minister, adding that the government was also planning to use Tele-Presence technology in which one teacher can teach students in different schools connected to the system at the same time.
He said tomorrow he would launch a small model of the technology, which would be used to smoothen operations at his ministry.
Dr Kawambwa commended Mama Salma and WAMA for being a ‘’shoulder on which to lean’’ in the effort to promote education, especially targeting disadvantaged children.
President Jakaya Kikwete met with Mr Ricketts at the State House in Dar es Salaam on Sunday, where he thanked the OEF Founder for supporting development of the country’s education sector.
The president underscored the importance of science and technology for development,saying he strongly believed that the use of tablets in secondary schools would help address various challenges facing the sector The customised Opportunity Education Tablets are fitted with simplified features that allow easy access of the content and uploading of any other educational materials. They also have long battery life.
Beneficiaries of the pilot phase will be Form Two students at Ilboru, Mzumbe, Msalato, Fidel
Castro (Pemba), WAMA Nakayama (Coast), Bwiru Boys, J Ossian (Bukoba), Laureatte (Zanzibar), Notredame (Arusha) and Tusiime (Dar es Salaam).The 10 schools are part of 33 secondary schools which have been receiving support from the foundation.
 

Rais aamuru Jeshi kusimamia utoaji huduma kwa waathirika wa mafuriko Morogoro

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Daraja la Mto Mkundi mkoani Morogoro linalokarabatiwa baada ya kuharibiwa na mafuriko hivi karibuni.Rais Kikwete alitembelea eneo hilo na sehemu nyingine zilizokumbwa na mafuriko hayo kujionea uharibifu. Picha na Freddy Maro wa Ikulu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi la Ulinzi na
Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameliamuru Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) kuanza mara moja kazi ya kusimamia utoaji huduma kwa watu
walioathiriwa na mafuriko katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni pamoja na kusimamia
ujenzi wa nyumba za muda wa wahanga hao.
Rais
pia ameliamuru Jeshi kupeleka mashine za kusafisha maji katika makambi ambako
wahanga hao wa mafuriko ya Januari 22, mwaka huu wanaishi kwa muda.
Aidha,
Rais Kikwete amewahakikishia wahanga wa mafuriko hayo kuwa Serikali
itahakikisha inawapatia huduma zote za msingi ikiwa ni pamoja na chakula,
malazi, maji na huduma za afya hadi hapo watakapokuwa na uwezo wa kuanza
kujitegemea tena.
Rais
Kikwete ametoa amri hizo kwa Jeshi leo, Januari 27, 2014, wakati alipotembelea
kambi za wahanga wa mafuriko hayo kuwajulia hali walioathirika katika makambi
yaliyoko Shule ya Sekondari ya Magole katika eneo la Dumila na katika Kijiji
cha Mateteni kilichoko Dakawa, Wilaya ya Kilosa.
Katika
hotuba zake fupi baada ya kuwa ametembelea na kuona mahema ambamo wahanga hao
wanalala, Rais Kikwete amesema   ameagiza
Jeshi kuongoza harakati za kuwahudumia wahanga hao kwa sababu zikifuatwa
taratibu za kawaida za Kiserikali huduma zitachelewa sana kuwafia waathirika.
“Kazi
yetu ni kusimamia maisha ya watu hasa
kipindi cha shida za namna hii. Tukifuata taratibu za kawaida za
Kiserikali za tenda tutachelewesha sana huduma za dharura kwa waathirika. Ndiyo
maana nimeliamuru Jeshi kufanya kazi hii ikiwa ni pamoja na kujenga haraka
makazi ya muda wa waathirika,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Katika
mazungumzo hayo na Mkuu wa Majeshi, nimemwagiza pia kuleta mashine za kusafishia
maji ili kuhakikisha kuwa watu wanakunywa maji salama kwa sababu katika hali ya
sasa maji yasiyokuwa salama yanaweza kuwa chanzo cha magonjwa.”
Kuhusu
upatikanaji wa chakula cha msaada kwa wahanga, Rais Kikwete amesema kuwa
Serikali inacho chakula cha kutosha kwa ajili yao. “Tunacho chakula cha kutosha
na hata kile tusichokuwa nacho tutanunua. Tutabanana ndani ya Serikali ili
tupate fedha za kutosha za kuwahudumia.”
Kuhusu
malazi, Rais amesema:”Naambiwa kuna upungufu wa magodoro. Tutahakikisha kuwa
yanapatikana na yatafika katika siku mbili zijazo. Hatutaki watu walale chini
na waje kupata vichomi.”
                        Kuhusu
maji, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa huduma ya maji bure
kwa wahanga. “Tutaendelea kutoa bure huduma hii mpaka hapo huduma ya kawaida ya
maji itakapoanza kupatikana tena.”
Kuhusu
huduma za afya, Rais amesema kuwa anafurahi kuwa kila kambi ya wahanga inayo
huduma ya afya ambayo itaendelea kutolewa kwa kadri watu wanavyozidi kuishi
kwenye makambi.
Rais
ameagiza kuwa baada ya muda mfupi viongozi wa Mkoa wa Morogoro na wilaya husika
wakae chini ya viongozi wa ngazi za chini na wahanga kujadili na kutafuta
mwafaka kuhusu maisha ya baadaye ya wahanga – hasa kuhusu namna gani wanaweza
kupatiwa maeneo yaliyoko nje ya mikondo ya mafuriko.

 

                        “Hili
ni lazima kwa sababu hata kama imechukua miaka mingi kwa mafuriko ya sasa
kutokea ni dhahiri kuwa iko siku yatakuja tena – inaweza kuwa hata mwaka huu
kwa sababu zipo mvua za masika. Kwa hiyo ni lazima tukubaliane jinsi gani ya
kurudi ama kutokurudi katika maeneo yetu tulikotoka.”   

RAIS KIKWETE AKABIDHIWA JEZI YA TIMU YA CHICAGO CUBS TOKA KWA MWENYEKITI WA TIMU HIYO,JOE RICKETTS,PIA APOKEA TABLET 61 KWA AJILI YA WANAFUNZI WA SHULE YA WAMA NAKAYAMA

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi ya timu ya baseball ya Chicago Cubs toka kwa mmiliki wa timu hiyo na Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea akipokea moja ya Tabuleti 61 kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014.
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama Dkt Ramadhani Dau na Mkuu wa Shule hiyo wakipokea moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts akikabidhi moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule hiyo.
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama Dkt Ramadhani Dau na Mkuu wa Shule hiyo wakiangalaia matumizi ya ya Tabuleti 61 katika darasa la kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts akikabidhi moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule hiyo.PICHA NA IKULU.

RAIS KIKWETE AONGOZA WANANCHI WA MIONO KATIKA MAZIKO YA ALIYEKUWA MBUNGE WA CHALINZE, SAID BWANAMDOGO

 Rais Jakaya Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Said Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Said Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Said Bwanamdogo, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Miono leo wakati wa shughuli za maziko.

 Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwaongoza waombolezaji kuswalia mwili wa marehemu Said  Bwanamdogo, aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, aliyefariki juzi. Mazishi ya mbunge huyo yamefanyika leo kijijini kwao Miono.

  Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na kiuongozi wa kambi ya upinzani bungeni na Mwenyekiti wa Chadema, Mhe Freeman Mbowe (kushoto) na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, na Mbunge wa Monduli Mhe Edward Lowassa, wakati wakiwa katika maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Said Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi.

 Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwasili makaburini

 Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwaongoza waombolezaji katika mazishi ya marehemu Said Ramadhan Bwanamdogo,

 Sehemu ya waombolezaji

 Sehemu ya waombolezaji kinamama

 Baadhi ya waomboilezaji

 Rais Jakaya Kikwete, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Said Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Said Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo.

Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi hayo

RAIS KIKWETE AKIWA NA NAIBU RAIS WA KENYA MHE WILLIAM RUTO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa baadhi ya viongozi wa Kenya na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo Ijumaa January 24, 2014. Viongozi hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi, na kupanda ndege moja kuelekea nyumbani. Rais Kikwete ambaye alitua nairobi kwa muda, alikuwa akitokea Davos, Uswisi, alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba wa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said Bwanamdogo, ambaye amefariki dunia Januari 22, 2014 katika wodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (Moi) alikokuwa akitibiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni huku akishuhudiwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto na balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda Buriani walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo January 24, 2014. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo January 24, 2014. Viongozi hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi, na kupanda ndege moja kuelekea nyumbani. Rais Kikwete, aliyetua Nairobi kwa muda, alikuwa akitokea Davos, Uswisi, alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba wa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said Bwanamdogo, ambaye amefariki dunia Januari 22, 2014 katika wodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (Moi) alikokuwa akitibiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo.PICHA NA IKULU

MAMA SALMA KIKWETE AANDAA SHERRY PARTY KWA WAKE WA MABALOZI WA NCHI ZA NJE WAISHIO HAPA TANZANIA

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya (sherry party) aliyowaandalia wake wa mabalozi wa nchi za nje walioko hapa nchini. Sherehe hiyo ilifanyika Ikulu tarehe 23.1.2014.
Kiongozi wa Umoja wa wake wa mabalozi waliopo hapa Tanzania Mama Celine Mpango, (ambaye ni Mke wa Balozi Juma Mpango wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) akitoa salamu zake kwa niaba ya wanajumuia hiyo wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika Ikulu Trahe 23.1.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mume wa Balozi wa Zambia hapa nchini Bwana Victor Nsemiwe wakati wa sherry party aliyowaandalia wake wa mabalozi wa nchi za nje walioko hapa Tanzania. Sherehe hiyo ilifanyika Ikulu tarehe 23.01.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wake wa mabalozi wa nchi za nje walioko Tanzania pamoja na wageni wengine huko Ikulu tarehe 23.1.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Mke wa Balozi wa DR Congo Mama Celine Mpango (kushoto), Mama Asha Bilal (mke wa Makamu wa Rais), Mama Sitti Mwinyi na mwisho ni Mama Anna Mkapa wakielekea sehemu ya tafrija mara baada ya kupiga picha ya pamoja.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na Mama Celine Mpango (kushoto) akifuatiwa na Mama Sitti Mwinyi, Mama Khadija Mwinyi, Mama Asha Bilal na Mama Anna Mkapa.
Mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mama Celine Mpango na Mama Asha Bilal wakati wa sherry party aliyowaandalia wake wa mabalozi wa nchi za nje waliopo hapa Tanzania huko Ikulu tarehe 23.1.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI.

SHUGHULI MBALIMBALI ZA RAIS KIKWETE AKIWA MJINI DAVOS, USWISI

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa mkutano wa kujadili namna ya kuongeza kasi ya uboreshaji wa kilimo uliofanyika mjini Davos,Uswisi usiku wa kuamkia leo Januari 23, 2014.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza,Mhe. Niuck Clegg wakati walipokutana na kufanya mazungumzo katika hoteli ya Sheraton mjini Davos, Uswisi leo Janaury 23, 2014.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya JETRO ya Japan katika hoteli ta Sheraton mjini Davos,  Uswisi leo January 23, 2014.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya JETRO ya Japan katika hoteli ta Sheraton mjini Davos, Uswisi leo January 23, 2014.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani (USAID) Mhe Rajiv Shah katika ukumbi wa mikutano wa Davos, Uswisi, January 23, 2014.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani (USAID) Mhe Rajiv Shah mara baada ya mazungumzo yao katika ukumbi wa mikutano wa Davos, Uswisi, January 23, 2014.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika mkutano wa kujadili namna ya kuongeza kasi ya uboreshaji wa kupatikana na kulinda maji salama kwa miaka ijayo katika hoteli ya Derby,mjini Davos Uswisi Januari 23, 2014.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa mara baada ya kuhutubia wakati wa mkutano wa kujadili namna ya kuongeza kasi ya uboreshaji wa kupatikana na kulinda maji nsalama kwa miaka ijayo katika hoteli ya Derby,mjini Davos Uswisi Januari 23, 2014. PICHA NA IKULU.

RASIMU YA KATIBA KUTANGAZWA KWENYE GAZETI LA SERIKALI

Kifungu 20 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83, Toleo la 2013 inamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchapisha kwenye Gazeti la Serikali Rasimu ya Katiba ndani ya siku thelathini (30) baada ya kukabidhiwa rasimu hiyo na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inaeleza kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alikabidhiwa Rasimu ya Katiba tarehe 30 Desemba, 2013, na ataichapisha kwenye Gazeti la Serikali litakalotolewa Ijumaa, tarehe 24 Januari 2014.

Aidha, kifungu 22 (1) (c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83, Toleo la 2013, kinampa madaraka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushauriana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kuteua wajumbe 201 wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka miongoni mwa majina yanayopendekezwa kwao na makundi yaliyotajwa ndani ya Sheria hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anakusudia kukamilisha uteuzi wa Wajumbe hao baada ya kushauriana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mwanzoni mwa wiki ijayo na majina hayo kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali kama kifungu 22 (3) cha Sheria iliyotajwa inavyomtaka kufanya.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu

Dar es Salaam.

22 Januari, 2014

RAIS KIKWETE APOKEA HATI YA UTAMBULISHO YA BALOZI WA OMAN NCHINI

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Oman hapa nchini Mhe.Soud Ali Bin Mohamed Al Ruqaishi. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 21 Januari, 2014.
Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Ruqaishi Mhe. Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Ruqaishi, Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Ruqaishi (wa pili kushoto) na Maafisa waliofuatana na Balozi huyo.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi Ruqaishi mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho
Balozi Ruqaishi akimshukuru Kiongozi wa Bendi ya Polisi.Picha na Rosemary Malale, Mambo ya Nje

 

MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA MAJADILIANO YA WADAU KUHUSU KUTOKOMEZA MAAMBUKIZI YA VVU TOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mheshimiwa Dkt. Seif Rashid, kwenye hoteli ya Serena alikoenda kufungua mkutano wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto tarehe 21.1.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid (kulia) na Mheshimiwa Mama Zakhia Meghji, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA, (kushoto), wakielekea kwenye chumba cha mkutano.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akifungua rasmi mkutano wa siku moja wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto uliofanyika kwenye hoteli ya Serena tarehe 21.01.2014.
Dr. Khadija Mwamtemi kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili, alikuwa ni mmojawapo kati ya washiriki waliochangia mawazo yao mara baada ya mada mbalimbali kutolewa.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku moja wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete (hayupo pichani). Mkutano huo ulifanyika katika hoteli ya Serena hapa Dar es Salaam tarehe 21.1.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU JIJINI DAR LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe. Dkt. Hussein Ali
Mwinyi (Mb)
 Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
 Mhe. Mathias Meinrad
CHIKAWE (Mb) 
Waziri wa Mambo ya Ndani akila kiapo
 Mhe. Dkt. Asha-Rose
Mtengeti MIGIRO (Mb) 
Waziri wa Katiba na Sheria
 Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb) Waziri
wa Maliasili na Utalii akila kiapo
 Mhe.
Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb) 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii akila kiapo
Rais Kikwete akimuapisha  Mhe.
Saada Mkuya SALUM (Mb) 
Waziri wa Fedha
 Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas
KAMANI (Mb) 
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi akila kiapo
Mhe.
Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)
 Naibu Waziri wa Fedha akila kiapo
 Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb) Naibu Waziri (Nishati) akila kiapo
 Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb) Naibu
Waziri wa Maji
 Mhe. Janet Zebedayo MBENE
(Mb) 
Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara
 Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akila kiapo
 Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto akila kiapo
 Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) Naibu
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika akiapishwa
 Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)  Naibu Waziri wa Fedha akila kiapo
                        
 Mhe.
Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb) 
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii akila kiapo
  Mhe. Juma Selemani NKAMIA
(Mb) 
Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo
Mhe.
Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb) 
 Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii
 Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi wakipozi na mawaziri na manaibu waziri baada ya hafla ya kula viapo
 Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi wakipozi na mawaziri baada ya kiapo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb) Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
 Rais Kikwete na baadhi ya wanafamilia ya Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani 
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria
  Rais Kikwete na familia ya Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb) Waziri wa Maliasili na Utalii 
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
 Rais Kikwete na baadhi ya wanafamilia wa  Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) Waziri wa Fedha
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb) Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi 
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha 
 Rais Kikwete na familia ya Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb) Naibu Waziri (Nishati)
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb) Naibu Waziri wa Maji
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi 
 Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto 
 Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika 
 Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)  Naibu Waziri wa Fedha
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb) Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
 Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
  Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb) Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii 
 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali akiwa na baadhi ya mawazir na naibu waziri waliokula kiapo leo
  Rais  Kikwete na Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakiwa na makamanda na viongozi katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
 Rais Kikwete na Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani wakiwa na wakuu wa vyombo vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani
 Rais Kikwete akiongea na Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani na wakuu wa vyombo mbalimbali vya dola vilivyo chini ya wizara ya mambo ya ndani
 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani akiwa na viongozi wa vikosi mbalimbali vilivyo chini ya wizara yake
Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA Naibu Waziri wa Fedha na Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya fedha. PICHA NA IKULU.

RAIS KIKWETE AKABIDHIWA RASIMU YA PILI YA KATIBA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Rasimu ya pili ya Katiba Mpya kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa hafla ya kukabidhiwa rasimu hiyo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete aliitaka Tume hiyo ya Katiba kuhakikisha kuwa Rasimu hiyo inawekwa kwenye mitandao yote ya kijamii ili wananchi waweze kuisoma na kuielewa na kuweza kutoa maoni yao kwa urahisi kupitia mitandaoni.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akipokea Rasimu ya pili ya Katiba Mpya kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa hafla ya kukabidhiwa rasimu hiyo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal mara tu baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Shareef Hamad.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili,Mzee Ali Hasaan Mwinyi.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rasimu hiyo kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mzee Cleopa Msuya.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mh. Pandu akipokea Rasimu hiyo.
Spika wa Bunge.
Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu wa Zanzibar.
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue.

Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,Jaji Joseph Sinde Warioba akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kukabidhi kwa Rais,Rasimu ya Pili ya Katiba iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee,jijini Dar es Salaam.Jaji Warioba alisema kuwa kulingana na idadi ya kura zilizopatikana kutoka kwa wananchi kuhusu uundwaji wa Serikali tatu, alisema kuwa idadi kubwa zaidi ni ya watu waliohitaji Serikali tatu kuliko walioipinga, hivyo Serikali tatu haipingiki ambapo kwa sasa itabaki ni kazi ya maamuzi ya Bunge la Katiba linalotarajia kuundwa mapema mwezi Januari mwakani.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mhe. Joseph S. Warioba mara baaada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee Hall kupokea Rasimu ya Pili ya Katiba. Kulia ni Mhe. Assaa Rashid, Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, 
 Rais Kikwete akisalimiana na Mhe Assaa Rashid, Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, 
 Rais Kikwete akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu huku Jaji Mkuu wa Tanzania Bara Mhe Mohamed Chande Othman, Spika wa Bunge la Muungano Mhe Anne Makinda na Spika wa Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho wakisubiri zamu zao
 Rais Kikwete akimuamkia  na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi
 Rais Kikwete akimuamkia Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Cleopa David Msuya
 Meza kuu
 Sehemu ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
 Jukwaa kuu la pili
 Sehemu ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
 Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim akiwa na wajumbe wenzie wa Tume na maofisa wa serikali
 Dkt Asha Rose Migiro, Mama Amne Salim na Mama Warioba
 Sehemu ya wananchi walioshuhudia tukio hilo la kihistoria
 Wananchi wakiwa katika hafla hiyo
 Wananchi wakifuatilia hafla hiyo
 Watangazaji wa TBC wakiwa kazini kurusha live tukio hilo
 Baadhi ya wazee mashuhuri katika hafla hiyo. 
 Wadau mbalimbali
 Wadau katika hafla hiyo
 Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa
 Wadau wa habari 
 Wanasheria nguli, Mzee Mark Bomani na Profesa Issa Shivji wakiwa miongoni mwa wadau
 Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe Alfani Mpango akijumuika na wadau
 Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na mabalozi
 Wadau na maafisa wa serikali
 Maafisa wa ofisi wa Masajili wa vyama
 Wadau
 Wadau na maafisa mbalimbali
 Makatibu wakuu
 Mawasiri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
 Mawaziri wa Bara na Zanzibar
 Mawaziri, wabunge na maafisa wa serikali
 Sehemu ya mawaziri wa bara na wa Zanzibar
 Msajili wa vyama vya siasa Jaji Mutungi (wa tatu kushoto) akiwa ameketi na wabunge na viongozi wa vyama mbalimbali 
 Sehemu ya waliohudhuria hafla hiyo
 Meza kuu ikimsikilia Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mhe. Joseph S. Warioba 
 Rais Kikwete akimkabidhi Sir George Kahama nakala ya Rasimu ya Pili ya Katiba
 Rais Kikwete akiwakabidhi Mzee Hassan Nassoro Moyo na Jenerali Sarakikya nakala ya Rasimu ya Pili ya Katiba
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akisoma hotuba yake
 Rais Kikwete akihutubia
 Wabunge na wadau wengine wakifurahia hotuba ya Rais Kikwete
 Rais Kikwete, Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali wakiwapongeza wajumbe wa Tume kwa kazi nzuri
 Picha ya pamoja ya viongozi wakuu na wajumbe wa Tume
 Picha ya pamoja ya viongozi wakuu, wajumbe wa tume 
 Viongozi wakuu, viongozi wa vyama vya siasa na wajumbe wa Tume
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na Mhe Tundu Lissu
 Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba 
 Rais Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na Mbunge wa Kuteuliwa Mhe James Mbatia
Nikiripoti kutoka hapa katika viwanja vya Karimjee ni mimi…. wa Mlimani TV

PICHA NA IKULU

SOMA RASIMU HIYO HAPO CHINI

Rais Kikwete akutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani 24/12/2013.
 
Bwana Ban Ki Moon alimwalika Rais Kikwete ambapo viongozi hao wawili walijadili masuala mbalimbali ya kimataifa hususan masuala ya amani na ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika kudumisha amani sehemu mbalimbali Afrika na katika nchi nyingine duniani. Tanzania ina majeshi ya kulinda amani katika nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Darfur nchini Sudan na Lebanon.
 
Rais Kikwete yupo jijini New York nchini Marekani ambapo anaendelea vyema na ukaguzi wa kawaida wa afya yake.(picha na Freddy Maro)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwaajili ya kufanya mazungumzo nae.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Mazungumzo na Mwenyeji wake,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon alipomtembelea ofisi kwake jijini New York, Marekani 24/12/2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyeji wake,Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon mara baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini New York, Marekani 24/12/2013.

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA NELSON MANDELA, AONGEA KIJIJINI QUNU AFRIKA KUSINI

 
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Dkt Dlamini Zuma kwa hotuba ya kusisimua aliyoitoa wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Kushoto ni Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Malawi Mhe. Joyce Banda. Rais Kikwete alialikwa kuzungumzia sifa za mapambano ya ukombozi aliyoongoza Mzee Madiba ambapo Tanzania ndiyo ilikuwa ni nchi yake ya kwanza kusaidia mapambano yote ya ukombozi kusini mwa Afrika kwa kuwahifadhi na kuwapa misaada ya hali na mali wapigania ukombozi wake.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wageni wengine akitoka katika hema maalumu lililotumika kwa shughuli za mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Wa tatu kulia ni Mrithi wa kiti cha Ufalme wa Uingereza Prince Charles.PICHA NA IKULU

Rais Kikwete ahudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Kenya

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete(kulia) wakihudhuria sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Kenya zilizofanyika katika uwanja wa Michezo wa Kasarani mjini Nairobi leo.Kushoto ni Mwenyeji Rais Wa Kenya Uhuru Kenyatta.Watatu kushoto ni Naibu Rais Wa Kenya William Ruto,Watano Kushoto ni Waziri Mkuu wa Ethiopia Haile Mariam Desalegn, na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi na mkewe.(picha na Freddy Maro)

MAMA SALMA KIKWETE AMLAKI MALKIA WA UHOLANZI LEO

 Malkia Maxima kwa pamoja na Mhe. Mama Salma wakifurahia burudani kutoka kwa
mojawapo ya vikundi vilivyokuwepo uwanjani wakati wa mapokezi.
Malkia Maxima wa Uholanzi akiwa amefuatana na Mwenyeji wake Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. Mwingine pembeni ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Raymond Mushi.
 
Wakuu wa Wilaya za Kinondoni na Temeke, Mhe. Jordan Rugimbana (wa nne kutoka kushoto)
na Mhe. Sophia Mjema (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa uwanjani hapo wakati wa mapokezi ya Malkia Maxima. Wengine ni Balozi Dora Msechu (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Victoria Mwakasege (wa pili kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika na Bw. Songelaeli Shila, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa  katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Mama Salma akimtambulisha kwa Malkia Maxima  Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Ne na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu. Pembeni kwa Balozi Msechu ni Bibi Victoria Mwakasege,Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Ulaya na Amerika.
Malkia Maxima kwa pamoja na Mama Salma wakifurahia  wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshoghulikia masuala ya Chakula (WFP), Bi. Ertharin Cousin akiwaeleza jambo mara baada ya Malkia Maxima kuwasili nchini.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini, Dkt. Alberic Kacou (kushoto) akiwaeleza jambo Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi,Mhe. Wilson Masilingi (katikati)  na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mhe.
Jaap Frederics wakati wa mapokezi ya Malkia Maxima wa Uholanzi.

Rais Kikwete shughuli ya kumbukumbu ya mzee nelson mandela nchini afrika kusini

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya Kumbukumbu ya Mzee Nelson Mandela Uwanja wa FNB jijini Johannesburg Jumanne Novemba 10, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Rais Barack Obama wa Marekani kwa viongozi mbalimbali wa Afrika wakati wa hafla ya Kumbukumbu ya Mzee Nelson Mandela Uwanja wa FNB jijini Johannesburg Jumanne Novemba 10, 2013.PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE AWASILI AFRIKA KUSINI KUHUDHURIA MAZIKO YA MZEE NELSON MADELA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili nchini Afrika Kusini usiku wa kuamkia leo  Desemba 10, 2013 tayari kuhudhuria maziko ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya serilai, Ibada Kuu ya kumwombea Marehemu itafanyika leo Desemba 10, 2013 katika Uwanja wa FNB Johannesburg, ambapo viongozi na watu mashuhuri mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wataungana na wananchi wa Afrika Kusini katika shughuli hiyo ya kihistoria. 
Kesho Novemba 11 hadi Novemba 13, 2013 mwili wa marehemu utakuwepo katika jengo la Union Building ambapo viongozi na watu mashuhuri watatoa heshima zao za mwisho. Jengo hilo ni kama Ikulu ya nchi hiyo.
Maziko yatafanyika Desemba 15, 2013 katika kijiji cha Qunu, Mthatha, Easter Cape
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria alikowasili usiku wa kuamkia leo tayari kuhudhuria mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson R. Mandela.
Rais Kikwete akisalimiana na Mwambata wa Kijeshi katika Ubalozi wa Tanzania Afrika kusini katika uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake mwenye ushungi kichwani ni Mama Salma Kikwete
Rais Kikwete akisindikizwa kuelekea kwenye gari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Waterkloof Airforce Base ulioko Kusini mwa jiji la Pretoria . Nyuma yake kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahman Kinana. PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA UHURU LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi alipokua akiwasili uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea salam ya Rais na kupigiwa mizinga 21 kutoka kwa gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi ya Tanzania leo uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi na usalama leo uwanja wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.
Sehemu ya askari wa vikosi vya ulinzi na usalama wakiwa wamesimama kwa ukakamavu wakati kabla ya kamanda wa gwaride kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kukagua gwaride hilo leo jijini Dar es salaam.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akiwasili jukwaa kuu la Uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo.
Gwaride likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa mwendo wa haraka.
Rais Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakati gwaride la vikosi vya Ulinzi na Usalama likipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa haraka.
Baadhi ya Maofisa wa jeshi wakipiga saluti wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.
Picha na 9.Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam waliojitokeza kuhudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.
Wananchi wakifatilia
Vijana wa halaiki kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakitamka kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo jijini Dar es salaam ambayo ni “ Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu,Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ta Taifa Letu”.
Vijana wa halaiki wakiendelea kuwasilisha jumbe mbalimbali kama inavyoonekana mfano wa mnyama aina ya samba kuashiria utalii katika hifadhi za wanyama za Tanzania.
Vijana wa halaiki wakionyesha ukakamavu.
Baadhi ya Maafisha wa Jeshi wakitoa salamu.
Ujumbe ukiwasilishwa kwa njia ya picha kuhusu viongozi wapigania Uhuru wa Tanzania Bara, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hatuba fupi kwa watanzania wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Hatuba yake licha ya kujaa maneno ya kumkumbuka rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Rolihlahla Mandela Madiba aliyeaga dunia juzi nchini Afrika ya Kusini imesisitiza Upendo, Amani, Mshikamano miongoni mwa watanzania na kukemea tabia ya baadhi ya viongozi kulipiza kisasi pindi waingiapo madarakani.
Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein (kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo katika uwanja wa Uhuru wakati wa Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.
Raia wa kigeni waliohudhuria sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.
Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange alipokua akisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Freeman Mbowe akiwa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO

President Kikwete Speaks at the Ends of the Elysee Summit

President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a joint press conference at the end of the Elysee Summit for Peace and Security held in Paris and ended this afternoon. The Summit discussed among other things, Peace and Security in Africa, The Economic partnership and Development and Climate Change. Others in the pictures from left The UN Secretary General Ban Ki Moon, The host French President Francois Hollande and right is Senegal’s President Macky Sall(photos by Freddy Maro).

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AKIFUNGA RASMI MKUTANO WA MAWAZIRI WA NCHI ZA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA KUHUSU ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA VIJANA

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Botswana na Mjumbe wa High Level Group Dr. Festus Mogae wakati wa kikao cha Mawaziri wa Elimu na Afya kutoka nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaofanyika Cape Town nchini Afrika Kusini tarehe 7.12.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na viongozi waandamizi waliohudhuria mkutano wa High Level Group hukom Cape Town wakisimama kwa dakika moja kwa ajili ya kumkumbuka hayati Rais Nelson Mandela. Kutoka kushoto ni Bwana Enver Surty, Waziri wa Elimu ya Msingi wa Afrika Kusini, Dr. Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana, Mama Salma, Bwana Luiz Loures, Naibu Mkurugenzi Mtendaji, UNAIDS, Dr. Julitha Onabanjo, Naibu Mkurugenzi Mkuu, UNFPA, Bwana Qian Tang, Naibu Mkurugenzi Mkuu-Elimu- UNESCO, Bwana Geeta Rao Gupta, Naibu Mkurugenzi Mtendaji, UNICEF.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Hussein Mwinyi akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa High Level Group unaofanyika huko Cape Town kuzungumzia elimu ya afya ya uzazi na ukimwi kwa vijana katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mawaziri wa Elimu na Afya kutoka nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wakiapa kwa niaba ya nchi zao kutekeleza majukumu waliyopitisha kwenye kikao cha High Level Group, kuhusiana na elimu ya afya ya uzazi ( comprehensive sexuality education and sexual and reproductive health services) mwishoni mwa kikao cha siku mbili kilichofanyika huko Cape Town.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha na Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Bwana Michel Sidibe wakionyesha umuhimu wa dhana nzima ya mkutano wa High Level Group ( YOUNG PEOPLE TODAY, TIME TO ACT NOW) kuhusiana na masuala ya elimu ya afya ya uzazi kwa vjijana katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa Mawaziri kutoka nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika kuhusu elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wa nchi hizo. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika nchini Afrika Kusini katika Mji wa Cape Town tarehe 6-7.12.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipongezwa na Dr. Julitha Onabanjo, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa UNFPA kwa hotuba aliyoitoa wakati wa kufunga mkutano wa siku mbili wa Mawaziri wa Elimu na Afya kutoka katika Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika huko Cape Town.
Baadhi ya washiriki wa mkutano waqkisikiliza hotuba ya ufungaji iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete huko Cape Town nchini Afrika Kusini tarehe 7.12.2013.
Baadhi ya washiriki wa mkutano waqkisikiliza hotuba ya ufungaji iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete huko Cape Town nchini Afrika Kusini tarehe 7.12.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoka kwenye ukumbi wa mkutano baada ya kuufunga rasmi huku akisindikizwa na washiriki baada ya kutoa hotuba (BEYOND THE COMMITMENT) iliyosisimua wajumbe wa mkutano huo.PICHA NA JOHN LUKUWI

MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA HIGH LEVEL GROUP KUHUSU ELIMU NA AFYA KWA VIJANA WA NCHI ZA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini ya Afrika wa UNAIDS na Mwenyekiti wa High Level Group Profesa Sheila Tlou wakati wa ufunguzi wa mkutano wa High Level Group unaofanyika Cape Town nchini Afrika Kusini tarehe 6.12.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa siku mbili wa High Level Group, unaofanyika huko Cape Town tarehe 6 na 7, Desemba 2013. Mkutano huo unazungumzia masuala ya elimu na afya kwa vijana wanaoishi katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na viongozi wengine wa High Level Group wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kanda wa UNAIDS, Profesa Sheila Tlou na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Mheshimiwa Jesca Eriyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa siku mbili wa High Level Group, unaofanyika huko Cape Town tarehe 6 na 7, Desemba 2013. Mkutano huo unazungumzia masuala ya elimu na afya kwa vijana wanaoishi katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza kijana Remmy Shawa, mjumbe wa High Level Group mara baada ya kutoa mada yake ‘Background to the East and Southern Africa Commitment Process’ kwenye mkutano wao wa siku mbili unaofanyika Cape Town nchini Afrika Kusini tarehe 6.12.2013.PICHA NA JOHN LUKUWI

Na Anna Nkinda, Cape Town.

Jamii imetakiwa kushirikiana kwa pamoja na kuchukua hatua za karibu kwa kuwalea watoto wa kike kama watoto wao wa kuwazaa huku wakiwapa nafasi kama watoto wa kiume, kuwapatia elimu, kuwaheshimu na kuwalinda jambo ambalo litawafanya wafanikiwe katika maisha yao.

Wito huo umetolewa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwenye mkutano wa kamati maalum ya viongozi wanaoshughulikia huduma na elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka nchi za Jumuia ya Afrika ya Mashariki (EAC) na Jumuia ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kikanda kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika katika Hoteli ya The Westin iliyopo mjini Cape Town nchini Afrika ya Kusini.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema tafiti zinaonyesha Duniani kote zaidi ya wasichana milioni 58 wameolewa wakiwa na umri wa chini ya miaka 18 kati ya hao milioni 15 wanaumri wa kati ya miaka 10 hadi 14 huku wengi wao wakiwa wameolewa kinyume na matakwa yao na kushuhudia unyanyasaji wa kijinsia, uelewa mdogo wa haki zao na kutopata elimu ya afya ya uzazi.

“Idadi ya watoto wa kike wanaomaliza elimu ya msingi imeongezeka na kuwazidi watoto wa kiume ingawa idadi ya wasichana wanaomaliza elimu ya Sekondari ni ndogo ukilinganisha na watoto wa kiume katika nchi nyingi za Afrika”, alisema Mama Kikwete.

Kwa upande wa maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi Mama Kikwete alisema asilimia 42 ya watu wanaopata maambukizi ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24, katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara vijana ni asilimia 80.

Mama Kikwete alisema, “Nchini Tanzania tafiti zilizofanyika zimeonyesha kuwa watoto wa kike wengi wanajihusisha na mahusiano ya kimapenzi mapema kwa asilimi 13 ambao wanafanya mapenzi kabla ya umri wa miaka 15 na kwa upande wa watoto wa kiume ni asilimia saba matokeo yake ni upatikanaji wa mimba za utotoni.

Msichana mmoja kati ya wasichana wanne wenye umri wa miaka 15 hadi 19 ni mjamzito au ameshazaa. Idadi hii ni kubwa katika nchi nyingi za Afrika inasikitisha kwani kubeba mimba katika umri mdogo kunaweza kusababisha kifo cha mama mjamzito pamoja na mtoto wakati wa kujifungua”.

Akifungua mkutano huo wa siku mbili Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupamba na Ukimwi (UNAIDS) Prof. Sheila Tlou alisema wajumbe wa kamati hiyo wanatakiwa kuhakikisha maazimio waliyokubaliana yanapitishwa na kufanyiwa kazi katika nchi husika ili vijana waweze kupata elimu ya afya ya uzazi.

Prof. Tlou alisema, “Tutahakikisha kuwa rasilimali za kutosha zinapatikana ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha kutoka kwa wafadhili mbalimbali hii ni kuhakikisha kuwa maadhimio haya yanafanikiwa kwani vijana ni viongozi wa leo wanaohitaji kupata huduma ikiwa ni pamoja na elimu ili waweze kujiepusha na mazingira ambayo yatawapelekea kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi”.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa EAC Jesca Eriyo alisema mwaka mmoja uliopita wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki walikubaliana kuhakikisha wanaimarisha utolewaji wa elimu ya afya ya uzazi katika nchi zao na hivyo kuwa rahisi kwa nchi hizo kufanyika kazi maazimio hayo.

“Vijana wanamaswali mengi kuhusu afya ya uzazi na inafika wakati hawajui wa kumuuliza hivyo basi elimu ya uzazi ifundishwe kwao kwani kutokana na mila za kiafrika ni vigumu kwa mzazi kuongea na mtoto wake kuhusu afya ya uzazi”, alisema Eriyo.

Alimalizia kwa kusema kuwa vijana wanatakiwa kujua hali ya afya zao ikiwa ni pamoja na kupima kama wamepata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kujiepusha na wababa na wamama (mafataki) ambao wanaweza kuwarubuni na kuwaharibia maisha yao jambo ambalo litasababisha kupatikana kwa kizazi kizuri hapo baadaye.

Kamati hiyo imekutana kwa mara ya pili kwa ajili ya kupitia rasimu ya maazimio ya kuhakikisha kuwa vijana wote katika nchi zilizopo ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kusini wanapata elimu kuhusiana na afya ya uzazi na ujinsia jambo ambalo litawasaidia kufahamu zaidi ugonjwa Ukimwi kwamara ya kwanza ilikutana mwezi wa nane nchini Botswana.

Makubaliano hayo yanatarajiwa kusainiwa na mawaziri wa Afya na Elimu kutoka nchi 21 za Afrika Mashariki na Kusini ambayo inatakuwa ni sehemu ya utekelezaji kwa nchi kabla ya kufanyika kwa mkutano wa kimataifa wa vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi na magonjwa ya zinaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni mjini humo.

President Kikwete Participates in MEETING ON ELEPHANT AND OTHER ENDANGERED SPECIES

President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete together with some heads of States from Africa who participated on the Roundtable meeting on Elephant and other endangered species held in Paris France this afternoon. 

Others in the picture from left Commoro’s President Dr. Ikililou Dhoinine,(left), Cameroon President Paul Biya (Third left) The Host President Francois Hollande of France (fourth), Togolese President Faure Eyadema (fifth), Gabon’s President Ally Bongo (second right), and right is Ivory Coast’s President Allasane Ouatarra. President Kikwete is in Paris for a working visit. Photos by Freddy Maro.


Rais Jakaya Kikwete Ahitimisha Ziara Yake Nchini Poland

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Fatma Fereji wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Nchi katika Makamu wa Rais Dkt Tereiya Huvisa wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Katibu Mkuu  katika Ofisi ya Makamu wa  Rais  Mhe Sazi Salula  wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono Mwandishi wa Uhuru na Mzalendo Bw. Ramadhani Mkoma wakati akaiaga na kuondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika. Kushoto ni mwandishi wa ITV Bw. Emmanuel Buhohela, akifuatiwa na Naibu Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi na Msaidizi wa Waziri Huvisa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Terezya Huvisa na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Fatma Fereji wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika.Picha Zote na IKULU

PRESIDENT KIKWETE AT THE UN CLIMATE CHANGE CONFERENCE (COP19/CM9) IN WARSAW, POLAND

President Jakaya Mrisho Kikwete addresses African Ministerial Conference on the Environment (AMCEN) Ministers and African Group of Negotiatiors (AGN) in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Warsaw National Stadium in Warsaw, Poland, November 21, 2013.
President Jakaya Mrisho Kikwete holds talks with the Commissioner of Agriculture and Rural Economy of the Africa Union in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Bristol hotel in Warsaw, Poland, November 21, 2013.
President Jakaya Mrisho Kikwete greets the Secretary General of the World Meteorological Organisation Mr Michael Jarraud as the Director General of the Tanzania Meteorological Agency Dr. Agnes Kijazi looks on in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Bristol hotel in Warsaw, Poland, November 21, 2013.
President Jakaya Mrisho Kikwete poses with the Secretary General of the World Meteorological Organisation (WMO) Mr Michael Jarraud, Assistant Secretary General pf WMO Ms Elena Manaenkova and the Director General of the Tanzania Meteorological Agency Dr. Agnes Kijazi when they met in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Bristol hotel in in Warsaw, Poland, November 21, 2013.
President Jakaya Mrisho Kikwete holds talks with the Secretary General of the World Meteorological Organisation (WMO) Mr Michael Jarraud and Assistant Secretary General pf WMO Ms Elena Manaenkova (left). Right is the Director General of the Tanzania Meteorological Agency Dr. Agnes Kijazi when they met in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Bristol hotel in in Warsaw, Poland, November 21, 2013.
President Jakaya Mrisho Kikwete addresss a High Level Meeting on Caring for Climate Business Dialogue that was also attended by the UN Secretary General Hon Ban Ki Moon in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Warsaw National Stadium in Warsaw, Poland, November 20, 2013.STATE HOUSE PHOTOS.

PRESIDENT KIKWETE’S STATEMENT AND PHOTOS AT THE UN CONFERENCE ON CLIMATE CHANGE IN WARSAW, POLAND

Coordinator of the Commitee of African Heads of State and Government on Climate Change President Jakaya Mrisho Kikwete addresses the UN Conference on Climate Change (COP19/CMP9) in Warsaw, Poland.
UN Secretary General Ban Ki Moon addresses the UN Conference on Climate Change (COP19/CMP9) in Warsaw, Poland.
The Tanzania delegation to the UN Conference on Climate Change (COP19/CMP9) in Warsaw, Poland.
A section of the crowd at the UN Conference on Climate Change (COP19/CMP9) in Warsaw, Poland.
Coordinator of the Commitee of African Heads of State and Government on Climate Change President Jakaya Mrisho Kikwete with members of the Tanzania delegation at the UN Conference on Climate Change (COP19/CMP9) in Warsaw, Poland.PHOTOS BY STATE HOUSE

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA MAENDELEO YA MINAZI WA SRI LANKA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokutana na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara (shati jeupe) na ujumbe wake mjini Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi inayotokana na zao la mnazi toka kwa Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara (shati jeupe) na ujumbe wake mjini Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
Picha ya pamoja ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara (shati jeupe) na ujumbe wake mjini Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia njia za kushirikiana
kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
PICHA NA IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Serikali imedhamiria kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
 
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa ni muhimu kwa Serikali kuchukua hatua za kukabiliana na tatizo la minazi kwa sababu watu wengi katika baadhi ya maeneo ambayo uchumi wake unategemea zao la mnazi wanakabiliwa na hatari ya kweli kweli ya kuathirika kwa maisha yao.
 
Rais Kikwete ametoa uhakikisho huo jana, Jumamosi, Novemba 16, 2013, wakati alipokutana na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara na ujumbe wake mjini Colombo. Waziri huyo aliandamana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti ya Minazi ya Sri Lanka.
 
Rais Kikwete yuko nchini Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Madola (CHOGM) unaomalizika leo, Jumapili, Novemba 17, 2013. Mkutano huo wa siku tatu, ulianza juzi, Ijumaa, Novemba 15, 2013.
 
Mheshimiwa Pushpakumara na ujumbe wake walikuwa wanamwelezea na kumkabidhi Rais Kikwete Ripoti ya Magonjwa ya Minazi iliyoandaliwa na wataalam wa minazi wa Sri Lanka ambao walitembelea Tanzania Julai mwaka huu.
 
Wataalam hao walitembea Tanzania na kufanya utafiti kuhusu ugonjwa unaolikabili zao la minazi kufuatia ahadi ya Rais Mahinda Rajapaksa aliyoitoa kwa Rais Kikwete wakati alipofanya ziara rasmi ya Tanzania Juni 27, 2013, na baadaye kushiriki katika Mkutano wa Smart Partnership Juni mwaka huu.
 
Rais Rajapaksa alitoa ahadi hiyo baada ya kuelezwa na Rais Kikwete kuhusu zao la kukauka kwa minazi nchini. Mnazi ni zao muhimu sana katika uchumi wa Sri Lanka na ni zao tegemeo kwa wananchi wa Taifa-Kisiwa hilo kilichoko kusini mashariki mwa India katika Barahri ya Hindi.
 
Wataalamu waliofuatana na Waziri huyo wamemwambia Rais Kikwete kuwa ugonjwa unaolikabili zao hilo la minazi ambao pia unashambulia minazi katika eneo la Caribbean hauna tiba kwa sababu mpaka sasa hakuna taasisi yoyote ya utafiti imegundua dawa hiyo.
 
Wataalam hao ambao walikaa Tanzania kwa wiki moja, zikiwamo siku mbili katika Zanzibar, wanasema kuwa zao hilo la mnazi, kama ilivyo katika nchi nyingine zinazolima zao hilo, lina uwezo mkubwa wa kusaidia uchumi kupitia viwanda vidogo vidogo.
 
Wakati wakiwa Tanzania, wataalam hao wa Sri Lanka walifanya uchunguzi na utafiti kwa karibu na wataalam wa Taasisi ya Utafiti ya Kilimo ya Mikocheni (MARI).

RAIS KIKWETE AKUTANA NA PRINCE CHARLES JIJINI COLOMBO, SRI LANKA, AHUDHURIA UFUNGUZI WA CHOGM 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwana wa Malkia  Elizabeth II wa Uingereza, Prince Charles,  jijini Colombo, Sri Lanka, leo Novemba 15, 2013 pembeni ya mkutano wa Wakuu wa nchi za Junuiya ya Madola (CHOGM 2013) ambako Prince Charles, maarufu zaidi kama His Royal Highness the Prince of Wales, anamwakilisha mama yake mwenye umri wa miaka 87 ambaye hakuhudhuria kwa mara ya kwanza katika miaka 40 ya historia ya mkutano huo unaofanyika kila baada ya miaka miwili katika nchi itayoteuliwa mwishoni mwa mkutano. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe Peter Kallaghe.
Malkia Elizabeth wa II alihudhuria CHOGM kwa mara ya kwanza mwaka 1973 jijini Ottawa, akiwa kakosa kikao cha mwaka 1971, na tokea hapo hajakosekana tena hadi safari hii. Alikuwepo pia katika mkutano wa mwisho uliofanyika mwaka 2011 jijini  Perth, Australia. Na hii ni mara ya kwanza kwa Prince Charles kumwakilisha mama yake ambaye imesemekana hakwenda Sri Lanka kutokana na ushauri wa kutosafiri umbali mrefu. Ila katika CHOGM 2007 iliyofanyika Kampala, Uganda, yeye na mama yake walihudhuria pamoja.


Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Uingereza, Prince Charles ambaye pia ni Mtoto wa Malkia wa nchi hiyo, Malkia Elizabeth II ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua zake za dhati za kulinda wanyamapori na kupambana na ujagili dhidi ya tembo na faru. 
 Aidha, Prince Charles amesema kuwa yuko tayari kuunga mkono juhudi hizo za Tanzania kwa kushirikiana na mtoto wake, Prince William ambaye amechagua shughuli za kulinda wanyamapori na kupambana na ujangili duniani kama moja ya shughuli zake kuu. 
 Moja ya hatua ambazo Prince Charles ameamua kuchukua ni kukabiliana na soko la bidhaa kuu za ujangili duniani, na hasa meno ya tembo na faru, na kufanya kampeni kubwa duniani dhidi ya biashara hiyo haramu. 
 Prince Charles ametoa pongezi hizo na msimamo wake wa kuunga mkono jitihada za Tanzania wakati alipokutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Viongozi hao wamekutana kwenye Jumba la Tintagel mjini Colombo, Sri Lanka, ambako amefikia wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) ambao Prince Charles ameufungua rasmi asubuhi ya leo, Ijumaa, Novemba 15, 2013, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mahinda Rajapaksa. 
Rais Kikwete naye yuko Sri Lanka kuhudhuria Mkutano huo. Wakati wa mazungumzo hayo, Rais Kikwete ametumia muda mrefu kumwelezea Prince Charles kuhusu hatua ambazo zimekuwa zinachukuliwa na Serikali yake kupambana na ujagili dhidi ya tembo na faru ikiwamo Operesheni Maalum – Operesheni Tokomeza -ambayo ilifanyika hivi karibuni kuwasaka na kukabiliana na wafanya biashara haramu ya meno ya tembo. 
 Rais Kikwete amemwambia Prince Charles kuwa pamoja na kuchunguza malalamiko yaliyotolewa na makundi mbali mbali ya watu kuhusu operesheni hiyo ya kwanza, bado operesheni hiyo itaendelea kwa sababu ni muhimu kulinda wanyamapori dhidi ya majangili. “Imefika mahali ambako tunahitaji kuchukua hatua kali. 
Wakati wa Uhuru wetu kulikuwepo na tembo kiasi cha 350,000 lakini ilipofika mwaka 1989 idadi hiyo ilikuwa imepungua na kubakia 55,000. Hata hivyo, baada ya operesheni maalum na kubwa, idadi hiyo ilikuwa imeongezeka hadi kufikia 110,000 kabla ya kuanza wimbi jipya la ujangili mwaka 2010. Operesheni lazima iendelee,” Rais Kikwete amemwambia Prince Charles. 
 “Tusaidie kufunga na kuvuruga hili soko la bidhaa za wanyampori. Operesheni ya sasa imethibitisha kuwa mtandao wa uwindaji haramu na biashara haramu ya meno ya tembo na faru ni mkubwa na watu wengi wanahusika, lakini kinachovuruga zaidi ni kwamba lipo soko la uhakika la meno ya tembo.” 
 Prince Charles amemweleza Rais Kikwete kuhusu hatua ambazo anakusudia kuzichukua kukabiliana na hali hiyo, ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano mkubwa wa wakuu wa nchi na Serikali Februari 13, mwakani na kufanya mkutano mwingine mkubwa na vyombo vya habari kutoka pote duniani mwakani. 
 “Nakusudia pia kutumia wasanii nyota mbali mbali duniani kuendesha kampeni ya kuielimisha dunia kuhusu athari za biashara hiyo haramu kwa sababu asilimia kubwa ya mapato ya ujangili inasaidia kugharimia vikundi vya kigaidi duniani.” 

 

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika kikao cha ufunguzi cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola jijini Colombo Srilanka leo asubuhi.kushoto ni Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague.


Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya
leo, Ijumaa, Novemba 15, 2013, alikuwa miongoni mwa Wakuu wa Nchi Wanachama wa
Jumuiya ya Madola 53 walioshiriki katika sherehe kubwa na za kufana za Mkutano
huo wa siku tatu.

 

Sherehe
hizo zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Nelum Pokuna Mahinda Rajapaksa
mjini Colombo, Sri Lanka, ziliendelea kwa karibu saa mbili kuanzia saa nne
kamili asubuhi.
Miongoni
mwa viongozi ambao walizungumza kwenye sherehe hiyo ya ufunguzi ni Rais wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka, Mheshimiwa Mahinda
Rajapaksa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mheshimiwa Kamalesh Sharma.
Mrithi
wa Kiti cha Ufalme wa Uingereza Prince Charles ndiye amefungua rasmi Mkutano
huo kwa niaba ya Mama yake, Malkia Elizabeth ambaye ni Mkuu wa Jumuiya ya
Madola. Malkia Elizabeth hakuweza kuhudhuria Mkutano huo.
Mara
baada ya ufunguzi huo uliopambwa na ngoma za kuvutia sana ukiwamo muziki wa
vijana na maonyesho ya watoto wa shule ambao walizunguka Ukumbi wa Mikutano,
wakuu hao walihamia kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kumbukumbu wa Bandaranaike kwa
ajili ya kuanza vikao rasmi.

 

Wakati
wa chakula cha mchana, viongozi hao walihudhuria hafla rasmi iliyoandaliwa na
Mheshimiwa Sharma na baadaye jioni wamehudhuria Chakula cha Usiku
kilichoandaliwa na Prince Charles na mkewe, The Duchess of Cornall kwenye
Hoteli ya Cinnamon Lakeside.
 


Imetolewa na; 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, 
Ikulu, DAR ES SALAAM. 
 15 Novemba, 2013

 

CHOGM 2013 officially kicks off

Official photograph at the Opening Ceremony of the Commonwealth Heads of Government Meeting (CHOGM) taken at the Nelum Pokuna, Mahinda Rajapaksa Theatre, Colombo, today November 15, 2013.  President Jakaya Mrisho Kikwete is standing 3rd left, front role.  
(Photo courtesy of the Commonwealth Secretariat)
By Tagie Daisy Mwakawago 

Colombo, Sri Lanka

The Sri Lankan President Mahinda Rajapaksa officially inaugurated the 2013 Commonwealth Heads of Government Meeting (CHOGM) this morning, an event that was widely attended by world dignitaries that included Tanzania President Jakaya Mrisho Kikwete.  

The event was held at the Nelum Pokuna Mahinda Rajapaksa Theatre in Colombo City, under the main theme of ”Growth with Equity; Inclusive Development.” 

In response to the foreign media questions about world leaders attendance, the Sri Lankan President said that he welcomed the international community to ascertain the ground situation and that his country has nothing to hide from the international community.  

“The country is on the right path to development, after putting an end to continuous brutal killings and bomb blasts by terrorists,” said President Rajapaksa during the pre-CHOGM press conference held yesterday November 14 at the Bandaranaike Memorial International Conference Hall in Colombo City. 

The Sri Lankan President further explained that his Government will not hesitate to take any action against anybody who violates human rights. “My country is committed to uphold Commonwealth values of democracy, rule of law and good governance in the shared vision of bringing better opportunities for people around the world,” said President Rajapaksa.   

He further noted the need for his Government to address other challenges such as the role of civil society in development, public-private partnership for wealth creation and enhancing the participation of youth in development and international trade. 
Meanwhile, other dignitaries from cross paths of the world have arrived in numbers since yesterday November 14, to the latter of  Presidents of Rwanda, South Africa and Cyprus, Vice Presidents from Malawi and Nigerian, Prime Ministers from New Zealand, Pakistan and Malaysia, as well as Prince Charles of the Wales who is here on behalf of his mother, Queen Elizabeth II.  Prince Charles is accompanied by wife Lady Camilla Parker Bowles, the Duchess of Cornwall.
Tanzania delegation, led by President Kikwete has participated in the Commonwealth Leaders’ meeting, the Business Forum, the Youth Forum and the two roundtable discussions with topic of opportunities available in Tanzania and how public and private sectors can collaborate to strengthen economic cooperation.
On the same margin of CHOGM week, the Public Administration and Home Affairs Ministry of Sri Lanka has put a request towards its citizens to hoist the National Flag of their country, in commemoration of the Commonwealth summit and the third anniversary of the second term of their President.  The said notice also requests the commemoration to begin November 14 to 19, 2013 when CHOGM ends.

Rais Kikwete akutana na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa jijini Colombo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa alipomtembelea kwa mazungumzo kwenye jengo la Temple Trees jijini Colombo Novemba 14, 2013 kabla ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya madola mwaka huu (CHOGM 2013).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati alipomtembelea Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa (mwenye nguo nyeupe) kwa mazungumzo kwenye jengo la Temple Trees jijini Colombo Novemba 14, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa wakati alipomtembelea kwenye jengo la Temple Trees jijini Colombo Novemba 14, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Mwenyeji wake,Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa pindi alipokuwa akiondoka kwenye jengo la Temple Trees jijini Colombo Novemba 14, 2013 mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.PICHA NA IKULU.

HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ALIYOITOA BUNGENI KUHUSU JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI, 7 NOVEMBA, 2013, DODOMA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride maalum kabla ya kulihutubia Bunge mjini Dodoma jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha Wageni kwenye Ofisi ya Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda (kushoto) huku Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akishuhudia.
Spika wa Bunge Anna Makinda akimaribisha Rais Kikwete kulihutubia Bunge.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.
Rais Wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal wakufuatilia hotuba ya Rais Kikwete kwa makini.
Baadhi ya Wabunge na Mawaziri wakifatilia Hotuba ya Mh. Rais.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Anna Makinda akimsindikiza Rais Kikwete nje ya Bunge baada ya kulihutubia leo mjini Dodoma.
Rais wa Muungano wa Jamhuri ya Tanzania ,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiwa katika picha ya Pamoja na Wabunge Baada ya Rais Kulihutubia Bunge mjini Dodoma.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta na kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe.Freeman Mbowe baada ya Rais kulihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.
Spika Mstaafu Pius Msekwa, Jaji Mkuu Othman Chande na Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal wakimpongeza Rais Kikwete baada ya kulihutubia Bunge leo mjini Dodoma.Picha na Freddy Maro.IKULU.

Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

 Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;

Mheshimiwa Mizengo Pinda, Waziri Mkuu;

Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri;

Mheshimiwa Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni;

Waheshimiwa Wabunge;

Mabibi na Mabwana;

 

          Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kukubali ombi langu na kutenga muda wenu ili niweze kuzungumza na Wabunge wa Bunge lako Tukufu kuhusu masuala muhimu kwa uhai, ustawi na maendeleo ya nchi yetu na watu wake.

Mheshimiwa Spika;

          Nimeambiwa kuwa taarifa ilipotolewa kuwa ninaomba kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wabunge, kumekuwepo na dhana mbalimbali.  Wapo waliodhani kuwa nakuja kuzungumzia mchakato wa kuunda Katiba mpya na hasa matukio ya wiki chache zilizopita.   Wapo waliodhani nakuja kuzungumzia “Operesheni Tokomeza”.  Tena wapo waliokwenda mbali na kufikiria kuwa nakuja kuwakaripia Waheshimiwa Wabunge waliotoa maoni yao kuelezea kasoro zilizojitokeza katika utekelezaji wa Operesheni hii muhimu. Na wapo pia waliodhani ninakuja kuzungumzia ushiriki wa majeshi yetu ya Tanzania katika Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa nchini Kongo.

 

Mheshimiwa Spika;

          Hayo si makusudio yangu.  Kinachonileta mbele ya Bunge lako Tukufu ni kuzungumzia Jumuiya ya Afrika Mashariki na mustakabali wa Tanzania katika Jumuiya hiyo.  Lakini, kwa sababu ya umuhimu wa masuala hayo niliyoyataja na rai niliyopewa kuwa niyasemee japo kidogo.  Nimeona ni vyema nifanye hivyo.

Mheshimiwa Spika;

  Kuhusu mchakato wa Katiba mpya, napenda kusema kuwa tumefikia hatua nzuri katika utekelezaji wake.  Kama mjuavyo Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekamilisha, kwa mafanikio, hatua ya mwanzo ya kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu Katiba wanayoitaka.  Pia walishatoa Rasimu ya Kwanza ya Katiba na kukamilisha mchakato wa Mabaraza ya Katiba.  Kinachosubiriwa kwa hamu na sisi wote, ni Rasimu ya Pili ya Katiba ambayo inatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 15 Desemba 2013 au kabla ya hapo.

Mheshimiwa Spika;

          Kwa upande wa Bunge lako Tukufu, tunategemea kupata mambo mawili kutoka kwenu yatakayowezesha mchakato kutekelezwa vizuri katika hatua zinazofuata.  Jambo la kwanza ni kutungwa kwa Sheria ya Kura ya Maoni na pili kufanyika kwa marekebisho ya nyongeza ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu Bunge Maalum ili kuboresha utekelezaji wake.  Baada ya Bunge kukamilisha kazi yake hiyo itafuatia uteuzi wa Wajumbe wa Bunge Maalum ili kazi ya kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba ifanyike na kutupatia Rasimu ya Mwisho. Rasimu ambayo ikikubaliwa na wananchi katika Kura ya Maoni itakayofanyika wakati wo wote mwakani, tutakuwa tumepata Katiba Mpya.  Hivi sasa katika Serikali tunaendelea kufanya tafakuri na tunachukua hatua za kuwezesha Bunge Maalum na Kura ya Maoni kufanyika kwa mafanikio.

 

Operesheni Tokomeza

Mheshimiwa Spika;

          Napenda kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge wa Bunge lako Tukufu kuwa sikukasirishwa na maoni yao kuhusu madai ya kuwepo kasoro katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza. Shabaha ya Operesheni hii ni kuokoa maliasili za misitu na wanyamapori dhidi ya uvunaji haramu ambao umefikia kiwango kinachotishia kutoweka kwa raslimali hizo.  Kwa kweli hali inatisha.  Miti inakwisha na ndovu na faru wanaangamia. 

 

Mheshimiwa Spika;

          Wakati, tunapata Uhuru Tanzania ilikuwa na ndovu waliokadiriwa kuwa takribani 350,000.  Lakini, kwa sababu ya ujangili uliokithiri katika miaka ya 1970 na 1980  ilipofika mwaka 1989 kulikuwa na ndovu wapatao 55,000 tu.  Ilipofikia hali hiyo Serikali ikaanzisha Operesheni Uhai iliyohusisha Jeshi la Ulinzi na kuongozwa na Meja Jenerali  John Walden (ambaye sasa ni marehemu) kuendesha mapambano dhidi ya majangili. Kutokana na hatua hiyo na uamuzi wa Shirika linalosimamia biashara ya wanyama walioko kwenye hatari ya kutoweka (CITES) kupiga marufuku biashara ya pembe za ndovu duniani, idadi ya ndovu nchini iliongezeka na kufikia 110,000 mwaka 2009.

 

Tumewaomba Fankfurt Zoological Society ambao ni wabia wetu katika uhifadhi wa wanyama pori kwa miaka mingi wafanye sensa maalum ya ndovu katika Hifadhi ya Selous na kote nchini ili tujue hali halisi ikoje.  Kazi hiyo inaendelea hivi sasa.

 

Mheshimiwa Spika; 

  Baada ya mwaka 2009 kumezuka wimbi jipya, tena la nguvu kubwa, la kuua ndovu na faru nchini na kwingineko katika Bara la Afrika ambako wanyama hao wapo.  Idadi kubwa ya meno ya ndovu yaliyokamatwa na yanaoendelea kukamatwa nchini na kwingineko duniani inathibitisha ukweli huo.  Kwa mfano, kati ya mwaka 2010 na Septemba, 2013, hapa nchini, kwa jitihada zetu vipande 3,899 vya pembe za ndovu vyenye uzito wa kilo 11,212 na vipande 22 vya pembe za ndovu zilizochakatwa zenye uzito wa kilo 3,978 vilikamatwa.  Aidha, katika kipindi hicho vipande 4,692 vya pembe za ndovu vilivyotokea Tanzania vyenye uzito wa kilo 17,797 vilikamatwa nje ya nchi.     

 

Mheshimiwa Spika;

          Kama nilivyokwisha sema hapo awali matatizo ya kuuawa kwa wingi kwa ndovu na faru lipo pia katika nchi nyingine Afrika zenye wanyama hao.   Nchi za Gabon, Kenya, Afrika ya Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Uganda, Zimbabwe, Zambia na nyinginezo nazo zinakabiliwa na matatizo kama yetu.  Tatizo limekuwa kubwa kiasi cha kuifanya Jumuiya ya Kimataifa kushtuka na kuamua kuingilia kati kwa namna mbili.  Kwanza kuunga mkono juhudi za uhifadhi wa ndovu na faru katika nchi zenye wanyama hao.  Na, pili, kuchukua hatua thabiti kudhibiti biashara ya meno ya ndovu duniani.  Ni ukweli ulio wazi kuwa kama hakutakuwepo na wanunuzi wa meno ya ndovu na faru hakuna ndovu au faru atakayeuawa.

Mheshimiwa Spika;

 Kutokana na ukweli ulivyo uamuzi wetu wa kuendesha Operesheni Tokomeza ni sahihi kabisa.  Manufaa yaliyopatikana baada ya Operesheni Uhai ya mwaka 1989 yanatupa imani kuwa na safari hii pia tutafanikiwa.  Tusipochukua hatua kama hii sasa ni sawa na kuwapa kibali majangili waendelee kumaliza ndovu na faru nchini.  Hakika wanyama hao watakwisha.  Itakuwa ni aibu kubwa kwetu na historia itatuhukumu vibaya.

 

Mheshimiwa Spika;

          Tumeyasikia maelezo ya Wabunge kuhusu kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.  Nawaahidi kuwa tutayafanyia kazi.  Serikali imeahirisha kwa muda Operesheni hii ili kujipa muda wa kurekebisha kasoro hizo na kujipanga upya.  Watendaji wasiokuwa waadilifu na wale wasiokuwa waaminifu wataondolewa.  Halikadhalika, kasoro za kimfumo nazo zitasahihishwa ili tutakapoanza upya Operesheni itekelezwe kwa mafanikio yaliyokusudiwa.

 

Mheshimiwa Spika;

          Miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa kwa uchungu ni ukamataji wa mifugo iliyokutwa kwenye mapori ya hifadhi za wanyama na vitendo vibaya walivyofanyiwa wenye mifugo na mifugo yenyewe.  Narudia kusisitiza kuwa taarifa zote hizo zitafanyiwa kazi na waliohusika watachukuliwa hatua zipasazo.  Pamoja na hayo, napenda kuwakumbusha ninyi watunga sheria wetu kuwa sheria ya hifadhi za wanyamapori hairuhusu mifugo kuchungwa katika maeneo ya hifadhi. 

 

Naomba tuwakumbushe wananchi tunaowaongoza wajiepushe na kufanya hivyo.  Ni uvunjifu wa Sheria za nchi.  Naomba pia, wananchi waelimishwe ili wajue kuwa wakifanya hivyo na kukutwa katika maeneo hayo na mifugo yao kuna adhabu iliyotamkwa kwenye sheria.   Hivyo tusiwalaumu wala kuwaona maafisa wanyamapori kuwa ni watu wabaya.  Wanatekeleza Sheria iliyotungwa na Bunge hili.  Pale wanapotenda visivyo tuseme, watawajibishwa ipasavyo.

 

Jeshi la Umoja wa Mataifa Kongo

Mheshimiwa Spika;

          Mapema mwaka huu (2013) Umoja wa Mataifa uliomba nchi yetu ichangie kikosi kimoja cha wanajeshi katika Brigedi Maalum iliyoundwa na Umoja huo kuongeza nguvu ya kudhibiti waasi Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.  Lengo la msingi ni kuiwezesha nchi hiyo kupata amani ya kudumu ambayo imekosekana kwa muda mrefu kutokana na kuibuka kwa uasi mara kwa mara.

 

Mheshimiwa Spika;

          Tulikubali, kwani hata kabla ya kuombwa na Umoja wa Mataifa tulishakubali maombi kama hayo yaliyotolewa kwenye Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu.  Ni miezi saba (tangu Aprili) sasa tangu wanajeshi wetu waende Kongo na wamekuwa wanatekeleza majukumu yao vizuri tena kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu.  Sifa hiyo kwa wanajeshi wetu imekuwa inatolewa na viongozi wa juu wa Umoja wa Mataifa, viongozi wa juu wa Jeshi la Umoja wa Mataifa Kongo (MONUSCO) na viongozi wa juu wa Serikali ya Kongo.

 

Mheshimiwa Spika;

          Majeshi ya Umoja wa Mataifa hupewa majukumu na mamlaka ya namna mbili.  Yapo yanayopewa jukumu la kulinda amani tu.  Wanajeshi wake huwa hawapewi majukumu ya kimapigano na hata pale wanaposhambuliwa wanatakiwa kujihami tu.  Kwa kawaida majeshi yenye jukumu hili hupelekwa mahali ambapo kumekuwepo na makubaliano ya kuacha mapigano.  Wanapelekwa kusaidia kuona Mkataba unatekelezwa ipasavyo. 

 

Aina ya pili ni ile ya majeshi yanayopelekwa mahali ambapo hakuna amani hivyo wanapewa jukumu la kuchukua hatua za kufanya amani ipatikane.  Majeshi haya hupewa mamlaka ya kutumia nguvu ya kijeshi dhidi ya wanaosababisha amani ikosekane kama ni lazima kufanya hivyo.  Maana yake ni kwamba wanayo ruhusa kuingia katika mapigano dhidi ya watu au vikundi vinavyovuruga amani.  Tofauti na wenzao wa kundi la kwanza, wanajeshi wa kundi la pili wako kwenye hatari zaidi ya kupoteza maisha au kujeruhiwa kuliko wenzao ingawaje wapo wengi nao wameuawa na kujeruhiwa.

 

Mheshimiwa Spika; 

Wanajeshi wetu wamekwenda Kongo chini ya utaratibu huu wa pili ambao unahusu kuingia kwenye mapigano dhidi ya waasi kama hapana budi kufanya hivyo.   Wametekeleza majukumu yao vyema na kwa ujasiri mkubwa na weledi wa hali ya juu. Bahati mbaya tumepoteza vijana wetu watatu shupavu.  Daima tutawakumbuka na tutawaenzi ipasavyo mashujaa wetu hawa.  Tuzidi kuwaombea kwa Mola awape mapumziko mema.  Ameen.

 

Wakati huo huo, Mheshimiwa Spika, napenda kutumia nafasi hii kumpongeza Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mafanikio ya kihistoria waliyoyapata hivi majuzi dhidi ya waasi wa M23.  Tunamtakia yeye na wananchi wa Kongo kila la heri katika kazi ngumu iliyo mbele yao ya kujenga upya eneo hilo na kujenga mahusiano mapya miongoni mwa watu wa Kongo.  Pia nawapongeza sana wanajeshi wa Brigedi Maalum ya Umoja wa Mataifa kwa kazi nzuri waliyoifanya iliyowezesha mafanikio kupatikana.   Wanajeshi hao ni kutoka Afrika Kusini, Tanzania na Malawi wanaoongozwa na Brigedia Jenerali James Aloisi Mwakibolwa wa JWTZ.

 

Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mheshimiwa Spika;

          Kama nilivyosema awali, haya mambo matatu siyo hasa makusudio yangu nilipoomba kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wabunge wetu.  Nimeyachomekea tu kwa sababu ya umuhimu wake katika jamii kwa wakati tulio nao.  Jambo lililonileta hapa leo ni kuzungumzia hali ilivyo sasa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na nafasi ya Tanzania katika Jumuiya hiyo.  Nimeona nifanye hivyo kutokana na maswali mengi ambayo Watanzania wanajiuliza kufuatia matukio ya hivi karibuni ya viongozi wa nchi tatu wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaani Uganda, Rwanda na Kenya kukutana bila ya ushiriki wa viongozi wa Tanzania na Burundi.  Viongozi wenzangu hao wamefanya mikutano mitatu yaani: tarehe 24-25 Juni, 2013 mjini Entebbe, Uganda; tarehe 28 Agosti, 2013 mjini Mombasa, Kenya; na tarehe 28 Oktoba, 2013 mjini Kigali, Rwanda.

 

Mheshimiwa Spika;

          Naomba kwanza niweke wazi jambo moja, kwamba nchi mbili wanachama au zaidi hazikatazwi kuwa na makubaliano ya ushirikiano katika kufanya mambo mbalimbali.  Hata sisi Tanzania tunao ushirikiano wa namna hiyo na nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.  Lakini, nchi wanachama zinatakiwa kufanya hivyo kwa yale mambo ambayo hayako kwenye shughuli za Jumuiya kwa maana kwamba hayamo katika Mkataba au Itifaki au hakuna uamuzi wa msingi uliofanywa na vikao au taasisi za Jumuiya kuyashughulikia.  Pia, tunaweza kufanya hivyo kwa mambo ambayo yalishaamuliwa na Jumuiya yatekelezwe na ruhusa imetolewa kwa nchi yo yote iliyokuwa tayari kutekeleza ama peke yake au kwa kushirikiana na nchi nyingine.

 

Mheshimiwa Spika;

          Kwa mujibu wa matamko ya pamoja (Communique) yaliyotolewa baada ya mikutano hiyo, kuna mambo yapatayo manane ya msingi yaliyoamuliwa kufanywa na nchi hizo kwa lengo la kuendeleza utengamano wa nchi hizo wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.  Mambo hayo ni haya yafuatayo: 

(1)              Kujenga reli ya kisasa kutoka Mombasa hadi Kampala,  Kigali  na Bujumbura.

(2)             Ujenzi wa Bomba la Mafuta la kutoka Kenya hadi Uganda na Sudani ya Kusini.

(3)             Kujenga Kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Uganda.

(4)             Kuanzisha Himaya Moja ya Ushuru  wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutekeleza vipengele vyote;

(5)             Kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki na kwamba itaundwa Kamati ya kuandaa rasimu ya Katiba ya Shirikisho.

(6)             Kuharakisha uanzishwaji wa Visa ya pamoja ya Utalii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (Single East African Community Tourist Visa); 

(7)             Kuandaa utaratibu wa kutumia vitambulisho vya taifa kama hati ya kusafiria katika nchi zao; na

(8)             Kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme.

 

 

Mheshimiwa Spika;

          Ni dhahiri kwamba orodha hiyo imechanganya mambo yale ambayo ni ya Jumuiya na yale yasiyo ya Jumuiya.  Kwa mfano, mambo manne kati ya hayo manane hayamo kwenye masharti ya kutokufanyika bila ya kuihusisha au kupata ridhaa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.  Jambo la kwanza ni uzalishaji na usambazaji wa umeme.  Ni kweli kwamba tunao mkakati wa kuwa na akiba ya pamoja ya nguvu ya umeme (East African Power Pool).  Hata hivyo, bado jukumu la kuzalisha na kusambaza umeme huo limeachiwa nchi wanachama zenyewe kuamua.  Lakini, hivi ndugu zetu hawa wanao muhali kuishirikisha Tanzania katika mpango ambao kimsingi umebuniwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo sote ni wanachama?    

 

Jambo la pili, ni ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Uganda.  Hili si suala la Jumuiya bali la nchi ya Uganda kuamua yenyewe peke yake au kwa kushirikiana na wadau wengine.  Rais Yoweri Museveni alituarifu mpango huo na sote tuliupokea kwa furaha kwamba sasa tutapata mafuta karibu na nyumbani.   Alitualika kushiriki katika ujenzi wake sijui sasa amebadili mawazo kwamba Tanzania siyo muhimu.

 

Mheshimiwa Spika;

Jambo la tatu ni ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Kenya hadi Sudani ya Kusini na Uganda.  Hili si jambo linalobanwa na masharti ya Jumuiya. Ni juu ya nchi hizi tatu kuamua kufanya ili kuwezesha mafuta yao kufika kwenye masoko.  Hata hivyo, nimeambiwa kuwa Jumuiya imeshazungumzia bomba la mafuta kutoka Eldoret hadi Uganda, Rwanda na Burundi kuwa nalo lifike Tanzania kupitia upande wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.  Inaelekea mpango huo sasa haupo maana hatujausikia kutajwa katika ujenzi wa bomba hilo. 

Mheshimiwa Spika;

Jambo la nne ni ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mombasa – Kampala – Kigali – Bujumbura.  Hili nalo hatuna tatizo nalo.  Si mradi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni jambo lililo chini ya mamlaka ya nchi wanachama husika.  Hata hivyo, ni vyema kutambua ujenzi wa miundombinu ya reli, barabara na usafiri wa anga na majini kuunganisha nchi za Afrika Mashariki ni miongoni mwa mambo ya kipaumbele cha juu yanayoshughulikiwa na Jumuiya yetu.  Jumuiya hutengeneza mikakati ya pamoja na ndiyo maana tuna East African Railway Masterplan, tuna East African Road Network, na tuna Lake Victoria Development Programme kwa ziwa Victoria. 

Kwa ajili hiyo, nilitegemea kuwa reli ya kutoka Mombasa hadi Kigali na Juba ingekuwa na tawi linalounganisha reli hiyo na reli ya Tanzania kama ilivyo reli ya Moshi – Voi – Taveta aliyotuachia mkoloni. Tulitegemea hivyo kwa minajili ya kuunganisha soko la Afrika Mashariki ambapo naamini Tanzania ni mdau muhimu.  Lakini inaelekea kwa maoni ya wenzetu hivyo sivyo. 

 

Mheshimiwa Spika;

Lazima nikiri kuwa inashangaza na tunayo kila sababu ya kuuliza kwa nini wenzetu wameamua kufanya hivi.  Kumetokea nini toka tukutane pale Arusha Aprili 28, 2013 na Juni 24, 2013 walipokutana kuamua kufanya mambo ya kujenga na kuimarisha utengamano wa Afrika Mashariki kwa kubaguana,  Haijawahi kuwa hivi kabla.   

 

Mheshimiwa Spika;

          Katika mambo manne yaliyosalia ambayo yaliamuliwa na kuwekewa utaratibu wake wa utekelezaji na Jumuiya ya Afrika Mashariki mawili hatuna maneno nayo.  Mambo hayo ni matumizi ya vitambulisho vya taifa kama hati ya kusafiria na Visa ya Pamoja ya Utalii kwani tuliamua kwa pamoja kuwa nchi wanachama zilizokuwa tayari waanze.  Lakini, kwa upande wa kuanzishwa kwa Himaya Moja ya Ushuru wa Forodha (Single Customs Territory) na Shirikisho la Afrika Mashariki tunadhani wenzetu wamekiuka uamuzi wetu wa pamoja.

 

Mheshimiwa Spika;

          Katika Mkutano Maalum wa 11 wa Wakuu wa Nchi wanachama uliofanyika tarehe 28 Aprili, 2012 Jijini Arusha, tulipokea na kuridhia mapendekezo ya kuanzisha Himaya Moja ya Ushuru wa Forodha (Single Customs Territory).  Kwa mujibu wa mapendekezo hayo kila nchi mwanachama itasimamia shughuli zake za kiforodha na kukusanya mapato yake kama ilivyo sasa.  Hata hivyo, kwa bidhaa zinazopitia nchi moja kwenda nchi nyingine mwanachama, ukaguzi na ukusanyaji wa mapato utafanyika katika kituo cha kwanza bidhaa hizo zinapoingilia.  Mapato hayo yatawasilishwa kwa nchi husika baada ya kuthibitisha kuwa bidhaa zilivuka mpaka. 

 

Mheshimiwa Spika;

Kutokana na uamuzi huo, Wakuu wa Nchi waliagiza Baraza la Mawaziri kuunda Kikosi Kazi cha kujadiliana na kuandaa utaratibu wa utekelezaji wa mfumo huo.  Taarifa ya kikosi kazi inatakiwa kutolewa katika Mkutano wa 15 wa Wakuu wa Nchi utakaofanyika Kampala, Uganda tarehe 30 Novemba, 2013.  Iweje leo nchi tatu wanachama ziamue peke yao kuanza kutekeleza?  Wanatekeleza nini na kwa nini wafanye hivyo? 

 

 

 

Mheshimiwa Spika;

          Kuhusu Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki hadithi yake inafanana na hii ya Himaya ya Forodha.  Katika Mkutano wa 14  wa Wakuu wa Nchi wanachama uliofanyika tarehe 30 Novemba, 2012, Nairobi, tulipokea taarifa ya hatua iliyofikiwa kuhusu mchakato wa kutaka kuanzishwa kwa Shirikisho.   Mkutano huo uliagiza nchi wanachama kujadiliana zaidi kuhusu mpango kazi wa kufikia Shirikisho la Kisiasa na mpango wa kutekeleza mapendekezo mengine yaliyotolewa na Timu ya Wataalamu.  Inategemewa kuwa Baraza la Mawaziri litawasilisha mapendekezo ya majadiliano hayo katika Mkutano wa 15 wa Wakuu wa Nchi mwezi Novemba, 2013.  Iweje leo wenzetu hawa waamue kuanzisha mchakato wao wa kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki.   

 

Mheshimiwa Spika;

     Kwa kweli huwa najiuliza maswali mengi na kukosa majibu kuhusu nini kinachoendelea kufanywa na viongozi wenzangu watatu na kwa nini!  Nakosa majibu ya uhakika.  Je wenzetu wamekosa imani na Jumuiya ya Afrika Mashariki na je wanataka kuunda yao?  Je wanaichukia nchi yetu na hivyo wameamua kutufanyia vitimbi tutoke!  Au sijui wanachuki na mimi!  Napenda kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge kuwa hatuna mpango wa kutoka (kama vijana wasemavyo hatoki mtu hapa).  Tupo na tutaendelea kuwepo!  

 

Mheshimiwa Spika;

          Tanzania haijafanya jambo lo lote baya dhidi ya Jumuiya au nchi yo yote mwanachama.  Na ukweli ni kwamba ni mwanachama mvumilivu, mtiifu na mwaminifu kwa Jumuiya.  Tunatimiza ipasavyo wajibu wetu kwa Jumuiya na kushiriki kwa ukamilifu katika ujenzi wake na utengamano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.  Sabahu ya wenzetu watatu kuamua kufanya mambo yahusuyo Jumuiya yetu peke yao kwa kweli haieleweki.   

 

Mheshimiwa Spika;

Tunasikia eti kuwa baadhi yao walipoulizwa kwa nini wengine hatupo wakasema kuwa wao wametangulia na sisi tutakapokuwa tayari tutajiunga.  Yaani wana Umoja wa Waliokuwa Tayari (Coalition of the Willing).  Hivi ni nani hayuko tayari (who is not willing?)  Haiwezekani watu waitane wenyewe bila ya kutualika halafu wadai kuwa wao ndiyo wako tayari na kujenga dhana kuwa sisi wasiotualika ndiyo ambao hatuko tayari.  Madai hayo hayana ukweli.  Ni vyema waseme ukweli.  Kama walitualika tukakataa ndiyo wanaweza kusema hayo.        

 

Mheshimiwa Spika;

Kumekuwepo na madai kutoka kwa baadhi ya wenzetu, eti kwamba Tanzania haina moyo wala dhamira ya dhati ya kuendeleza  utengamano wa Afrika Mashariki.  Kwa sababu hiyo inasemekana eti nchi yetu imekuwa kikwazo kwa maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba Tanzania tunawachelewesha wengine kupiga hatua za haraka.  Wanadai kama siyo hivyo Jumuiya ya Afrika Mashariki ingekuwa mbali kwa maendeleo. Maneno hayo yamekuwa yanarudiwa au kujirudia mara nyingi kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu wa Afrika Mashariki na hata kwingineko duniani waamini hivyo.    

 

Mheshimiwa Spika;

Napenda kusema kwa dhati ya moyo wangu kwamba madai hayo hayana ukweli wo wote.  Isitoshe hata sababu zinazotolewa kuthibitisha ukweli wake hazina mashiko.  Hazifanani na ukweli kuhusu Tanzania na Watanzania walivyo.  Tanzania ni muumini wa dhati wa umoja na utengamano wa nchi za Afrika Mashariki na Afrika.  Tumethibitisha hivyo kwa vitendo kwa kuunganisha nchi zetu mbili huru yaani Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika na kuwa taifa moja liitwalo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Muungano wa nchi zetu mbili ndio pekee uliodumu kwa muda mrefu kuliko yote Afrika.  

 

Mheshimiwa Spika; 

 Tanzania ni mwanachama mwaminifu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa maana ya kutekeleza Mkataba ulioanzisha Jumuiya hiyo, kwa Itifaki zake na maamuzi halali ya vikao na taasisi za Jumuiya.  Kama lipo jambo ambalo hatujalifanya ilivyotakiwa itakuwa ni kwa sababu za msingi na siyo kwa sababu ya kupuuza Jumuiya. Tunaithamini sana Jumuiya na tumeipa kipaumbele cha juu.  Hatuwezi kuhangaika kwa gharama kubwa ya muda wetu, fedha zetu na kutoa mchango wa hali na mali kuianzisha, kujenga na kuifikisha Jumuiya hapa ilipo halafu tuwe ni watu tunaoongoza kutokuipenda na kudhoofisha maendeleo na ustawi wake. Ni maneno ya kushangaza na wala hayaingii akilini.  Ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi.

 

Mheshimiwa Spika;

          Nionavyo mimi msimamo wetu kuhusu kuharakisha Shirikisho na masuala ya ardhi, ajira, uhamiaji, pengine ndiyo yanayotuletea hisia zisizokuwa sahihi juu yetu.  Mimi siamini kama kuna mengine.  Hata hivyo, napata taabu kuamini kwamba kutofautiana kwa mawazo katika mambo hayo kutapelekea baadhi ya wenzetu wasipende hata kushirikiana nasi kwa mambo ambayo hayana matatizo na tumekuwa tunashirikiana vizuri. 

 

 

Mheshimiwa Spika;

Tanzania imekuwa inawasihi wanachama wenzetu kuwa tujenge Jumuiya yetu hatua moja baada ya nyingine kama ilivyo kwenye Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.  Hatuna tatizo la kuongeza kasi ya ujenzi wa Jumuiya lakini tusivuke hatua yo yote.  Tusiende kasi ya kupindukia. Mkataba unaelekeza tunaanza na Umoja wa Forodha, inafuatia Soko la Pamoja kisha Umoja wa Kifedha na hatimaye Shirikisho la Kisiasa. 

 

Mheshimiwa Spika;

          Ni kweli kabisa hatukuunga mkono kuharakisha Shirikisho la Kisasa kabla ya kukamilisha baadhi ya hatua.  Na, tulifanya hivyo kwa nia njema ya kutaka Shirikisho lijengwe juu ya msingi imara.  Na, msingi huo si mwingine bali utengamano wa kiuchumi kwa maana ya Umoja wa Forodha, Soko la Pamoja na Umoja wa Kifedha zilizojengeka vizuri na kufanya kazi ipasavyo na kunufaisha wanachama wote sawia.

 

Mheshimiwa Spika;

 

          Lazima tutambue ukweli kuwa kunufaika kiuchumi ndicho kichocheo kikubwa cha nchi kujiunga na kuendelea kuwa mwanachama wa Jumuiya yetu.  Kama mambo ya kiuchumi yakipangika vizuri na kila nchi ikanufaika sawia, unajenga msingi imara kwa Shirikisho la Kisiasa kustawi na kudumu.  Kama ngazi hizi tatu za awali hazitashughulikiwa vizuri na nchi wanachama zikahisi hazinufaiki ipasavyo, Shirikisho litayumba au kuyumbishwa hivyo kudumu kwake kutakuwa kwa mashaka.

 

 

 

Mheshimiwa Spika;

          Tanzania ni kati ya zile nchi zinazotaka ngazi zote za mchakato wa utengamano zitekelezwe moja baada ya nyingine bila kuruka hata moja.  Kwa msimamo na mtazamo wetu,  Shirikisho iwe ndiyo hatua ya mwisho.  Na huo siyo msimamo wangu au wa Serikali peke yake, ndiyo msimamo wa Watanzania walio wengi.

          Bila ya shaka sote tutakumbuka kuwa mwaka 2006 Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya waliunda Kamati Maalum katika kila nchi kukusanya maoni ya wananchi kuhusu kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki.  Kwa hapa nchini Kamati hiyo iliongozwa na Profesa Samwel Wangwe na katika taarifa yake,  Kamati ilieleza kuwa asilimia 74.4 ya Watanzania wanaunga mkono kuwepo kwa Shirikisho lakini ni asilimia 25.4 tu ndiyo waliunga mkono kuharakishwa kwake. 

 

Mheshimiwa Spika;

          Takwimu hizi zinaelezea ukweli kuhusu hisia za Watanzania, kuhusu kuwepo kwa Shirikisho na kasi ya utekelezaji wake.  Watanzania wengi sana wanaunga mkono kuwepo kwa Shirikisho la Afrika Mashariki lakini wanataka jambo hilo lisifanywe haraka haraka.  Wanataka lifanywe kwa umakini mkubwa na tuende hatua kwa hatua kama ilivyoainishwa katika Mkataba uliounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Mheshimiwa Spika;

          Sera na msimamo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakwenda sambamba na ile ya wananchi wa Tanzania.  Ndiyo maana tumeafiki mapendekezo ya Kamati ile ya mwaka 2004 iliyoongozwa na Mheshimiwa Amos Wako wakati ule akiwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya.  Kamati hiyo iliundwa kupendekeza namna ya kuharakisha utekelezaji wa mchakato wa utengamano wa Afrika Mashariki.

          Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umetamka muda wa kutekeleza ngazi ya Umoja wa Forodha lakini uko kimya kuhusu ngazi zilizofuata.  Ili kuondoa kasoro hiyo na kwa nia ya kuharakisha Shirikisho Kamati ilipewa jukumu la kutoa maoni na mapendekezo juu ya namna ya kufanya hivyo.  Kamati ilifanya kazi nzuri ya kupata maoni na hisia za watu wa makundi mbalimbali katika nchi wanachama kuhusu ujenzi wa Jumuiya na utengamano.

 

Mheshimiwa Spika;

          Kwa upande wa Tanzania kwa mfano, Kamati ya Mheshimiwa Amos Wako ilitambua hisia za Watanzania kuhusu ardhi na ajira na kupendekezwa kuwa masuala hayo yabaki kwenye mamlaka ya nchi wanachama kuamua.  Kuhusu mchakato wa utengamano Kamati ilipendekeza kwanza kwamba mchakato wa ujenzi wa Umoja wa Forodha uachwe mpaka ufike ukomo wake wa miaka mitano.  Baada ya hapo muda wa kutekelezwa ngazi zinazofuata unaweza kupunguzwa.  Kwa mfano walipendekeza kuwa matayarisho ya kuunda Soko la Pamoja yaanze hata kabla ya mchakato wa Umoja wa Forodha kufika mwisho ili mara wakati huo ukifikiwa Soko la Pamoja linaanze.  Hivyo hivyo mara baada ya ngazi hiyo kuanza matayarisho ya kuanza ngazi ya Umoja wa Kifedha yanaanza.  Ngazi hiyo nayo ikianza matayarisho ya kuunda Shirikisho yanaanza.  Kamati pia imetoa mapendekezo ya namna ya kufikia uamuzi kuhusu Shirikisho kwamba wananchi wa nchi wanachama wataamua kwa kura.  Tukifuata mapendekezo ya Kamati ya Mheshimiwa Amos Wako na wenzake kama tufanyavyo sasa Tanzania haina matatizo nayo.

 

Mheshimiwa Spika;

          Baada ya kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na wana-Afrika Mashariki kuhusu ujenzi wa Jumuiya yao inasikitisha kuona vinafanyika vitendo vinavyoanzisha mivutano kuhusu mambo yaliyokwisha fanyiwa kazi na kuamuliwa.  Tunapata taabu zaidi pale watu wanapobagua wenzao na wanapofanya mambo yanayopingana na Mkataba wa Jumuiya na Itifaki zake.  Kwa kweli kama mwenendo huu hautabadilika sijui mambo yatakuwaje mbele ya safari. 

 

Mheshimiwa Spika;

Nchi yetu inapenda kuona kuwa tunakuwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyo imara na iliyo endelevu.  Jumuiya ambayo inaendeshwa vizuri, mambo yake ni mazuri na nchi zote wanachama na watu wake wananufaika nayo, na hivyo wanaifurahia.  Tanzania haina tatizo na kuharakisha mchakato wa utengamano, lakini tunapata taabu kuruka baadhi ya hatua kabla hazijakamilika.   Tunawaomba wenzetu kuwa makini katika kila hatua tunayochukua.  Bila ya kufanya hivyo,  Jumuiya yetu itakuwa imejengeka katika msingi dhaifu hivyo ustawi na uhai wake utakuwa na changamoto nyingi.  Hatupendi ya mwaka 1977 yatokee tena.

 

Mheshimiwa Spika;

          Napenda kuwahakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushiriki katika shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuimarisha utengamano wa Afrika Mashariki kwa kuzingatia matakwa ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Itifaki zake.   Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa Jumuiya haidhoofiki wala kufa.  Na iwapo itadhoofika au kufa kamwe hatutaki Tanzania inyooshewe kidole kuwa chanzo wala kichocheo chake.  Ndiyo maana, hatutachoka kuzungumza na wenzetu kuhakikisha kuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki inaendelea kustawi. 

Tutaendelea kukumbushana umuhimu wa kufanya mambo yanayojenga na kuepuka yale yanayoweza kubomoa.  Tutakumbushana umuhimu wa kuheshimu matakwa na masharti ya Mkataba ulioanzisha Jumuiya, Itifaki zake na maamuzi halali ya vikao rasmi na asasi za Jumuiya.  Tukifanya hivyo Jumuiya ya Afrika ya Mashariki itadumu, itazidi kustawi na kunufaisha nchi wanachama na watu wake kama yalivyo malengo na madhumuni ya kuundwa kwake.   

Mungu Ibariki Afrika

Mungu Ibariki Tanzania

Idumu Jumuiya ya Afrika Mashariki

 

Mheshimiwa Spika na

Waheshimiwa Wabunge;

 

                   Asanteni sana kwa kunisikiliza.

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WATOA POLE KWA MJANE NA FAMILIA YA BALOZI ISAAC SEPETU LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mjane wa Balozi Isaac Sepetu, Mama Miriam Sepetu, alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kwa mjane huyo na familia ya Marehemu Sepetu aliyefariki jana jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa wanafamilia wa Balozi Isaac Sepetu alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kufuatia msiba Marehemu Sepetu aliyefariki jana jijini Dar es salaam.
Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa Balozi Isaac Sepetu alipokwenda nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kufuatia msiba Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu alipokwenda nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole. Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam. . Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE AAPISHA BALOZI WA TANZANIA NCHINI NIGERIA, KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI, NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO NA KATIBU MTENDAJI BODI YA MISHAHARA NA MASLAHI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Mhe Daniel Ole Njolaay kuwa balozi leo Oktoba 28, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam. Balozi Njolaay amepangwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Nigeria.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mhe Daniel Ole Njolaay baada ya kumuapisha kuwa balozi leo Oktoba 28, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam. Balozi Njolaay amepangwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Nigeria.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Dkt. Bashir Mrindoko kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji leo Oktoba 28, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Dkt. Bashir Mrindoko baada ya kumuapisha kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji leo Oktoba 28, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe. Raphael Leyani Duluti kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika leo Oktoba 28, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mhe Raphael Leyani Duluti baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Chakula na Ushirika leo Oktoba 28, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Tamika Mwakahesya kuwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Maslahi leo Oktoba 28, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mhe Tamika Mwakahesya baada ya kumuapisha kuwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Maslahi leo Oktoba 28, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais wakiwa katika picha ya pamoja na walioapishwa leo kushika nyadhifa mbalimbali Ikulu jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Mhe. Raphael Leyani Duluti kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt. Bashir Mrindoko kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji. toka kulia ni Mhe Daniel Ole Njolaay aliyeapishwa kuwa balozi wa Tanzania nchini nigeria akifuatiwa na Mhe Tamika Mwakahesya aliyeapishwa kuwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Maslahi.PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MGODI WA CHUMA WA LIGANGA,LUDEWA MKOANI NJOMBE

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Meneja mradi wa Maganga Matatitu Resource Development limited Bw. Lawrence Manyama kuhusu mlima huo uliosheheni mashapu ya chuma alipotembelea eneo lenye utajiri wa chuma la Liganga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe leo Oktoba 22, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wawekezaji wa kampuni ya Sichuan Hongda ya China ambao ni wawekezaji katika eneo lenye utajiri wa chuma la Liganga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe leo Oktoba 22, 2013. Kampuni hiyo inatarajiwa kujenga kiwanda cha kufua chuma mapema mwakani kitachajiri watu 32,000 kitakapokamilika.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionesha kilele cha Central Liganga hill ambacho ni mojawapo ya sehemu ambazo kampuni ya Sichuan Hongda ya China itachimba mashapu ya chuma na kuyafua katika kiwanda kikubwa cha kufua chuma kitachoajiri watu 32, 000 katika eneo hilo lenye utajiri wa chuma la Liganga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe leo Oktoba 22, 2013. Kampuni hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi alipoowasili katika uwanja wa mikutano wa Ludewa ambako alihutubia mkutano wa hadhara.PICHA NA IKULU